Tuesday, April 27, 2010

JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA MTOTO KUTOKA KATIKA RATIBA

JINSI YA KUANDAA CHAKULA CHA JUMATANO

KIFUNGUA KINYWA ( BREAKFAST)
Yai la kuvuruga na mkate wa ufuta
1 yai
20 gram maziwa ya maji

hilo ndo yai la kuvuruga kisha unaweka juu ya kipande cha mkate

Piga yai pamoja na maziwa kisha kaanga kwenye kikaango vuruga vuruga kumbuka lisiive sana likakauka liive kawaida tu kisha muwekee mtoto juu ya mkate wa ufuta kama hauna basi weka katika kipande cha makte wowote ule uwe mweupe au wa kahawia nitaweka recipe ya kutengeneza mkate hivi karibuni.

Uji wa soya

100 gram maziwa ya maji
300 gram maji
250 gram unga wa soya
50 gram mtindi usio na ladha ya matunda

Changanya unga wa soya na maziwa katika bakuli kisha chukua sufuria weka maji hiyo gram 300 chemsha yakisha chemka weka mchanganyiko wa maziwa na unga wa ulezi koroga mpaka uchemke na kuchanganyika safi kabisa ili uji wako usishike chini na kuungua. Acha uchemke vizuri kisha onja ukipata ladha ya kuiva kwa nafaka utakua tayari.

Toa jikoni weka kaitka bakuli atakalo tumia mtoto kisha changaya mtindi usio na ladha yamatunda pamoja na sukati tayari kwa mtoto kunywa.
CHAKULA CHA MCHANA

SALAD YA KUKU WA KUKAANGA MCHANGANYIKO WA MBOGA NA JUISI YA PASSION

Mahitaji

100 gram nyama yakuku
50 gram caroti
50 gram brocoli au zuchini
50 gram nyanya mbivu
50 gram pili pili hoho

Kata kata nyama ya kuku katika umbo dogo upana wa kidole isiwe na mifupa kisha weka mafuta kiasi katika kikaango weka kitunguu swaumu kidogo na tangawizi kaanga nyama kwa dakika 7 - 10 itakua imeiva kabisa.

Kisha chukua mchanganyiko wa mboga hizo osha vizuri kisha kata katika umbo dogo pia iwe rahisi kwa mtoto kula kisha weka katika kikaango pia zipate moto tu kwa dakika 5 toa changanya na ile nyama ya kuku kisha weka juisi ya limao kiasi na chumvi mpatie mtoto ale. kama mtoto ni mdogo kutafuna shida chukua mchanganyiko wote huo saga katika mashine ya kusagia nyama kisha mpate mtoto.

Juisi ya passion

Tengeneza kama kawaida tu kamua tunda lako safi kisha toa mbegu na uchangaye na maji kiasi kutoa chachu kisha ifadhi katika friji sukari weka wakati mtoto anataka kunywa ili juisi yako isiharibike.
CHAKULA CHA JIONI

MTINDI USIO NA LADHA YAMATUNDA NA MCHANGANYIKO WA MATUNDA

Mahitaji

100 gram mtindi halisi usio na ladha ya matunda
50 gram embe bivu
50 gram papai bivu
50 gram ndizi mbivu
50 gram apple rangi yeyote ile
30 gram karanga au korosho


Katakata matunda katika maumbo madogo kabisa ili mtoto aweze kula kiurahisi kisha changanya matunda pamoja na mtindi juu yake rushia karanga au korosho mpatie mtoto ale.
CHAKULA CHA USIKU
VIPANDE VYA NYAMA YA NG'OMBE NA TAMBI

Mahitaji
150 gram Nyama ya ng'ombe
150 gram tambi
50 gram kitunguu
50 gram karoti
50 gram maharage mabichi
15 gram soya sauce

Kata kata nyama ya ng'ombe vipande vidogo kisha weka mafuta kiasi kwenye kikaango kisha anza kukaanga nyama ya ngombe weka na chumvi kiasi kaanga mpaka ikauke kabisa itakau imeisha iva. Kisha weka mchanganyiko wa mboga majani hizo nazo unakua umekata mikato midogo midogo ili mtoto isimsumbue kula.
Chukua tambi ulizokwisha chemsha changanya katika mchanganyiko huo wenye nyama na mboga mboga kisha pika kwa dakika 3 tu ili vichanganyike vizuri weka na soya sauce kish mpatie mtoto ale kikiwa cha moto.



Tambi na vipande vya nyama muonekano na harufu yake safi itamvutia sana mtoto na atafurahia chakula

ORODHA YA MANUNUZI

Yai, mkate wa ufuta au wowote ule, unga wa soya, maziwa , sukari, mtindi uio na ladha ya matunda, nyama ya kuku, karoti, pilipili hoho, maharage mabichi, tambi, nyama ya ng'ombe, soya sauce, kitunguu maji, embe, papai, ndizi mbivu, apple, karanga na zucchini.





1 comment:

  1. hi. naipenda sana hii blog. naomba kuuliza hapa hizi ni tambi au pasta? au pasta kwa kiswahili zinaitwa tambi? mi ninavyojua tambi ni za kupika kwa sukari

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako