Friday, April 9, 2010

BISKUTI BISKUTI


BISKUTI ZA LADHA YA COCOAMACHUNGWA, TANGAWIZI NA VANILLA


Picha hii inaonyesha mahitaji kwajili ya biskuti

3 Mayai
250 gram sukari ya unga / Icing sugar 
750 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai baking powder
250 gram siagi /  margarine
70 gram cocoa powder
1 Chungwa au limao
1 kijiko kidogo cha chai Tangawizi 




Changanya unga wa ngano, baking powder, sukari ya unga pamoja na siagi



Kisha iponde ponde ichanganyike vizuri kabisa




Baada ya hapo tengeneza shimo katikati kisha vynjia mayani na endlea kuchanganya mpaka upate mchanganyiko safi kabisa



Huu ni muonekano safi wa mchanganyiko safi wa unga wa biskuti ukielekea kukamilika




Kwaruza chungwa mpaka upate vichenga chenga vya ganda la chungwa au unaweza tumia limao



Gawanyisha unga wako uliokwisha kandwa katika pande mbili sawa weka cocoa powder kwenye moja ya unga uliotenga




Kisha uchanganye vizuri kabisa ili ili kokoa yote iingie safi kabisa kwenye mchanganyiko huo wa unga wa biskuit



Huu ni uonekano wa mchangayiko wa unga wa biskuti kila moja lina ladha na muonekano tofauti kwasasa



Anza kusukuma kwanza ulemchanganyiko mweupe kwa upana wa wastaniisiye nyembamba sana biskuti zako zitakakamaa sana 




kisha sukuma ule mchanganyiko wa pili uliobaki wa cocoa uwe na upana sawa na ule mchanganyko mweupe


Kisha zungushia kwenye mpini wa kusukumila ule mchanganyiko wa cocoa ili iwe rahisi kubeba kisha beba weka juu wa mchanganyiko mweupe na kisha zungusha mpini pole pole ili mchanganyiko wako uachie pole pole mpaka mwisho



Kisha sukuma kwa juu ya mchanganyiko mweupe upate usawa mzuri na michanganyiko hiyo miwili ishikane safi kabisa




ukimaliza anzia mwanzo kuja kiasi kisha endelea kuzungusha mpaka umalize mduara wote




Baada ya hapo chukua aluminium foilzungushia kwa juu ifunike safi kabisa kisha weka kwenye freezer kwa masaa 2 itakua imepoa vizuri na imeshikana safi kabisa tayari kwa kukatwa na kuchomwa kwenye oven



Toa mduara wako wa biskuti katika freezer kisha anza kukata upana wowote unaopenda wewe kisha weka kwenye tray na choma kwa dakika 15 - 20 kikubwa angalia biskuti zimekua ngumu na rangi nzuri ya kahawia angalia zisiungue.



HUU NI MUONEKANO SAFI NA THABITI WA BISKUTI YAKO YENYE LADHA ASFI SANA UNAWEZA KUTUMIA KWA CHAI YA JIONI SAA 10 AU SAA 4 ASUBUHI IWE OFISINI NYUMBANI AU HOTELINI.



12 comments:

  1. Mmmhh! Ahsante kwa biskuti zinaonekana tamu kweli. Je zinatengenezwaje?

    ReplyDelete
  2. uuuuh tupe habari, haya ndiyo mambo yenyewe majumbani.

    ReplyDelete
  3. hizi ni habari njema kwa sisi wenye familia.

    ReplyDelete
  4. no comment this is what i've been wating

    ReplyDelete
  5. Asante sana kaka, biscut za s.market bye bye

    ReplyDelete
  6. Hi Chef Issa, zile chengachenga za machungwa unaziweka wakati gani?

    ReplyDelete
  7. Asante kwa darasa, chengachenga za ganda la chunguwa/limau zinatumika wakati gani?

    ReplyDelete
  8. Kaka Issa, chenga za ganda la chungwa/limau na tangawizi vinawekwa wakati wa hatua ipi?

    ReplyDelete
  9. Naona unaelekea kunifanya kuwa mke na Mama bora, asante sana

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako