Thursday, August 5, 2010

JINSI YA KUPIKA BEEF AU CHICKEN CURRY YENYE NAZI


MAHITAJI
3 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia
1000 gram nyama ya ngombe au ya kuku
2 vitungu kata vipande vidogo vidogo
2 kijiko kikubwa cha chakula Thai red curry paste
1 kijiko kikubwa cha chakula maji ya limao au ukwaju
850 gram tui la nazi
2 kijiko kikubwa cha chakula sukari
6 mbegu za hiriki ziponde
1 nanasi dogo menya na kata vipande vidogo


JINSI YA KUPIKA

1. Pasha moto sufuria yako tayari kwa kupika.

2. Kaanga yama safi kabisa mpaka iwe ya kahawia kisha weka pembeni

3. Kisha weka mafuta katika sufuri, kaanga kitunguu kilainike na kianze kubadili rangi kuwa kahawia
 
4. kisha ongeza curry paste pika kwa dakika 1, endelea kukoroga.

5. Kisha weka ndani yake maaji ya ukwaju, tui la nzai na sukari.

6. Acha ichemke, punguza moto na weka nyama kwenye sufuria pamoja na mbegu za hiriki.
7. Acha ichemke pole pole kwa moto mdogo sana bila ya kufunika sufuria mpaka nyama ilainike

8. Kumbuka kukoroga mara kwa mara mpaka ikikaukia kisha funika.

9. Mimina vipande vya nanai na pika kwa dakika 5 tu.

10. Curry inatakiwa iwe na mchuzi mzito, kama unapenda mchuzi mwingi basi ongezea maziwa kidogo a maji.

MPATIE MLAJI CHAKULA HIKI KIKIWA CHAMOTO, UNAWEZA KULA NA WALI, UGALI, VIAZI, MIHOGO AU CHAPATI.



Huu ni muonekano wa beef curry yenye nazi ladha safi sana


Huu ni muonekano wa chicken curry yenye nazi saafi kabisa

FURAHIA NA FAMI,LIA YAKO


No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako