Saturday, July 10, 2010

JINSI YA KUANDAA SALAD YA MBOGA MAJANI NA SAMAKI TUNA

SALAD YA MAYAI, MBOGA MAJANI NA SAMAKI TUNA

MAHITAJI

1/2 kilo nyama ya samaki tuna
3 nyanya zilizoiva
1 kitunguu kikubwa
1 lettyce kubwa
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
1 chupa ya mayonaise
1 tango kubwa
30 gram vinega ( siki nyeupe)
50 gram corn oil
4 mayai ya kuku


JINSI YAKUANDA FATA MAELEKEZO KWA CHINI KATIKA PICHA




Huu ni muonekano wa samaki tuna akiwa sokoni

Hii ni nyama ya tuna baada ya kuchunwa ngozi


Huu ni munekano wa yai lililochemshwa kisha tumia kifaa hicho hapo katika picha kukatia mayai yako yatakua katika umbo safi la mviringo


Huu ni muonekano wa majani aina ya chive ni jamii moja na majani ya kitunguu cho chop kwa umbo dogo kama inavyoonekana kwenye picha

Huu ni muonekano wa tangu kubwa zuri la kijani


Huu ni muonekano wa kitunguu kikubwa kata skama inavyoonekana kwenye picha maumbo ya duara

Huu ni muonekano wa nyanya nzuri ngumu iliyoiva tayari kwa salad kata umbo kama linaloonekana kwenye picha


Huu ni muonekano wa mayonaise safi ukweli american garden mayonaise ni nzuri na inapatika dunia nzima


Huu ni muonekano wa majani ya lettuce ni kubwa na inaafya safi kabisa kwa kupendezesha salad yako

JINSI YA KUANDAA

Kwanza chemsha mayai kwa dakika 7 , kisha chemsha nyama ya samaki tuna weka vinega, chumvi na pili pili manga ili kuweka ladha safi.

Kisha kata kata mboga zako zote kama inavyoonesha kwenye picha

kisha chukua nyama ya tuna iliyopoa changanya mayonaise na majani ya chives pamoja na mafuta ya mahindi ( corn oil) maana hata ukihifadhi salad yako katika friji huwa hayana tabia ya kuganda.

kisha weka jana la lettuce kwenye sahani juu yake weka nyama ya tuna, juu ya nyama weka vitunguu na pembeni weka mayai pamoja na nyanya na matango.



MPATIE MLAJI SALAD HII KABLA YA MLO KAMILI AU UNAWEZA KULA MCHANA KAMA MLO KAMILI PAMOJA NA KIPANDE CHA MKATE AU VIAZI VYA KUCHEMSHA AU VIAZI VYA KUKAANGA NA UKAFURAHIA SANA KWA KUSHIBA CHAKULA KITAMU NA CHENYE FAIDA NA MWILI WAKO.


No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako