JUISI HII YA PARACHICHI INA VIRUTUBISHO VINGI SANA KATIKA MWILI NI TIBA KWA AFYA YA MLAJI TENGENA KWAJILI YA FYA YA FAMILIA YAKO
Kata parachichi nusu kama inavyoonekana katika picha
Kisha toambegu ya kati kati chukua kijiko toa nyama ya ndani weka katika blenda kwajili ya kusaga pamoja na matunda mengine
Mahitaji
1 parachichi lililoiva
2 ndimu safi zenye maji ya kutosha
50 gram maji safi ya baridi
2 vipande viwili vya papai la kuiva
3 sukari kijiko kikubwa cha chakula
2 asali kijiko kikubwa ca chakula
5 gram chumvi
Kwa ladhazaidi unaweza ngezea jani la fresh mint sio lazima
Jinsi ya kuandaa:
WEka katika blenda parachichi, vipande vya papai, jani la mint kisha anza kusaga wakati unasaga unaongezea maji kiasi ili mchanganyiko usiwe mzito sana ukashindwa kuchanganyika . Mwisho kabisa ongezea asali, chumvi, limao na sukari kisha blend vizuri upate mchanganikio safi na wenye ladha safi.
Kisha weka katika friji ipoe nakushauri juisi hii kunywa muda wa mchana wakati huu mwili unakua umejiandaa kupekea virutubisho vilivyopotea. Safi sana kwa mtu mzima na mtoto pia ni nzuri sana kwa wale wanaozingatia mlo safi ili wasiongezeke uzito.
MPATIE MWANAO AU MUMEO GLASI MOJA ANGALAU KILA BAADA YA SIKU 2 JUISI HII INA LADHAYA KIPEKEE
Asante chef. kwema lakini? maana ulikuwa kimya kidogo.
ReplyDeletemmmh! itakuwa tamu sana let me go & try
ReplyDeletehellen
Nisipoweka sukari si takuwa poa tu
ReplyDeletekaka upo?
ReplyDeleteasante sana kwa juice nzuri kama hizi. nyumba zetu zina furaha kubwa sana kwa matunda ya mafunzo yako. Mungu akuzidishie.
Hi Chef,nilikua na swali nje ya topic hii. Nauliza juice ya passion inatengenezwaje? Ukizingatia tunda lenyewe lina mbegu nyingi unazichambua kwanza ama unablend na mbegu zake tu na hazina tatizo? Naomba jibu tafadhali.
ReplyDeleteasante kaka kwa huduma yako
ReplyDelete