RECIPE YA SAMAKI KAMBA (PRAWNS) KWA MITINDO TOFAUTI
MAHITAJI
1 Chupa ya Mayonaise
1 chupa ya Tomato sauce
20 gram Chumvi
10 gram Pili Pili manga
1 kijiko kidogo cha chai Tabasco
100 ram Maji ya limao
1 kubwa lettuce
1 kubwa Limao
2 kubwa Nyanya fresh
1 kilo Samaki kamba
Huu ni muonekano wa samaki kamba wabichi
Huu ni muonekano wa lettuce
Huu ni muonekano wa prawns waliochemshwa baada ya kumenywa magamba na kusafishwa vizuri
Huu ni muonekano wa coctail sauce
JINSI YA KUANDAA
Chukua prawns wamenye magamba ya juu kisha wasafishe safi na maji baridi, kisha wachemshe katika maji moto kwa dakika 5 - 8 tu watakua wameishaiva watoe waweke kwenye maji baridi wapoe tayari kwa kuandaa salad yako safi kabisa.
Kisha chukua mayonaise, tomato sauce au tomato ketchup, chumvi, pili pili manga, maji ya limao pia kama una white wine unaweza kuweka kisai kisha chukua uma au mchapo tumia kuchanganyia mchanganyiko wako mpaka uchanganyike safi na kupata ladha safi kama muonekano katika picha hapo juu.
Kisha chukua prawns wako waliopoa safi changanya na hiyo coctail sauce vizuri kisha fata maelekezo katika picha hapo chini jinsi ya kupamba kwa matumizi tofauti tayari kwa kumuudumia mlaji.
Unaweza kutumia glasi nzuri kama hiyo hapo juu chini weka majani ya lettuce kisha juu yake weka mchanganyiko wa hao prawns na Pembeni pamba na kipande cha nyanya pamoja na limao. Kisha mpatie mlaji.
Huu ni muonekano wa juu ya glasi jinsi ilivyopendeza tayari kwa kumuudumia mlaji.
Huu ni mtindo wa pili jinsi ya kupamba kwenye sahani kama kawaida chini weka majani ya lettuce kisha juu weka mchanganyiko wa prawns na coctail sauce pembeni chora mduara kwa kutumia balsamic vinegar na rushia vipande vya nyanya juu kabisa weka maotea ya mbegu ( sprout) kisha muhudumie mlaji.
Hii ya mwisho ni muonekano wa kisherehe zaidi au familia kubwa unaweka kwenye sahani kubwa kisha unaweka mezani ili kilammoja ajipakulie na kuenjoy kiasi anachotaka. mfululizo ni ule ule weka chini majani ya lettuce kisha juu nakshi prawns wako safi waliochanganywa na coctail sauce.
FANYA UBUNIFU WOWOTE ULE ILIMRADI CHAKULA CHAKO KIPENDEZE NA KIVUTIE KWA WALAJI NA UJIVUNIE KIPAJI CHAKO.
hapa utakuwa umetufikisha wapenda prawns
ReplyDelete