HIKI NI KIAZI CHA KUKAANGA KWA MTINDO WA AINA YAKE RECIPE SAFI KABISA FURAHIA NA FAMILIA YAKO.
MAHITAJI
250 gram za kiazi mbatata au kiazi ulaya
1 Kitunguu maji chop chop
60 gram njegere za kuchemshwa
1 au 2 pili pili mbuzi (sio lazima)
1/2 kijiko kidogo cha chai mustard seeds (sio lazima)
5 gram unga wa binzali
1 fungu la majani ya corriender
5 gram chumvi
MAHITAJI YA MCHANGANYIKO KWAJILI YA KUCHOMEA KIAZI CHAKO
2 kijiko kikubwa cha chakula unga wa dengu
1/2 kijiko kidogo cha chai ginger powder (unga wa tangawizi)
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa cayene ( sio lazima)
JINSI YA KUANDAA FATA MAELEKEZO CHINI KATIKA PICHA
Osha vizuri viazi vyako na kisha kata kata kama picha inavyoelekeza kisha weka katika sufuria na vichemshe mpaka viive viwe laini visipondeke.
Kisha viponde ponde mpaka vilainike kabisa unaweza kutoa ngozi ya juu ya kiazi au ukaiacha bado kiazi chako kitakua na ladha nzuri ya maganda.
Katika kikaango weka kijiko kimoja kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia, kisha weka mustard seeds kama umeamua kuzitumia ila sio lazima. Zikishaanza kupasuka, Kisha ongezea kitunguu maji, unga wa binzali, pili pili mbuzi na chumvi kisha endelea kukoroga.
Baada ya hapo weka viazi ulivyokua umeshaviponda pamoja na majani ya korienda na njegere zilizokwisha chemshwa.
Kaanga kwa dakika 1 au 2 mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.
Kisha chukua mchanganyiko wako wa viazi na anza kutengeneza miduara midogo midogo kama picha inavyoelekeza. kwa kipimo hichi utapata miduara 11 hadi 12.
Sasa tunaanda ulemchanganyiko kwajili ya kuchomea viazi vyetu, chukua vyote na weka katika bakuli moja.
Kisha weka maji kiasi katika mchangayiko huo wa unga. Hakikisha sio nzito sana wala sio nyepesi sana. Inatakiwa iwe nzito uwezo wa kushika kwenye mduara wa kiazi chako.
Kisha chukua miduara ya viazi vyako na weka katika mchanganyiko wa unga mzito zungusha ikamate kiazi chote vizuri kabisa.
Unaweza tumia kikaango cha vitumbua au pan cake puffs. Weka kijiko kiomja cha mafuta katika kila shimo katika kikaango mafuta yakishapata moto tumbukiza miduara yako ili ikaangike. kama huna aina hii ya kikaango basi tumia sufuri au kikaango kikubwa na wewka mafuta yakutosha ili viazi viweze kuelea katika mafuta.
Kaanga kwa dakika 2 hadi 3 katika moto wa wastani kisha geuza upande wa pili ili kiazi chote kiive .
Kisha toa na weka kwenye sahani kama una tawel safi weka juu yake ili inyonye mafuta yanayodondoka toka katika kiazi kwa dakia 1 tu. Kawaida unaweza kula na mayonaisi au piko yeyote ile ya pili pili au ya maembe na inapendeza kula ikiwa ya moto.
Ukipasua kwa ndani muonekano ndio huu ladha yake ni safi sana sana.
KWA WALE WASIOPENDA MAFUTA KABISA AU KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA HAWARUHUSIWI KUTUMIA MAFUTA.
UKISHAMALIZA KUCHOVYA MCHANGANYIKO MIDUARA YOTE YA VIAZI, WASHA OVEN IPATE MOTO KISHA WEKA VIAZI HVYO KATIKA TREI NA UIPAKE MAFUTA KIASI ISAIDIE VIAZI VISISHIKE CHINI KISHA CHOMA MPAKA IBADILIKE RANGI NA ITAKUA YA KAHAWIA.
LADHA HAITABADILIKA TOFAUTI NI KUA HAVITAKUA NA MAFUTA KAMA VILE VYA KUKAANGA.
ENJOY YOUR LOVELY WEEKEND!!!
No comments:
Post a Comment
Tunaheshimu sana maoni yako