Wednesday, June 23, 2010

JINSI YAKUTENGENEZA SPINACH AND RICOTTA CANNELLONI

CHAKUL AHIKI KINASAIDIA SANA KUONGEZA MADINI JOTO MWILINI

Mahitaji kwajili ya watu 4


600 gram ricotta cheese
250 gram spinach iliyochemshwa kidogo na kukatwa katwa
20 gram parmesan pamesan cheese
5 gram kila moja chumvi na pili pili manga

6 fresh lasagne sheets 
240 gram mozzarella cheese
25 gram parmesan cheese
1 fungu jani ya basil


 


Huu ni muonekano wa majani ya spinach

huu ni muonekano wa pasta aina ya lasagne zinauzwa katika maduka ya chakula ni rahisi kuzipata na sio ghalia kabisa uliza tu lasagne ( matamshi sema lazania) zipo katika muonekano kama karatasi


Huu ni muonekano wa cheese inaitwa ricotta ikiwa imekwaruzwa vizuri


Katakata na chemsha kiasi spinach katika vipande vidogo kisha changanya ricotta cheese, spinach, mozarella cheese, majani ya basil, parmesan, chumvi na pili pilimanga kisha weka katika mashine ya kusagia nyama saga usitu,ie blenda itakua maji na inatakiwa iwe nzito kabisa kama inavyoonekana kwenye picha.

Kisha chukua lasagne ziweke kwenye maji kwa muda wa saa nzima zilowane zikishalowana zinakua laini toa weka juu ya meza panga kama inavyoonekan katika picha chota mchanganyiko wako wa spinach weka juu na kisha zungurusha na tengeneza mduara.

 
hapa ni baada ya kuzungurusha na muonekano unakua kama huu tayari kwa kuwekwa kwenye oven ili kuokwa tayari kwa matumizi ya chakula



Washa oven kwa nyuzi joto 190°C kumbuka kuweka mafuta kiasi katika tray yako ya kuokea  ili zisishike chini wakati zikiwa kwenye oven. choma katika oven kwa dakika 15 mpaka 20 kisha mwagia juu mchuzi mzito wa nyanya na cheese tena kiasi acha mpaka cheese iyeyuke na kuwa na rangi safi ya kahawia toa na mpatie mlaji ikiwa ya moto.

CHAKULA HIKI NI SAFI SANA KWA KUONGEZA MADINI JOTO KWAKUA KINAMCHANGANYIKO WA AINA TATU ZA CHEESE NA HASA WANAUME UKILA CHAKULA HIKI UNARUDISHA NGUVU SAFI KWA MUDA MFUPI TU HII ITAKUJENGA KUA JASIRI WAKATI WOTE KAM UMEPOTEZA NGUVU KWANI CHAKULA HIKI KINAVIRUTUBISHO SANA NA MAJIBU UTAYAONA BAADA YA MASAA MAWILI TU BAADA YA KULA.


2 comments:

  1. Habari kaka,
    Pole na kazi ya kutuelimisha kuhusu mapishi,
    Naomba unisaidie mapishi ya mboga inaitwa "Brokoli"
    Nimeambiwa inatibu na kukinga magonjwa mengi hasa baridi yabisi, mimi pia huwa nasumbuliwa na hiyo,
    Sijawahi kuipika mboga hii, Naomba unisaidie namna ya kuipika, nipo Tz.
    Thanks
    Mungu akubariki.
    Joy

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha Chef, asante sana kwa hii recipe!
    Inabidi nimtayarishie mzee!!

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako