Monday, January 25, 2010

NAMNA YA KUTENGENEZA CHAPATI



Unga kilo moja weka sukari kijiko kimoja cha chai pamoja na chumvi kijiko kimoja cha chai




weka mafuta ya kupikia yamoto kikombe kimoja cha chai kidogo kisha changanya




Kisha weka maji ya uvugu vugu kikombe kimoja cha chai kidogo na endelea kuchanganya















Kanda mpaka upate mchanganyiko mzuri laini na mkavu



Kata saizi ya unga ambao ukisukuma itatosha kwenye kikaango chako



huu ni muonekano wa chapati ndogo itakayoweza kuenea katika kikaango kidogo hata kwa matumizi ya nyumbani iweke kwenye kikaango cha moto  bila mafuta pika pande zote mbili



kisha weka mafuta naigeuze geuze





hii ni chapati yako imekamilika na ni laini na ina lea kama daftari na ni tamu kupita maelezo


11 comments:

  1. Kaka nakufagilia sana,
    unaweza kunitembela hapa kwa kupeana ushari wa hapa na pale
    www.kaluse.blogspot.com

    ReplyDelete
  2. habari za kazi chief,
    ninafurahishwa na kupendezwa na kazi zako za kuakikisha kila mtu anaanda/kupika chakula kinavyotakiwa na kupata ladha nzuri.

    Ila mi kwenye hii topic ya maandalizi ya CHAPATI, umenichanganya kwenye hicho kipimo cha Kikombe kidogo cha chai, mi nimeshindwa kuelewa kikombe kidogo cha chai ni kipi, maana siku hizi kuna kila aina ya vikombe.

    Ningeomba uwe unaweka vipimo kwenye UNITS, pamoja na hivyo vya kukadiria kama kikombe cha chai n.k, maana si wote tunauwezo wa kuwa na hivyo vipimo vya Units.

    Nakutakia kazi njema Chief Issa

    ReplyDelete
  3. Mimi kukanda chapati wakati mwingine huwa natumia maji ya baridi ambayo nimeyatoa kwenye friji, yaani yabaridi sana tuseme ninayaweka kwenye friza kabla hayajaganda ndio nakandia chapati. Kisha unga ukishakandika, nakata ukunja vidonge navisukuma kisha napaka samli kidogo au ghee au mafuta yoyote kidogo sana kisha naukunja tena kuwa vidonge vidogo vidogo. Nikishamaliza kukunja wote, ndio naanza sasa kusukuma chapati zangu na kuzichoma. Kwa kuwa tayari unga una mafuta natumia mafuta kidogo sana kuchomea.

    Hizo cgapati zinaweza kukaa hata siku 2 au 3 bado laini zinalika bila wasi2

    NB: Wakati mwingine naweka viazi au vitunguu kwenye huo unga kuongeza ladha.

    Mswahili

    ReplyDelete
  4. Kaka Issa nashukuru sana kwa haya mapishi ya chapati na maandazi,upishi wangu sio mzuri chapati zangu huwa ngumu kama ubao hata kuzikunja wakati wa kula haziwezekani, nilikuwa nimepanga kukuuliza kama utatuwekea hii topic. Nimefurahishwa sana na wepesi wa mapishi yako ni lazima niyafanyie kazi siku za hivi karibuni. Je waweza kutuandikia na mapishi ya sambusa? -MDAU, USA

    ReplyDelete
  5. mimi nimekula chapati lakini chapati zetu za atl za dada Linda ni tamu jamani chapati kama croissant! embu aulizwe zinapikwaje jamani mh yule dada mashalau anapika chapati hata wa Iran hawaingii sijui wahindi waharabu ziro! tena mimi uwa nazila na chai sitaki mchuzi wala maharagwe mana ntaharibu radha,chapati za Linda express mwishoooo!

    ReplyDelete
  6. hi

    yaan bro huwa tunabishana sana kwenye kupika chapati kila mtu anaweka kipimo chake thank GOD unaweka na kiasi cha kipimo jaman..

    very hapi maana moja ya hobbies zangu ni kupika...

    ReplyDelete
  7. thanx a lot.
    mie nakaa mbali na nyumbani and have been dying to know how make chapatis....

    ReplyDelete
  8. Mimi naona chef Issa yupo sahihi.Unajua asilimia kubwa ya sis tuliokulia huku kwetu tz anatusaidia sana.

    Maana ukiniambia unit sijui mililita kwa kweli utatupoteza wengi na wachache ndio watao mpata.Hususani tukiwa tunatengeneza maakuli ya nyumbani.


    ILA kama ndio kutengeneza misosi ya magharibu au asia ya mbali sio mbaya akiweka hivyo vipimo vyenu vya unit au moto sio 200-250 dakika 10-15

    ila kwa issue ya chapati,makande wali biriani nafikiri bado anaweza kutumia vipimo asilia ..

    kila la kheri chef

    ReplyDelete
  9. WEWE NI COMMANDO WA MAPISHI, YAANI MUME WANGU ATANIKOMA

    ReplyDelete
  10. Thanx Issa, nimeifahamu hii blog karibuni ila nimeipenda na naitembelea kila siku

    ReplyDelete
  11. 5 Years later bado this is the best recipe everrrr

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako