CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Wednesday, September 29, 2010

JIFUNZE UWIANO WA VIPIMO KITAALAMU ZAIDI


KWA WALE WOTE MNAOPATA SHIDA YA UWIANO WA VIPIMO NAOMBA MSOME VIZURI VIPIMO HIVI KISHA UTACHAGUA UTUMIE KIPIMO KIPI AMBACHO KWAKO NI RAHISI KUELEWA ILI NAWE UWEZE KUFURAHISA MAFUNZO KWA KUTUMIA VIPIMO SAHIHI.

PIA VYOMBO YA KUTUMIA KUPIMIA CHAKULA AU VIMIMINIKA KAMA MAZIWA NA MAFUTA UNAWEZA KUNUNUA KATIKA DUKA LA VYOMBO VYA NYUMBANI ULIZA JUG LA KUPIMIA AU VIJIKO VYENYE VIPIMO UTAPATA VYA CHUMA NA PLASTIKI KWA BEI NAFUU SANA NA VINAPATIKANA KWA URAHISI SANA KOTE DUNIANI.


1 Kijiko kidogo cha chai ni sawa na   6 mili lita.

1 Kijiko kikubwa cha chakula ni sawa na  17 mili lita.

240 gram ni swa na  280 mili lita.

1 kg     =   1,000 g

1/2 kg   =   500 g

1/4 kg   =  250 g

1/8 kg   =  125 g

240 gram  = 16 kijiko kikubwa cha chakula


1 Kijiko kikubwa cha chakula  =  3 Kijiko kidogo cha chai

6 yai zima = 240 gram
10ute wa yai mweupe  = 240 gram
1 ute wa yai wa njano  =  2 Kijiko kikubwa cha chakula

12 hadi 14 ute wa njano wa yai  =  240 gram


LENGO NI KILA MMOJA WETU AWE SAMBAMBA NA MAFUNZO NA AFURAHIE

 

Friday, September 24, 2010

TAARIFA RASMI KWA WAPENZI WOTE WA BLOG

KWA WALE WAPENZI WA DONUT SAMAHANI SANA NILIKOSEA VIPIMO NA NIMESHAREKEBISHA SASA MNAWEZA KUANGALIA UPYA RECIPE NA KUTENGENEZA KWA KUTUMIA RECIPE HIYO KWANI KIPIMO CHA MAZIWA KILIZIDI HII ITAKUA NZURI NA MTAFURAHIA NAOMBA MATOKEO BAADA YA KUTENGENEZA. KWA WASOMI WAPYA WA BLOG HII FUNGUA UPANDE WA KULIA SEHEMU ILIYOANDIKWA MAFUNZO YALIYOPITA UTAIONA.

POLENI SANA WAPENZI WA BLOG HII MLIOTUMA EMAIL KWANGU ILI NIWEZE KUWATUMIA RATIBA NA JINSI YA KUANDAA TAKE AWAY YA WATOTO!

NILIAGIZA BEI ZA VYAKULA DAR ES SALAAM ZIMECHELEWA KUFIKA NATARAJIA KESHO NITAPATA ILI NIFANYIE MAHESABU ILI NIWAONYESHE KILA CHAKULA UTAKACHOTENGENEZA KITAGHARIMU KIASI GANI.

 KISHA NITAWATUMIA SIKU YA JUMA TATU TAR 27.

 NAONA BEI ZA VYAKULA HAZIPISHANI SANA DUNIANA\I KAMA UKIONA MCHELE DOLA1 ULAYA BASI UNAKUA UNAUZWA SH 1300 HADI 1500 TANZANIA.

PILI WALE WOTE MNAOPATA SHIDA KATIKA VIPIMO PIA MTANIANDIKIA EMAIL JUMATATU NIWEZE KUWATUMIA KARATASI  INAYO ONYESHA VIPIMO VYOTE ITAKUA KAZI KWENU MCHAGUE KUTUMIA VIPIMO GANI KIKOMBE, KIJIKO, GRAM AU LITER.
KARATASI HII INATAFSIRI VIPIMO VYOTE TOKA KIMOJA KWENDA KINGINE.

PIA BADO NASUBIRI SANA PICHA ZA VYAKULA MNAVYOTENGENEZA NAHAMU SANA KUONA MAENDELEO YETU TAFADHALI AU KAMA UNA RECIPE YEYOTE ILE UNGEPENDA WATU WAJIFUNZE TOKA KWAKO WE NITUMIE TU KATIKA EMAIL YANGU NI issakesu@gmail.com.

NAWATAKIA KAZI NA SIKU NJEMA

CHEF ISSA



JIFUNZE KUTENGENEZA WALI HUU MAARUFU SANA NCHINI NIGERIA NA GHANA

WALI HUU MAARUFU SANA KAMA JOLLOFU UNALIWA SANA NIGERIA NA GHANA KAA TAYARI KWA RECIPE

MAHITAJI

240 gram ya mchele wowote ule
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia 
1 kijiko kidogo cha chai binzali nyembamba ( cumin seed)

1 kijiko kidogo cha chai unga wa binzali
1/4 kijiko kidogo cha chai unga wa kungu manga (nutmeg powder)
1 kitunguu maji kikubwa 
20 gram kitunguu swaumu
10 gram tangawizi
150 gram uyoga wowote ule
1 au 2  pili pili mbuzi mbichi (sio lazima)
1 kijiko kikubwa cha chakula nyanya ya kopo (tomato paste)
2 nyanya ya kuiva kubwa chop chop 
1 carrot kata vipande vidogo vidogo 
60 gram maharage mabichi
60 gram njegere mbichi 
10 gram chumvi
1 fungu majani ya giligilani (corrienda)


JINSI YA KUPIKA FATA MAFUNZO CHINI KAMA PICHA ZINAVYOONYESHA




Weka katika sufuria au kikaango mafuta ya kupikia kijiko 1, kishs weka cumin seeds zikisha pata moto zikapasuka weka kitunguu maji, tangawizi, kitunguu swaumu na pili pili mbuzi vyote viwe umekata chop chop na uendelee kukaanga.




Kisha ongeza carrots koroga na kisha weka chumvi.




Kisha weka tomato paste, nyanya ya kuiva uliyokata vipande vidogo pamoja na curry powder. Pika mapka uhakikishe nyanya imeiva. Kisha weka wali. Kaanga wali wako kwa dakika 3 hakikisha moto ni wa wastani.




Ksha ongeza maji 480 gram,  onja chumvi kama haitoshi ongeza tena kidogo,Kisha funika kikaango chako au sufuria na pika mpaka maji yakauke kabisa



Kisha weka maharage mabichi na njegere na uyoga hakikisha ulisha zichemsha kabla kama ni mbichi basi unatakiwa uzipike wakati unaweka mchele mwanzo kabisa ili nazo ziweze kuiva.






Hakikisha unakoroga vizuri kabisa mpaka inachanganyika saafi, kisha ongeza unga wa kungu manga pika kwa dakika 5 ili ladha ichanganyike safi kabisa kati ya wali wako na mboga majani.

 


Mwisho kabisa weka majai ya korienda ili kuongeza ladha na harufu nzuri hakikisha una mpatia mlaji chakua hiki kikiwa cha moto.

Pia badala ya uyoga unaweza tumia nyama ya ngombe au nyama ya kuku na pia hata prawns lakini inabidi uzikaange nyama hizi wakati unaweka mchele ili ziive pamoja na unatakiw aukate vipande vidogo vidogo sana iwe rahisi kuiva.

FURAHIA NA FAMILIA YAKO




Thursday, September 23, 2010

KITAFUNWA SAFI KABISA KWA MUDA WOTE

HIKI NI KIAZI CHA KUKAANGA KWA MTINDO WA AINA YAKE RECIPE SAFI KABISA FURAHIA NA FAMILIA YAKO.


MAHITAJI
  250 gram za kiazi mbatata au kiazi ulaya
1 Kitunguu maji chop chop
60 gram njegere za kuchemshwa
1 au 2  pili pili mbuzi (sio lazima)
1/2 kijiko kidogo cha chai mustard seeds (sio lazima)
5 gram unga wa binzali  
1 fungu la majani ya corriender
5 gram chumvi 


MAHITAJI YA MCHANGANYIKO KWAJILI YA KUCHOMEA KIAZI CHAKO

2 kijiko kikubwa cha chakula unga wa dengu  
1/2 kijiko kidogo cha chai ginger powder  (unga wa tangawizi)
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa cayene ( sio lazima)


JINSI YA KUANDAA FATA MAELEKEZO CHINI KATIKA PICHA

 
 

 
Osha vizuri viazi vyako na kisha kata kata kama picha inavyoelekeza kisha weka katika sufuria na vichemshe mpaka viive viwe laini visipondeke.


 

Kisha viponde ponde mpaka vilainike kabisa unaweza kutoa ngozi ya juu ya kiazi au ukaiacha bado kiazi chako kitakua na ladha nzuri ya maganda.




Katika kikaango weka kijiko kimoja kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia, kisha weka mustard seeds kama umeamua kuzitumia ila sio lazima. Zikishaanza kupasuka, Kisha ongezea kitunguu maji, unga wa binzali, pili pili mbuzi na chumvi kisha endelea kukoroga. 





Baada ya hapo weka viazi ulivyokua umeshaviponda pamoja na majani ya korienda na njegere zilizokwisha chemshwa.




Kaanga kwa dakika 1 au 2 mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.





Kisha chukua mchanganyiko wako wa viazi na anza kutengeneza miduara midogo midogo kama picha inavyoelekeza. kwa kipimo hichi utapata miduara 11 hadi 12.




Sasa tunaanda ulemchanganyiko kwajili ya kuchomea viazi vyetu, chukua vyote na weka katika bakuli moja.



Kisha weka maji kiasi katika mchangayiko huo wa unga. Hakikisha sio nzito sana wala sio nyepesi sana. Inatakiwa iwe nzito uwezo wa kushika kwenye mduara wa kiazi chako.




Kisha chukua miduara ya viazi vyako na weka katika mchanganyiko wa unga mzito zungusha ikamate kiazi chote vizuri kabisa.




Unaweza tumia kikaango cha vitumbua au pan cake puffs. Weka kijiko kiomja cha mafuta katika kila shimo katika kikaango mafuta yakishapata moto tumbukiza miduara yako ili ikaangike. kama huna aina hii ya kikaango basi tumia sufuri au kikaango kikubwa na wewka mafuta yakutosha ili viazi viweze kuelea katika mafuta.




Kaanga kwa dakika 2  hadi 3 katika moto wa wastani kisha geuza upande wa pili ili kiazi chote kiive .






Kisha toa na weka kwenye sahani kama una tawel safi weka juu yake ili inyonye mafuta yanayodondoka toka katika kiazi kwa dakia 1 tu. Kawaida unaweza kula na mayonaisi au piko yeyote ile ya pili pili au ya maembe na inapendeza kula ikiwa ya moto.




Ukipasua kwa ndani muonekano ndio huu ladha yake ni safi sana sana.

KWA WALE WASIOPENDA MAFUTA KABISA AU KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA HAWARUHUSIWI KUTUMIA MAFUTA.

UKISHAMALIZA KUCHOVYA MCHANGANYIKO MIDUARA YOTE YA VIAZI, WASHA OVEN IPATE MOTO KISHA WEKA VIAZI HVYO KATIKA TREI NA UIPAKE MAFUTA KIASI ISAIDIE VIAZI VISISHIKE CHINI KISHA CHOMA MPAKA IBADILIKE RANGI NA ITAKUA YA KAHAWIA.

LADHA HAITABADILIKA TOFAUTI NI KUA HAVITAKUA NA MAFUTA KAMA VILE VYA KUKAANGA.

ENJOY YOUR LOVELY WEEKEND!!!



Tuesday, September 21, 2010

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA NJUGU NA NJEGERE

WALI  HUU NI MAARUFU SANA KWA WATOTO HUWA WANAUITA WALI MATUNDA HAHAHAHAAAAAAA!!!

MAHITAJI

240 gram mchele wa basmati rice (au mchele wowote mrefu – pia unaweza tumia wali uliobaki)
360 gram njugu mawe zilizochemshwa
1 kijiko kidogo cha chakula mbegu za binzali nyembamba
1 bay leaf
2 au 3 hiriki nzima za kukauka
2 au 3 mbegu ya karafuu 
1/4 kijiko kidogo cha chai unga wa binzali
1 kitunguu maji chop chop
1 carrot kata kat vipande vidogo vidogo
60 gram mahindi ya njano ya kopo
60 gram njegere za kuchemshwa au za kopo
Chumvi weka kulingana na ladha 
1 fungu la giligilani (fresh coriender) kwajili ya kupambia na kuweka harufu nzuri.






Nakusahuri loweka mchele wako kwenye maji kwa dakika 20. Hii itakusaidia unapopika wali wako usishikane na uive haraka kutoka na na aina ya mapishi haya. Ila tumia njia hii ukiwa na muda tu kama huna muda wakusubiri piaka kawaida. Washa jiko kisha weka kikaango au sufuri ili lipate moto kisha weka kijiko kimoja kikubwa cha mafuta. Ongezea mbegu za binzali nyembamba. Kisha weka vitunguu chop chop kaanga kwa dakika 1 kisha weka, karafuu, mbegu za hiriki, bay leaf , binzali ya unga na chumvi endelea kukoroga ili viive viungo vyote.



KIsha ongeza carrots na kaanga kwa 40 sekunde. Kisha weka mchele (Kama uliloweka kwenye maji hakiisha unauchuja vizuri uwe mkavu).endelea kukaanga na hakikisha mchele wote unakua mkavu na kuelekea kuiva.




Kihs weka maji 480gram  (kama wali wako utakua haujaiva unaweza kuongeza maji 240 gram inategemea na ubora wa mchele wako). Funga mfuniko na pika kwa dakika 8-10 mpka wali uive na uone maji yamekauka kabisa. Kisha weka njugu mawe na njegere endelea kukoroga uchanganyike safi kabisa.

 

KIsha mwagia majani ya giligilani (corriender) kwa ldha safi na harufu nzuri. Kama unatumia wali ulio bakia, kumbuka karoti kuziweka pamoja na njugu na njegere wakati wa kupika. 

Kupika wali uliobakia kwanza vile viungo vyote vya mwanzo pamoja na kitunguu weka kama kawaida kaanga kisha unaweka karoti, njegere na njugu mawe kaanga mapaka zilainike kisha unaeka wali na kuendelea kukoroga. pika kwa dakika 3-5 au mapak wali wako ukiwa unamoto wa kutosha na umechanganyika vizuri na mboga zote.



KIsha kata vipande vya mkate na uvikaushe kwenye oven au kwenye mafuta na pamnba juu ya wali wako. Sasa itakau tayari kwa kula nakuachi kazi ya kuandaa mboga ya kulia iwe nyama au samaki au hata ukitaka kula hivyo hivyo inafaa sana tu  ;)




 
Huu ni muonekano wa wali uliokwisha iva unapendeza katika sahani

 




CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA KWA FAMILIA YAKO!! ONEKANA BORA KWA KUA MBUNIFU WA MAPISHI MBALI MABALI KATIKA FAMILIA YAKO.



TENGENEZA ICE CREAM YA MAEMBE NA LADHA YA NAZI BILA YA KUTUMIA MASHINE


  RECIPE SAFI KABISA NI RAHISI SANA NA UNATENGENEZA KIASI CHA KUTOSHA KISHA UNAHIFADHI KWA MATUMIZI YA MUDA MREFU KWA FAMILIA.

MAHITAJI

2 maembe makubwa yaliyoiva wastani
2 kijiko cha chai juice ya limao
240 gram tui la nazi iwe ya unga au fresh 
240 gram maziwa ya maji 
3 kijiko kikubwa cha chakula maizena (cornstach)
120 sukari
1/4 chumvi kijiko cha chai  
2 kijiko kikubwa cha chakula machicha ya nazi
2 ute wa yai mweupe
120 fresh heavy cream

JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO KATIKA PICHA HAPO CHINI






Menya maembe yako vizuri na kisha katakata vipande vidogo vidogo na weka katika mashine ya kusagia yasage mpaka upate uji mzito kabisa wa maembe.


 



Chukua tui la nazi na nusu ya maziwa kisha weka katika kikaango au sufuri ana yapashe moto.





maziwa yaliyobakia weka katika bakuli nyingine na changanya cornstar chsukari pamoja na chumvi.





Kisha chukua mchanganyiko wa maziwa na sukari weka kwenye mchanganyiko wa maziwa na nazi na endelea kupasha katika moto mdogo sana iwe vugu vugu tu isichemke.





koroga moja kwa moja bila kuacha mpaka mchanganyiko wako uwe mzito kabisa.






 
Kisha ongezea yale machicha ya nazni na weka pembeni ipoe.




Kisha chukua uji mzito wa maembe na changanya katika ule mchanganyiko wako wa maziwa na nazi




Koroga uchanganyike vizuri mchanganyiko wote kama inavyoonekana katika picha




Kisha mimina katika bakuli la kioo na iweke kwenye freezer igande



 
Tumia mashine ay mchapo chapa ute wa mweupe wa mayai




 
Hakikisha ute unakua laini mpaka unakau kama mapovu




Kisha piga cream kwa kutumia mchapo au mashine

Kisha chukua ule ute wa mayai changanya na cream uliyopiga tayari pole pole mpaka ichanganyike vizuri.




Kisha chukua ule mchanganyiko wa maembe utakua umesha ganda nusu hamishia katika bakuli safi




 
Kisha chukua ule mchanganyiko wa cream mwagia katika mchanganyiko wa maembe na changanya pole pole.



Hakikisha unachanganya pole pole usitumie nguvu utaharibu ni pole pole.





Mchanganyiko wako sasa upo safi kabisa kama unavyoonekana katika picha





Kisha chukua mchanganyiko wako na hamishia kwenye lile bakuli ulilotumia mwanzo kugandishia weka kwenye freezer na igandishe kwa masaa 3. Kisha itoe na ikoroge mpaka iwe laini kabisa kisha irudishie tena mpaka igande kabisa.






Kabla ya kuchota hakikisha kijiko cha chakula au kijiko maalumu cha kuchotea unakiweka kwenye maji moto ili ikurahisicshie kutoshika na kutoa umbo zuri.








Unaweza weka kwenye bakuli na ukala ukafurahia au unaweza weka kwenye biscuit

 



Pia unaweza weka kipande cha embe kwa juu kama urembo na ikapendeza kabisa



 


HUU NDIO MUONEKANO WA ICE CREAM YETU UNAWEZA WEKA LADHA YEYOTE ILE IWE VANILLA AU CHOCOLATE AU KARANGA NI WEWE BINAFSI UPENDAVYO SIO LAZIMA IWE YA NZAI NA BADO ITAPENDEZA SNA HATA UNAWEZA WEKA LADHA YA MACHUNGWA AU PAPAI AU NANASI FURAHIA HII NA FAMILIA YAKO



 

Wednesday, September 15, 2010

JINFUNZE KUTENGENEZA KEKI YA MAEMBE BILA KUTUMIA MAYAI

KWA WALE WOTE WENYE MATATIZO WASIO TUMIA MAYAI HUU NI WAKATI WAO NAO PIA KUJIDAI KWA KUJIFUNZA KUANDAA KEKI HII YA LADHA YA TUNDA EMBE LA KUIVA BILA YA KUTUMIA MAYAI


MAHITAJI

600gr unga wa ngano

2 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
1/2 kijiko kikubwa cha chakula chumvi 
1 kijiko kikubwa cha chakula unga wa hiriki
360gr Nyama ya maembe yaliyoiva
60gr siagi
120gr sukari 
1 kijiko kikubwa cha chakula vanilla ya maji


SUKARI TUMEWEKA KIASI TU KUMBUKA MAEMBE TAYARI YANASUKARI




Weka vipande vya embe ulivyomenya uka kata kata kwenye mashine ya kusagia kisha saga






Baada ya kusaga utapata muonekano huu safi kabisa wa rojo zito la maembe





Kisha chuja unga safi kabisa kwa kutumia chujio




Baada ya kuchuja unga wako safi kabisa weka unga wa hiriki ndani ya unga wako pamoja na baking powder.



Kisha kwenye bakuli nyingine weka ile rojo zito za maembe na changanya na sukari pamoja na siagi iliyoyeyushwa na ukoroge kwa kutumia mchapo





Baada ya hapo anza kuweka unga kwenye mchanganyiko wako wenye maembe na sukari pole pole mimina unga ndani ya mchanganyiko wa maembe


Changanya pole pole  mpaka maembe na unga vichanganyike kwa kutumia mwiko kama inavyoonekana hapo katika picha.




Kisha chukua chombo chako cha kuokea keki kipake siagi kwa pembeni na chini ili isaidie keki yako isiungue na kushika. Choma keki yako katika oven iliyokwisha pashwa moto 320F mpaka 350 F kwa dakika 30 - 40.





Baada ya dakika hizo kuisha weka kijiti cha mbao kama inavyoonekana katika picha kikitoka kikavu basi keki yako imeshaiva kikitika na maji maji basi bado haijaiva punguza moto na irudishe tena kwa dakika 5 angalau na upime tena kwa kijiti kama imeiva.



Sasa huu ni muonekano keki yetu imeshaiva iache ipoe na itajimega yenyewe na kuachia chombo ulichotumia kuokea kisha utaimimina pole pole kwenye sahani na kuanza kuipamba wewe upendavyo





Unaweza ukamwagia sukari ya unga kwa juu kisha uka kata kata maembe na ukamalizia na jani la mint itakua na muonekano kama hapo katika picha na inavutia kwa mlaji.





Pia unaweza ukaitaka katika umbo akama hilo hapo juu na kwa mduara mdogo kiasi cha kuweza kula mtu mmoja na mlaji akafurahia.

KWA UTANASHATI ZAIDI UNAWEA UKATUMIA ZILE TRAY ZA KUOKEA MUFFIN NA UKATENGENZA KEKI NDOGO NDOGO KWA MAUMBO TOFAUTI ILI MRADI MLAJI AVUTIWE NA MUONEKANO.

ENJOY WITH YOUR FAMILY!!