Sunday, July 25, 2010

JE UNAPENDA KULA BURGER YA SAMAKI

KAA TAYARI KWA KULA BURGER YA SAMAKI YENYE PILI PILI HOHO NA AVOCADO SAUCE

MAHITAJI

1 kijiko kidogo cha chai mayonaise
1 sauce ya Parachichi
200 gram Nyama ya samaki
1 Jalapeno au Pili pili hoho
1 Mkate wa mviringo kwajili ya burger
1 Nyanya
1 lettuce



Huu ni muonekano wa parachichi safi lililoiva

MAHITAJI KWAJILI YA SAUCE YA PARACHICHI

2 parachcichi ndogo
3 kijikocha chakula olive oil
4 kijikocha chakula juisi ya ndimu
¼ kijiko cha chai Tabasco (Silazima)
60 gram cream
60 gram mayonnaise
1 kijikocha chakula kitunguu maji chop chop
¼ kijiko cha chai chumvi
¼ kijiko cha chai pili pli manga
JINSI YA KUANDAA

1. Menya na katkata katika vipande vidogo parachichi. Weka katika chombo parachichi, olive oil and juisi ya ndimu katika blender au food processor.
2. Kisha ongezea mayonaise, fresh cream, Kitunguu maji, Tabasco, Chumvi na pili pili manga nakisha blend mpka iwe laini na imechanganyika vizuri weka katika friji ipoe vizuri.



Huu ndio muonekano wa sauce ya parachichi kwajili ya kuweka kwenye burger yako ya samaki


Huu ni muonekano safi kabisa wa vipande vya samaki vilivyokata kwa uzito wa grama 200 kwajili ya burger. ipake chumvi, juisi ya ndimu au limao na pilipi manga.

Kisha ipakae unga wa ngao kiasi tu na iweke kwenye kikaango chenye mafuta na moto wa wastani ikaange kwa muda wa dakika 15- 20 itakua imeiva safi kabisa kwajili ya kuweka kweney burger yako.

pia unaweza kuiweka kwenye oven baada ya kuipaka unga ili kuepuka kutumia mafuta kisha tumia muda huo huo kwa moto wa wastani itaiva na kua tayari kwa kuiweka katika burger

 Huu ni muonekano wa jalapeno ukikosa tumia pili pili hoho hazipishani sana ladha zinapisha maumbo tu

Samaki akishaiva chukua mkate kata kati kati kisha paka mayonaise kwa chini na kisha weka majani ya lettuce, juu yake weka samaki ikiwa bado ya moto.

Juu ya samaki weka sauce ya parachichi ya kutosha maana ndio inabeba ladha ya burger yako pia weka kipande cha nyanya na slice za jalapeno kisha funika ka kipande cha pili cha mkate

Huu ni muonekano safi kabisa wa burger yako ya samaki ni salama kwa mlaji, furahia na familia yako.




 

1 comment:

  1. Na hii ya samaki ndiyo hasaaa kipenda roho.
    Ya prowns pia tafadhali

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako