KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA
1 Kitunguu maji kikubwa
6 au 7 miti ya celery, safisha na kata ndogo ndogo
3 viazi ulaya vya umbo la kati
1 lita ya maji
1 kijiko kidogo cha chai aromati
1 kijiko kikubwa cha chakula unga wa binzali (curry powder)
10 gram chumvi na pili pili manga
5 gram kitunguu swaumu kilicho sagwa
JINSI YA KUTENGENEZA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
weka katika kikaango kijiko kimoja cha siagi, kisha kaanga kitunguu maji na unga wa binzali (curry powder).
Kisha ongezea maji. halafu funika sufuria yako kwa dakika 10 mpaka 15.
Chukua mchanganyiko wako huu na weka katika blenda saga mpaka upate uji mzito kabisa
Kisha mimina tena katika sufuria, mwisho kabisa weka pili pili manga na ukoroge.
Chukua mchanganyiko wako huu na weka katika blenda saga mpaka upate uji mzito kabisa
Kisha mimina tena katika sufuria, mwisho kabisa weka pili pili manga na ukoroge.
Hakikisha unampatia mlaji ikiwa yamoto kabisa toka jikoni ili kupasha tumbo na kuamsha hamu ya kula mlo kamili kisha pamba na majani ya celery.
Asante kwa kutufundisha kupika kwa kutumia celery. Nitajaribu maana hili jani au miti nikiiona nashindwa hata kujua ni jinsi gani ya kuipika.
ReplyDeleteNitajaribu halafu nitakuambia kama nimepatia.
Salaam kwa wote
Mama Jeremiah
kaka hiyo celery kwa kiswahili inaitwaje
ReplyDelete