Tuesday, April 20, 2010

FAMILIA YAKO WANAPENDA KEBAB? WATENGEZEE HII WATAFURAHIA SANA

CHAKULA HIKI NI KIZURI SANA NA ANAWEZA KULA MTOTO KUANZIA MWAKA MMOJA MPAKA MTU MZIMA NI LAINI, SLAMA NA TAMU SANA.

MAHITAJI

1 kilo ya nyama ya kusaga
100 grama kitunguu chop chop
100 grama pili pili hoho chop chop
50 grama tomato pest
15 gram chumvi
10 gram pili pili manga
2 yai
100 gram unga mkavu wa mikate (bread crumbs)
50 gram soya sauce
15 gram tabasco sauce
2 majani ya korienda au parsley
50 gram kitunguu swaumu na tangawizi iliyosagwa


JINSI YA KUANDAA

Chukua nyama ya kusaga changanya na vitu vyote hivyo kwa mara moja



Kisha tengeneza miviringo ya nyama kama inavyoonekana katika picha kisha chukua miti ya mbao ya mishikaki iwe mirefu



Chukua mviringo mmoja wa nyama kisha uzungushie kwenye kijiti cha mshikaki kandamiza vizuri na tengeneza umbo refu zuri


kandamiza pole pole ili nyama ishike katika mti wa mshikaki



Kisha zungushia mti huo wa mshikaki aluminium foil ili isungue kwenye oven kisha paka mafuta kidogo kebab zako na weka katika oven choma kwa dakika 15 hadi 20 itakua imeiva.

Chakula hiki ni safi na salama hakina mafita mengi na unaweza kula na viazi aina tofauti nitakuletea recipe soon na au uanweza kula na ugali na wali pia.

KAMA HAUNA OVEN BASI FATA MFULULIZO HUO JISNI YA KUTENGENEZA KISHA TENGENEZA UMBO LOLOTE ZURI UNALOPENDA USITUMIE TENA MTI WA MSHIKAKI PIAGA MAYAI PEMBENI CHOVYA HIYO NYAMA KWENYE MAYAI KISHA KAANGA KWENYE MAFUTA YALIOCHEMKA VIZURI SIO SAANA MAANA ITABABUKA NA HAITAIVA NDANI YAWE NA MOTO WA WASTANI ILI IIVE POLE POLE KAMA UNAKAANGA MAANDAZI UTAPATA KABAB SAFI KABISA.

6 comments:

  1. Chef nisaidie unaweza ki=upika kababu kwa kufry kwenye mafuta km unavyopika maandazi nataka kupika ila oven sina nijbu kabla cjanunua mahitaji

    ReplyDelete
  2. mdau hapo juu nadhani unaweza kuchoma kama mshikaki sema moto huwe mdogo hili usiunguze.


    chef issa mimi nilikua naulizia badala grams unaweza kuniambia kiwango kwa kijiko manake sina vipimo kwa grams hapa asante sana.

    ReplyDelete
  3. heee kumbe mbao unaviringisha na foil??hahahahaa asante maana nilikua naunguza sana izo mbao katika oven

    elimu murua kabisa leo nimepata

    ReplyDelete
  4. na kweli izo grams wengi hatuna

    sie waswahili bwana,wee tupe kipimo cha kijiko gani

    ReplyDelete
  5. Habari kaka. tunashukuru sana kwa kutufumbua macho sie vipofu panapo mapishi. tatizo langu ni vipimo unavyotumia, sina kitchen scale sasa unaweza weka vipimo kwa vikombe

    ReplyDelete
  6. Habari kaka. Navyojua mimi foil paper hutakiwi kuweka kwenye microwave sasa inakuaje unaweza weka kwenye oven ya kawaida? what is the difference?

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako