KWA WALE WOTE WENYE MATATIZO WASIO TUMIA MAYAI HUU NI WAKATI WAO NAO PIA KUJIDAI KWA KUJIFUNZA KUANDAA KEKI HII YA LADHA YA TUNDA EMBE LA KUIVA BILA YA KUTUMIA MAYAI
MAHITAJI
MAHITAJI
600gr unga wa ngano
2 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
1/2 kijiko kikubwa cha chakula chumvi
1 kijiko kikubwa cha chakula unga wa hiriki
360gr Nyama ya maembe yaliyoiva
60gr siagi
120gr sukari
1 kijiko kikubwa cha chakula vanilla ya maji
SUKARI TUMEWEKA KIASI TU KUMBUKA MAEMBE TAYARI YANASUKARI
2 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
1/2 kijiko kikubwa cha chakula chumvi
1 kijiko kikubwa cha chakula unga wa hiriki
360gr Nyama ya maembe yaliyoiva
60gr siagi
120gr sukari
1 kijiko kikubwa cha chakula vanilla ya maji
SUKARI TUMEWEKA KIASI TU KUMBUKA MAEMBE TAYARI YANASUKARI
Weka vipande vya embe ulivyomenya uka kata kata kwenye mashine ya kusagia kisha saga
Baada ya kusaga utapata muonekano huu safi kabisa wa rojo zito la maembe
Kisha chuja unga safi kabisa kwa kutumia chujio
Baada ya kuchuja unga wako safi kabisa weka unga wa hiriki ndani ya unga wako pamoja na baking powder.
Kisha kwenye bakuli nyingine weka ile rojo zito za maembe na changanya na sukari pamoja na siagi iliyoyeyushwa na ukoroge kwa kutumia mchapo
Baada ya hapo anza kuweka unga kwenye mchanganyiko wako wenye maembe na sukari pole pole mimina unga ndani ya mchanganyiko wa maembe
Changanya pole pole mpaka maembe na unga vichanganyike kwa kutumia mwiko kama inavyoonekana hapo katika picha.
Kisha chukua chombo chako cha kuokea keki kipake siagi kwa pembeni na chini ili isaidie keki yako isiungue na kushika. Choma keki yako katika oven iliyokwisha pashwa moto 320F mpaka 350 F kwa dakika 30 - 40.
Baada ya dakika hizo kuisha weka kijiti cha mbao kama inavyoonekana katika picha kikitoka kikavu basi keki yako imeshaiva kikitika na maji maji basi bado haijaiva punguza moto na irudishe tena kwa dakika 5 angalau na upime tena kwa kijiti kama imeiva.
Sasa huu ni muonekano keki yetu imeshaiva iache ipoe na itajimega yenyewe na kuachia chombo ulichotumia kuokea kisha utaimimina pole pole kwenye sahani na kuanza kuipamba wewe upendavyo
Unaweza ukamwagia sukari ya unga kwa juu kisha uka kata kata maembe na ukamalizia na jani la mint itakua na muonekano kama hapo katika picha na inavutia kwa mlaji.
Pia unaweza ukaitaka katika umbo akama hilo hapo juu na kwa mduara mdogo kiasi cha kuweza kula mtu mmoja na mlaji akafurahia.
KWA UTANASHATI ZAIDI UNAWEA UKATUMIA ZILE TRAY ZA KUOKEA MUFFIN NA UKATENGENZA KEKI NDOGO NDOGO KWA MAUMBO TOFAUTI ILI MRADI MLAJI AVUTIWE NA MUONEKANO.
ENJOY WITH YOUR FAMILY!!
Sylvia vegetarian uko wapi?
ReplyDeletehaya ndiyo mambo yako dada
disminder.
Asante Chef Issa, Nina mdogo wangu hawezi kula keki sababu ya mayai. Hii recipe itamfaa sana. Asante sana kaka
ReplyDeletetupe basi vipimo chef Issa naona hii cake itakuwa na taste nzuri sana cant wait to try this recipe
ReplyDeletedu thanks chef i have to try to prepare for family hope they will love it. nasubiri huo mkate wa karanga na maembe
ReplyDeleteSijawahi kula cake ya embe. weekend hii nitajaribu nione ladha yake ikoje. ahsante chef.
ReplyDeleteasante sana wil try to bake but please twaomba measurements ziandike in cups and spoon kidogo natatizika na grs kama vile 60gr nitapima vijiko vingapi
ReplyDeleteasante sana kwa mapishi mazuri ila tu ninakuomba vipimo utuandikie ni mugs ama ni spoons grams kidogo zanitatiza kama 60gms sijui nipime vipi.
ReplyDeleteshukrani.
mhh chef hii cake hatuweki banking powder?
ReplyDelete