Wednesday, April 14, 2010

CHICKEN STIR FRIED RICE

WALI HUU NI MTAMU SANA TENGENEZA FAMILIA YAKO IFURAHI WEEKEND HII

MAHITAJI

1 kilo wali uliopikwa
150 gram kitunguu
150 gram karoti
250 gram kabechi
150 gram pili pili hoho
5 mayai mabichi
150 gram soya sauce
1 kuku mzima au kifua chakuku 500 gram
160 gram mafuta ua kupikia

Pika kwanza wali wako na usiweke chumvi maana wakati unaukaanga utaweka soya sauce na inachumvi kweli.


Kata mchanganyiko wa mboga kama inavyoonekana katika picha



Kisha chukua kuku mzima mtoe nyama yote na mifupa weka pembeni



Huu ni muonekano wa kuku baada ya kutenganishwa na mifupa kisha ikate nyama hii katika vipande vidogo vidogo kwa urefu



Huu ni muonekano wa nyama ya kuku ikiwa katika mkato wa urefu tayari kwa kupikwa




Weka mafuta kaika kikaango yakishapata moto weka mboga zote kwa wakati momoja na uendelee kuzikaanga


Hii ni chupa ya light soya sauce ni nzuri na mtu yeyote yule anaweza kula na akafurahia chakula kilichochawnganywa pia inapatikana maduka ya chakula yote nyumbani tanznaia na bei yake ni sh 800 tu.



Kumbuka mboga zisiive kabisa ziive nusu tu bado ziwe ngumu kisha kuku kaanga mpaka aive haichukui muda kwakua tayari umekata mikato midogo ikishaiva kuku weka mayai kaanga nayo yasiive kabisa ila yawe magumu kiasi yasikauke kisha weka wali uliokwaisha iva kaanga kisha weka soya sauce changanya mpaka wali wote uwe na rangi ya soya sauce.




Huu ndio muonekano wa wali wako ukiwa na rangi safi kabisa chukua nyanya zilizokatwa kwa urefu pamboa chakua chako kitamu kabisa




Mwisho kabisa juu unaweza pamba na majani yeyote yale ya kijani mi nimetumia maganda ya tango unamenya kisha unakata katika umbo hilo dogo chakula hiki nirahisi sana kuandaa pia ni nafuu na unaweza lisha familia ya watu 10 na wakashiba.

WALI HUU HAULINI NA MCHUZI UNAJITOSHELEZA KABISA NI LAINI WEEKEND NJEMA

12 comments:

  1. Sawa kaka. Naomba basi uipost kabla ya week end ili niandae maakuli ya mwisho wa wiki. Ahsante sana...

    ReplyDelete
  2. je chef wali huu ni lazima upike na kuku tu, je unaweza changanya na pronsi???

    ReplyDelete
  3. kaka nashukuru sana kwa kutuwezesha kupika mapishi mbalimbali MUNGU akubariki sana.

    ReplyDelete
  4. kaka nashukuru sana kwa kutuwezesha kupika mapishi mbalimbali MUNGU akubariki sana.

    ReplyDelete
  5. weka majina na majina ya kiswahili ya hivyo vyakula, maana wengine kingereza KWISHNE, hatuelewi kabisa, tunaona kuku tu! hatujui mlichokifanya

    ReplyDelete
  6. Naomba nione chupa ya soya sauce unayotumia na utuambie kazi zake plzzz.....(matumizi yake)

    ReplyDelete
  7. thanks kaka kwa kazi nzuri
    vipi huu wali unaliwa bila mboga i mean mchuzi rost au thupu

    ReplyDelete
  8. Thanks chef....kumbe hii soya inaasili ya kichina eee? thanks...halafu napitaga kwenye migahawa ya kichina saana ....kwenye mapishi yao huwa supu yao ni hii soya sauce...upatapo nafasi utupe na recipe za kichina na utuelezee hii soya sauce....naipenda ina test mnooo

    ReplyDelete
  9. Hi Issa, yani leo nimepata muda wakutembelea tovuti yako, nimependa sana ratiba ya chakula cha mtoto, yani so many interesting receip. nitaanza kupika kimojakimoja then i will let you know.
    Asante sana, nakutakia kazi njema.

    Vanessa

    ReplyDelete
  10. bei ya soya soauce tu hahahaaa
    kaka ubarikiwe nadhani unajua jinsi wateja wako uku tunavofaidi,mie naprint hivi vituz na kuweka km kijarida ivi ili nisisahau

    imenisaidia sana

    ReplyDelete
  11. Hivi unaweza kutumia nyama nyingine kutengeza huu msosi, kama ng'ombe, kitimoto, mbuzi?

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako