Thursday, March 17, 2011

WAPENZI WA PANCAKE JARIBU HIZI ZA UNGA WA MCHELE NA CHOROKO NA UTAFURAHIA


HABARI NJEMA KWA WALE WASIOTUMI NAFAKA AINA YA NGANO NA WALE WASIOTUMIA MAYAI NA WANGEPENDA SANA KULA CHAPATI HIZI ZA MAJI KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI SANA UFURAHIE NA FAMILIA YAKO.

MAHITAJI

180 gram za mchele uliochemshwa

180 gram za mchele uwe wenye mbegu fupi nene
120 gram za choroko zilizotolewa ngozi
1/2 kijiko cha chai Fenugreek seeds ( angalia chini hapo katika picha)
1-1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi




JINSI YA KUANDAA FATILIA MAFUNZO HAPA CHINI



Loweka choroko pamoja na  Fenugreek katika bakuli moja kisha loweka mchele katika bakuli jingine kwa masaa matatu tu.



Nahuu ni muonekano wa mbegu za  Fenugreek 


Huu ni muonekano wa choroko



Unaweza tumia blenda au ukalowanisha grinder kusaga mchanganyiko wako. Kama unavyoona katika picha hapo mimi natumia grinder ndogo naiweka juu ya meza na huw anatumia kusagia vitu vingi kwa urahisi zaidi. Kwasasa weka mchele na maji kisha washa amshine iendelee kusaga au blenda

 

Saga mapaka upate uji mzito. Hata baada ya kusaga kwa muda mrefu unaweza ona chenga chenga usikate tamaa ni kawaida na mchanganyiko wako uko safi kabisa. Mimina mchanganyiko wako katika bakuli pembeni.

 


Kisha usioshe blenda yako au mashine ya kusagia weka choroko na mbegu za fenugreek katika grinder pamoja na maji kiasi.




Saga tena upate mchanganyiko mzuri na mzito.




Kisha chukua mchanganyiko huo na changanya katika ule mchanganyiko wa mchele uliosagwa pia.




Hakikisha mikono yako ni safi na salama weka chumvi katika mchangayiko na changanya vizuri kwa kutumia mikono yako.Sio lazima kutumia mikono unaweza tumia mwiko pia, Lakini kumbuka joto la kwenye mikono yako linasaidia kufanya unga uchachuke vizuri pale unapouacha usiku mzima kabla ya kupika.




Weka mchangayiko wako katika bakuli safi kwa usiku mzima. Kama unaishi nchi au miji yenye joto unaacha tu nje itaumuka na kuchachuka safi sana ila kama unakaa nchi za baridi basi iwashe oven yako na kisha izime ipoe kiasi chukua unga wako na uweke humo ukae usiku mzima hakikisha oven imezimwa na joto ni dogo sana.
 

Siku inayofuata, changanya mchanganyiko wako safi. Kisha changanya vizuri tena mchanganyiko wako. Weka kikaango chako katika moto na kisha paka mafuta kiasi.Huwa natumia kitunguu kilichokatwa kuenezea mafuta katika kikaango hii husaidia mchangayiko wako wa unga usigandie wakati unakaanga.





Chukua upawa na chota mchanganyiko anza kumimina kati kati ya kikaango.




Baada ya kumimina kiasi hakikisha unasambaza kwanza uone kama inatosha au uongeze



Kiwango ni iwe nyembemba ili iweze kuiva kwa haraka

 

Acha iive kwa dakika 3 au mpaka uone mwisho mwa chapati kuna jikunja na kuacha kikaango na kua na rangi ya kahawia. Hapo itakua rahisi kugeuza na kuivisha upande mwingine.





Geuza na pika tena kwa dakika 2.




Huu ndio muonekano saafi wa chapati yako ya maji na mchanganyiko wa mchele na choroko.

 


Baada ya kuiva ikunje nusu na mpatie mlaji ikiwa ya moto.Inakua na ubora wake endapo utampatia mlaji mara tu baada ya kuiva. Enjoy chapati yako na Coconut Chutney, Tomato Chutney, Onion Chutney, Jam ya ladha yeyote au Asali.


4 comments:

  1. hii nimeipenda kaka.. sasa mbona hakuna maelezo jamani? plz weka hutujuze..

    ReplyDelete
  2. Mbona hivyo kwetu tunaita visra au visira au wengine wanaita anjera? Tofauti yake ni kuwa unaweka unga wa mtama na mchele na unapata hivyo hivyo vinavyoonekana!

    ReplyDelete
  3. kwanza nakupongeza sana chef Issa, mapishi yako yamekwenda shule,ningependa sana kujua kupika hizo chapati maji za unga wa mchele, nimeona picha tu za maandalizi ya kupika Ombi langu kwako Chef Issa ni maelezo kidogo ya jinsi ya kuandaa hayo mapishi ya chapati maji.Aksante.

    ReplyDelete
  4. kwanza nakupongeza sana chef Issa, mapishi yako yamekwenda shule,ningependa sana kujua kupika hizo chapati maji za unga wa mchele, nimeona picha tu za maandalizi ya kupika Ombi langu kwako Chef Issa ni maelezo kidogo ya jinsi ya kuandaa hayo mapishi ya chapati maji.Aksante.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako