CHAKULA HIKI NI SAFI NA SALAMA KWA WATU WASIOPENDA MAFUTA KABISA NA WASIOPENDA VITAMBI NA WANOTAKA KUDUMISHA UZITO WALIONAO USIENDELEE LADHA NA MUONEKANO NI SAFI SANA!
MAHITAJI
1 kilo Samaki fillet aina yeyote
400 gram karoti
400 gram spinach
200 gram kitunguu
Kata kata mboga zote hizi kisha zichemshe katika maji yaliyochemka kwa dakika 5 kisha toa weka mafuta ya kupikia kidogo na chumvi ili kuweka ladha katika mboga na kufanya mboga yako ing'ae.
Kisha chukua chombeo cha duara kiwe cha chuma au plastiki yote sawa ili uweze kuishape mboga katika sahani.
Kisha pakua wali ulio katika umbo la duara tumia kikombe weka wali wako uliokwisha iva na kikombe kisiwe kikubwa sana kiwe na umbo la duara uswa na mduara wa mboga tayari uliokwisha tengeneza.
Baada ya kuweka wali mwisho unaweka samaki wako aliyechemshwa jinsi kuchemsha samaki.
chukua fillet ya samaki kisha ikate upana wa kidole gumba kwa urefu kisha izungushe iwe na umbo la duara na ichome na toothpick ili isfunguke kisha itumbukize kwenye maji yaliyochemka na kuchanganywa na mboga mboga kama kariti na kitungu na pili pili hoho pamoja na maji ya limao ili kuongeza ladha kwa samaki huyu chemsha kwa dakika 10 hadi 15 atakua ameiva.
Mtoe samaki na weka juu ya wali kama picha inavyoonyesha.
MAHITAJI YA KUTENGENEZA WHITE SAUCE
150 gram Unga wa ngano
200gram Blue band au butter
1/2 kijiko cha chai unga wa binzali au safron
1 lita maziwa
1 maji ya limao
1/4 kijiko cha chai kungu manga
2 mbegu za karafuu kavu
1 kikubwa kitunguu chop chop
JINSI YA KUTENGENEZA
weka blue band au butter katika kikaango au sufuria acha iyeyuke kiasi kisha weka kitunguu chop chop kaanga kilainike.
Huyu ndie samaki alie kamilka sauce yake inawekwa mwisho kabisa baa ya samaki kupangwa unaweka katika umbo la duara kuzunguka chakua hicho mwisho kabisa juu unaweka kipande cha limao.
Furahia siku na familai yako.
Kisha weka unga wa ngano koroga uchanganyike vizuri na mafuta kisha chukua mchapo wa chuma (Whisker) ili utumie kukorogea wakati unaweka maziwa.
Anza kumimina pole pole mziwa huku ukikoroga na mchapo mapaka upate rojo zito kabisa endelea kumimina maziwa mapaka upate rojo laini kabisa kama maziwa yamekuishia basi ongezea hata maji kiasi. kisha weka kungu manga, unga wa binzali kwa rangi nzuri au safron ya njao au ya orange na karafuu kuongeza ladha safi kabisa.
Huyu ndie samaki alie kamilka sauce yake inawekwa mwisho kabisa baa ya samaki kupangwa unaweka katika umbo la duara kuzunguka chakua hicho mwisho kabisa juu unaweka kipande cha limao.
Furahia siku na familai yako.
Kaka habari miminimeipenda sana blog yako sana sana kwa sisi watz ambao tunaishi nje hatuna choice ya chakula kama unapokuwa home tz ,ila nilikuwa naomba unapoweka majina ya viungo utuandikie majina yote 2 la kiingereza na la kiswahili ,si unajua tena huku nchi za watu unaweza ukawa unataka tangawizi lkn sbb hujui km inaitwa ginger ukahangaika kutafuta ukakata tamaa ukasema hamna kumbe tatzo ni jina kuwa katikalugha tofauti,asante mungu akubarikikwa kuanzisha hii blog ya mapishi iliyokatika lugha ya nyumbani,asante
ReplyDeleteIssah I am your fan! Naishi nje ya nchi and always wanted to share Swahili food with friends but had no idea how to make it look pretty! I am a very hard to please person but I take my hat off man! Ya it's best you share the ingredients names both in English and Swahili. I like this porched fish, it's healthy, taste and also a feast for the eyes too. Keep it up!
ReplyDelete