Thursday, March 24, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA KUKAANGA WA KITUNGUU SWAUMU


KAA TAYARI KWA MAPISHI YA WALI HUU SAFI WENYE LADHA YA KITUNGUU SWAUMU NI MAARUFU SANA KWA WENZETU WAPHILIPINO.

MAHITAJI

500 gram za wali ulio iva au wali uliopikwa ukalala ( Huwa natumia mchele wa Basmati)

2 kijikjo kikubwa cha chakula kitunguu swaumu kilichosagwa
4 mbegu nzima za kitunguu swaumu kilichomenywa (sio lazima)
4 miti ya majini ya kitunguu maji chop chop
5 gram chumvi
 1 kijiko kikubwa cha chakula siagi ( butter)
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI



Katika kikaango weka siagi kisha iyeyuke kisha tupia mbegu za kitunguu swaumu ziendelee kuiva.




Kaanga mpaka iwe ya kahawia hakikisha haiunguwi. Hii hatua sio lazima ila mimi nimeongezea tu kwakua huwa napenda sana ladha ya kitunguu swaumu (garlic lovers) kisha toa hizo mbegu na weka pembeni.


Katika kikaango hicho hicho, weka kitunguu swaumu cha kusangwa na majini ya kitunguu maji mabichi yalio katwa katwa



Mchanganyiko wako ukishalainika na kutoa arufu nzuri, kisha chukua wali wako na weka katika kikaango.




Hakikisha una changanya haraka haraka ili iweze changanyika vizuri.


Kisha rushia zile mbegu za kitunguu swaumu ulizokaanga mwanzo na uendelee kuchanganya.





Hakikisha unampatia mlaji haraka chakula kikiwa cha moto chakula hiki unaweza kula na mchuzi au mboga ya aina yeyote.





AINA HII YA MAPISHI INATUFUNDISHA KUA TUNAWEZA AMSHA LADHA ILIYOPOTEA KATIKA WALI ULIOPIKWA JANA UKALALA BADALA YA KUTUPA TUNAONGEZA LADHA NA MLAJI ANAFURAHIA KAMA UMEPIKWA LEO. NI DHAMBI KUTUPA CHAKULA CHYUKUA UTAALAMU HUU NA FAMILAI YAKO ITAFURAHI SANA.


4 comments:

  1. Habari ya kazi,mmh mbona hamna maelezo,natamani sana nijue ili niongeza ladha kwenye ubwabwa,
    all the besr

    ReplyDelete
  2. asante sana kwa utahamu huu nimzuri san be bless my bro

    ReplyDelete
  3. yaani, nimefurahi sana, so simple and looks delicious, nitajaribu week end hii, ijumaa unapika wali mwingiii halafu jumamosi unafanya mambo.
    great bro, keep it up, and God be with u

    ReplyDelete
  4. Habari yako chef, mimi nimtanzania ninaeishi US,ninapenda kupika nakujifunza mapishi mapya. Nimefurahi kuona watalaam wa mapishi kutoka Tanzania mnajitokeza na kuonyesha ujuzi, kwani mara nyingi huwa nategemea Food Network,Cooking Channel pamoja na vitabu. Unafanya kazi kwenye restaurant gani ili nikija bongo nije kula?
    Great job and keep it up!

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako