RECIPE SAFI KABISA YA WALI HUU MAARUFU MIJI YA PWANI YA BAHARI YA HINDI
MAHITAJI
480 gram nazi iliyokunwa
240 grama za mchele ( Basmati), loweka katika maji kwa dakika 20. Au wali uliokwisha pikwa ukaiva ila uwe umechambuka pia nao unafaa.
2 kijiko kikubwa cha chakula dengu au choroko loweka katika maji kwa dakika 10
1 au 2 pili pili mbuzi kuongeza ladha lakini sio lazima
1 kijiko cha chakula ( mbegu za mastad) mustard seeds
5 majani fresh ya binzali (curry leaves)
100 gram za korosho au karanga ziwe zimekaangwa
5 grama chumvi
2 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAELEZO NA PICHA HAPO CHINI
Kabla hatujaanza kupika tunatakiwa kukuna nazi, unatakiwa kuvunja nazi zako ziwe katika vipande viwili kama inavyoonekana katika picha.
Hii ndio mashine ya kukunia nazi ukienda katika duka la kuuzia vyombo utapata tu kwa be nafuu inatumia umeme na inarahisisha kazi.
Unatakiwa uwashe kwanza mashine kisha ndio uchukue kipande kimoja cha nazi na uweke kwenye mashine ili ianze kukwaruza na kupata machicha na muonekano katika picha ndio njia sahihi ya kukuna nazi kwa mashine.
Unaona jinsi kikwaruzo cha nazi kinavyozunguka kwa kasi katika picha jitaidi usiongee na simu au kupiga stori ukajisahau mashine hii ni kali sana itakutoboa vidole jitaidi kuna nazi yako haraka kisha endelea na mambo yako.
hapa umeshamaliza kukuna nazi yako saafi kabisa na umepata machicha ya kutosha kwajili ya wali wako. Machicha haya ni matamu sana sana ukila mabichi.
Weka vijiko 2 vya mafuta kula katika sufuria, weka mbegu za mastard zikianza tu kupasuka, ongeza dengu, pili pili mbuzi, korosho , majani ya binzali (curry leaves) . Kisha endelea kukaanga kwa dakika 2.
Baada ya dengu kua za kahawia na korosho kukaangika, Kisha ongeza machicha ya nazi na kaanga kwa dakika 5 hadi 10 au mapka machicha ya nazi yaange kugeuka rangi na kua kama kahawia.
Sasa weka wali wako uliokua umelowekwa kwa dakika 20.
Hakikisha unakoroga vizuri mpaka wote uchanganyike vizuri kwa dakika 10 tayari utakua umeiva hakikisha unakoroga tu ili wali wako usiungue na kushika chini. Wali huu haupikwi na maji maana uliloweka mchele kwa dakika 20 kwahiyo unakua umemeza maji pia kumbuka unaweza tumia wali uliokwisha iva.
Muonekano wa wali wako ukiwa tayari umeisha iva tayari kwa mlaji kufaidi!
Inapendeza sana kua mbunifu kifuu kile kile cha nzai ulicho kuna unaweza kukitumia kama bakuli ya kupakulaia wali wako na ikapendeza sana.
(Samahani wapenzi wa blog sikuahinisha Mchele uliotumika hapa ni aina ya basmati, kawaida mchele huu ukilowekwa katika maji kwa dakika 20 na ukaukaanga kwa dakika 10 unakua umeiva kabisa tayari kwa chakula jumla ya muda wako wa maandalizi inakua dakika 30 na zinatosha bakisa kuivisha wali wako. Endapo utatumia aina nyinge ya mchele bora tumia ulioisha iva ili usikosee recipe ukala wali mbichi)
MUONEKANO WA KUMUHUDIMIA MLAJI NDANI YA KIFUU CHA NAZI NI KIVUTIO CHA KIPEKEE SANA. WALI HUU UNAPIKWA KWA MUDA MFUPI SANA HAUPOTEZI MUDA WAKO NA LADHA YAKE NI OOHHHH YAMY YAMY!!!!
habari asante kwa kutuonyeshahyo mashine ya nazi samahani naomba ututajie inaitwaje kwa kiingereza ili tuitafute maana huku overseas ktu ambacho nakichukia ni nazi ya kopo haina hata test na mimi ni mtoto wa Dar es salaam nmezoea wali nazi
ReplyDeleteasante na kaz njema
Hakikisha unakoroga vizuri mpaka wote uchanganyike vizuri kwa dakika 10 tayari utakua umeiva hakikisha unakoroga tu ili wali wako usiungue na kushika chini. Wali huu haupikwi na maji maana uliloweka mchele kwa dakika 20 kwahiyo unakua umemeza maji pia kumbuka unaweza tumia wali uliokwisha iva.
ReplyDeletemi hapa haa sijaelewa hivi jamani kweli mchele ulio lowekwa kwa dk ishiri utaunkaanga kwa dk kumi na utakuwa wali? mhhh hiii hapana chef
bora tu ongesema kama ulivyosema unaweza kutumia mchele ulio chemshwa sawa lakini sio mchele mbichi uloweke na ukaange bila hta ya maji hauiviiii
na kama nimekosea kukosoa basi nawe nikosoe