Chukua Amira ya chenga gram 11
Chumvi nusu kijiko kidogo cha chai
Sukari gram 250
Unga wa ngano kilo moja
Maji ya uvugu vugu nusu lita
Mafuta ya kupikia lita 2 na nusu
Weka pakiti ndogo ya amira yenye ujazo wa gramu 11 yoote kwenye unga wako wa kilo moja
Kisha weka chumvi nusu kijiko kidogo cha chai chumvi hii husaidia kupunguza mafuta ndai yaa andazi baada ya kuiva andazi lako litakua halina mafuta safi na salama kwa mlaji
Weka sukari gram 250 katika unga wako
Baada ya hapo weka mafuta ya moto ujazo wa kikombe kidogo cha chai au gr 250
changanya vizuri mafuta bado yakiwa yamoto
Kisha weka maji ya uvuguvugu ili kuuwa ngano nakufanya amira kuweza kumuka haraka
Kanda mchanganyiko wako safi kwa kutumia nguvu na umakini mpaka mchanganyiko wako uwe laini
Mchangyanyiko wako kama uko bado ni teketeke na ulizidisha maji kidogo weka unga kiasi kisha endelea kukanda mpakja uwe mkavu na laini
Hapa safi sasa
Shepu vizuri tayari kwa maandalizi ya kusukuma na kukata
Sukuma unga wako mpaka saizi ya unmene halisi wa andazi lako utakavyopenda liwe
Kisha tumia kitu chechote kile kukatia kwa umbo lolote lile utakalo lipenda
Yaache kwa muda wa dakika 10 baada ya kuyakata yaumuke kisha itakua tayari kwa kuyachoma
Baada ya kukata maumbo mazuri ya duara unga unaobakia unaweza viringisha maumbo tofauti kama uonavyo katika picha pia unaweza tengeneza hata herufi
Pasaha mafuta yako katika moto wa wastani yasiwe na moto mkali utapelekea maandazi yako kuungua kisha yaweke katika moto na geuza kila mara ili yasivimbe upande mmoja na ikawa vigumu kuyageuza
Hili ni anfazi lako safi limeshaiva na halina mafuta ndani na safi kabisa
Du yamy yamyiii, am going to do it for Kids over this weekend, Mungu akubariki kwa kushare nasi kipaji chako kaka. tupe ushauri juu ya watoto wasiopenda kula
ReplyDeleteMdau
Lim2217
Mbona maandazi hayana iliki? Sie watu wa pwani maandazi yanatiwa iliki, yaani zile mbegu zake unatoa unazisaga kidogo unachanganya kwenye unga kabla hujaweka maji. Mimi maandazi kwa ajili ya watoto huweka mayai na maziwa au tui la nazi badala ya maji ili kuongeza virutubisho.
ReplyDeleteMswahili
mswahilki sie hatutaki mapishi ya kiswahili,kaka hapa ye anatufundisha ya kwake hivyo hajakosea.we na iliki kivyako vyako.Wapishi wengii...........???
ReplyDeletechef hongera kwa kazi nzuri,endelea kutuelimisha na kutunufaisha kwa kipaji ulichopewa na Mola.
ReplyDeletekila la kheri Chef
mama Roxxie.
asante kaka sana kwa recipe yako nzuri sana ya maandazi, hata mie sipendi vikorombenzo naipenda style yako hiyo, ukiweka iliki sipendi kabisa hiyo arufu yake kwenye maandazi asante naenda kupika saa hii ,
ReplyDeletenakukubali sana kaka angu...mara nyingi nikitaka kupika hua nachungulia humu ndani nipate maujanja mara moja namsuprise husband
ReplyDeletekila nikikaanga maandazi au kalimati yanakuwa na done ndani yani halichambuki kama sponji, nakosea nini??
ReplyDeleteAsante kwa maelekezo. Nataka kupika maandazi lakini natumia dough mixer kukandia je nafuata utaratibu huo
ReplyDeleteChef katika siku zote nilizowahi kupika maandazi haya kiboko! Malaini na mazuri mno na ndani hayana mafuta. Ubarikiwe sana. Asante!
ReplyDeleteChief nimeyapenda sana haya maandazi, maana hayana viungo ving me hua sipend maandazi yenye ilik na viungo viingii.
ReplyDeleteChief hakika nakupongeza sana kwa elimu ya ujasiliamali uliyoitoa bure tena kwa kueleweka. Tushindwe wenyewe maana maandishi pamoja na picha vinajieleza wazi kabisa
ReplyDelete