CULINARY CHAMBER

LIBENEKE LA CHAKULA BORA WATU LAZIMA WALE MSOSI MTAMU NA SALAMA KUJIFUNZA NI BURE

Tuesday, December 30, 2014

CHEF ISSA AFANYA MAAJABU KWENYE KOMBE LA DUNIA LA MAPISHI 2014 NCHINI LUXEMBORG

K
 Executive Chef Issa Kipande  tunayemfahamu kama Chef Issa (aliyeshika kombe) wiki hii amefanya makubwa kwa kuwa mmoja wa ma-Chef  wa timu ya Stockholm, Sweden, kushiriki na hatimaye kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha timu za kanda kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Mapishi  2014 yajulikanayo kama  Villeroy & Boch Culinary World Cup 2014  yaliyofanyika nchini Luxemborg. Mshindi wa jumla alikuwa Singapore.

Kushinda kombe la dunia si mchezo katika tasnia yoyote ile nasi hatuna budi kumpongeza Chef Issa kwa kuwakilisha vyema Watanzania na Waafrika kwa jumla.
 Mtanzania huyu anayefanya kazi huko Sweden na Mtwara kuliko na hoteli yake aliyoifungua hivi karibuni, ameshiriki katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika kila baada ya miaka minne na yaliyoshirikisha ma-Chef zaidi ya 3000 kutoka nchi 56 za mabara yote matano ya dunia.

Mpaka sasa Chef Issa Kapande mbali ya kushinda tuzo nyingi tofauti katika fani yake ya upishi pia anashikilia rekodi ya kuwa Chef Mtanzania Msomi na mdogo kuliko wote aliyewahi kufungua na kuongoza hotel ya nyota tano  akiwa Internationally  Certified Executive Chef  akiwa na umri wa miaka 25 tu. Hili ni jambo la kujivunia sana.
Chef Issa anasema kuwa Mola ajaliapo anatamani sana mwaka 2018 aipeleke Timu ya Taifa ya Tanzania mashindano haya. "Na nina imani tutafanya vizuri tu kwani kuna wapishi wazuri sana nyumbani Tanzania ingawa wamekosa nafasi au muongozo wa kuweza kuonyesha uwezo wao. Mungu ibariki Tanzania", anasema.
 Executive Chef Issa Kipande  tunayemfahamu kama Chef Issa (aliyeshika kombe) akiwa na  timu yake ya  Stockholm, Sweden,
Switzerland 
 Executive Chef Issa Kipande alipoitwa mbele kwenda kupokea tuzo akiwa mtu  mweusi peke yake
 Executive Chef Issa alipata heshima kubwa sana ya kuhudhuria executive lunch kwa watu maalumu tu iliofanyika  wakati wa kutoa kombe la dunia kushoto ni Raisi wa mashindano hayo na kulia ni mtoto wa mfalme wa nchi ya Luxembourg Crown Prince Guillaum
Executive Chef Issa akiwa na Raisi wa chama cha ma-chef dunia nzima 
Bw. Gissur Gudmundsson.