Wednesday, January 26, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA KITAFUNWA HIKI KWAKUTUMIA UNGA WA MCHELE


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA NA JINSI YA KUANDAA KITAFUNWA HIKI


MAHITAJI

240 gram Unga wa mchele

240 gram maji baridi
 2 kijiko kikubwa cha chakula dengu za njano
1 kijiko kidogo cha chai mbegu za Cumin
1 kijiko kidogo cha chai mbegu za ufuta
1 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya samli
5 gram chumvi
1.5 au 2 lita ya mafuta kwajili ya kukaanga


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



Loweka dengu katika maji kwa saa 1



Kisha chukua dengu pamoja na maji uliolowekea weka katika moto ichemke changanya chumvi na samli ichemke pamoja kwa dakika 30 tu.


Baada ya hapo changanya na unga wa mchele ndani ya dengu zinazochemka. Hakikisha unatumia mwiko kuchanganya ili dengu zipondeke na zichanganyike vizuri kati ya maji na unga wa mchele kama unavyopika ugali. Unga ukichanganyika vizuri zima jiko haraka. Funika na kifuniko cha sufuria yako kisha weka pembeni kwa dakika 10 hadi 15.




Mchanganyiko wako ukishapoa changanya unga wa pili pili, mbegu za ufuta, mbegu za cumin kisha endelea kukanda tena kwa dakika 1 tu ili ichanganyike vizuri na kua laini pia unaweza ongezea chumvi kidogo kulingana na ladha upendayo.



Chukua kikaango kisha weka mafuta na weka katika jiko la moto, Hakikisha mafuta yanapata moto ila yasitoe moshi maana hayataivisha yatababua chakula chako. Kata kiasi kidogo cha unga kisha zungurusha kama unafinyanga kwa kutumia mikono miwili upate umbo la duara kama muonekano katika picha.



Kisha zungusha na ikutane ifunge kabisa na upate mduara safi kati kuwe na tobo hakikisha inashikana vizuri ili ukiaanga isiachane.




Huu ni muonekano wa umbo zuri la kitafunwa chetu


Endelea kwa mtindo huu mpaka mchanganyiko wote wa unga uishe. Unaweza tumia kitambaa au mfuniko kufunika ili unga wako usikauke na kuharibika. Weka miduara ya kitafunwa hiki kwakua mafuta yamechemka vizuri vitazama chini kisha vitajitokeza juu baada ya kuiva,



Punguza moto uwe wa stani ili usiunguze vitafunwa vyako


Hakikisha unakaanga mpaka upate rangi ya kahawia safi kabisa


 
Angalia picha ya chini kitafunwa kinapendeza zaidi kuliko kitafunwa katika picha ya hapo juu

Baada ya kitafunwa kuwa cha kahawia toa kwa kutumia mwiko wenye matundu ili kuchuja mafuta na weka katika taulo maalumu kwa jikoni ili ziendelee kujichuja mafuta.


Kisha weka katika bakuli baada ya kupoa kwa matumizi ya muda mrefu!



Kumbuka kua hutakiwi kukaanga kwa moto mdogo kwani kitafunwa kitanyonya mafuta na kua teketeke.



NAIMANI FAMILIA YAKO WATAPENDA SANA KITAFUNWA HIKI



4 comments:

  1. Asante kaka!!! Nasubiria kwa hamu!
    usiwe unatusahau hivi!

    ReplyDelete
  2. JAMANI HII INATENGENEZWAJE JAMANI?

    ReplyDelete
  3. Asante chef kwa kutuwekea mahitaji. Ila hapo kwenye picha, kidogo umeniacha. Je hizo dengu nachemsha au naloweka? Halafu unapozichanganya na unga wa mchele, unafanyaje fanyaje hapo? naomba maelezo kaka yangu, ili familia ifurahi

    ReplyDelete
  4. Asante sana kaka.
    Mungu azidi kukubariki.

    Ninashukuru sana

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako