Thursday, June 16, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA MAHARAGE YA LADHA YA KUOKA


WATU WENGI WAMEKUA WAKINUNUA KATIKA MADUKA AU KULA KATIKA MAHOTEL MAHARAGE HAYA YA LADHA YA KUOKA AU BAKED BEANS SASA NI WAKATI MUAFAKA WA KUJUA JINSI YA KUYATENGENEZA NYUMBANI

MAHITAJI

480gram maharage mekundu, Loweka usiku kucha (Unaweza tumia maharage aina ya pinto)

1 Kitunguu kikubwa
1 fungu celery chop chop miti na majani yake
1 carrot kubwa kata mara 4
5 gram kitunguu swaumu kusagwa
5 gram tangawizi ya kusagwa
1 bay leaf
150 gram sukari
3 mbegu za karafuu
3 kijiko kikubwa cha chakula soy sauce
2 kijiko kikubwa cha chakula olive oil
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa : 8 masaa mpaka siku 1
Muda wa kupika: 30 dakika hadi saa 1
Idadi ya walaji: Watu 4


Chukua  pressure cooker, weka maharage, caroti, celery, kitunguu, kitunguu swaumu, karafuu, tangawizi na bay leaf. Weka maji kwenye sufuria yafunike urefu wa 1 inch.



Pika kwenye Pressure cook kwa dakika 10-15.



Baada ya hapo maji yatakua yamekauka weka chumvi, pili pili manga kisha ongezea soy sauce, sukari, olive oil na unendelee kukoroga  kwa dakika 1.



Kisha rudisha katika jiko kwa moto mdogo na usifinike sufuria yako, weka maji 400 gram chemsha kwa dakika 20 au mpaka utakapo ona yamelainika maharage. 

 


Baada ya hapo mchuzi wote utakua umekauka na utaona mchuzi mzito kabisa.


Muonekano mzuri wa maharage katika bakuli tayari kw amlaji kushambulia




Hakikisha unampatia mlaji yakiwa yamoto, maharage haya unaweza kula wakati wowote ule ingawa watu wengi hupenda kula asubuhi wakati wa chai. Pia Unaweza kula na mkate au chapati au viazi aina yeyote ile.

WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE

No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako