Monday, April 18, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA KINYWAJI HIKI KIZITO CHA MAEMBE


UTEGENEZAJI WAKE NI RAHISI SANA NA NI NAFUU HUJULIKANA MAARUFU KAMA
MILK SHAKE YA MAEMBE NI TAMU SANA NA HUPENDWA NA WATU WA LIKA ZOTE

MAHITAJI



Kinywaji hiki kinatosha watu wawili kwa kutumia vipimo hivi
3  maembe makubwa
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa hiriki cardamom powder (weka kidogo kidogo kulingana na ladha)
2 kijiko kikubwa cha chakula sukari (Weka kidogo kidogo kulingana na utamu wa embe)
240 gram ya maziwa ya maji
5 vipande vya barafu (Ice cubes)
1 kijoko kikubwa vanilla ice cream


Unaweza tumia maembe yaliyogandishwa katika friji au maembe ya kwenye kopo.



Menya maembe kisha weka katika bakuli la kusagia



Weka maziwa ya maji na cardamom powder. Washa blenda yako kwa kasi ndogo ili kusaidia isage pole pole ukipata mapovu toa kwa kijiko.






KIsha weka barafu na endelea kusaga ipondeke kabisa na barafu.Kisha ongeza sukari na jitaidi kulamba uweze pata ladha unayotaka.



Kisha mimina katika kikombe juu yake unaweza weka ice cream







Huu ni muonekano safi kabisa wa kinywaji hiki kinakua cha bariidi na ni tayari kunywa watengenezee familia wafurahie na pasaka hii.


 

3 comments:

  1. yummy-yummy-my tummy. Chef tuandikie maelekezo ya kutengeneza.

    ReplyDelete
  2. kaka weka maelezo nikatengeze leo.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako