Wednesday, June 29, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA MCHUZI WA MBOGA MAJANI NA NAZI


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA CHAKULA HIKI YA NAZI NA MBOGA MBOGA MCHANGANYIKO

MAHITAJI

120 gram Mtindi (yogurt)

1 kilo ya Mchanganyiko wa mboga ( karot, kiazi ulaya, njegere, pilipili hoho, bilinganya, kabichi na kitunguu)
1 kijiko kikubwa cha chakula cha mafuta ya nazi (coconut oil)
1 kijiko kidogo cha chai binzali nyembamba ( cummin seeds)
1 pili pili ya kijani mbichi
120 gram tui la nazi, ( Pia nazi ya kopo au ya paketi inafaa ingawa mimi napendelea nazi fresh)
0.5 kijiko cha chai unga wa manjao (turmeric powder)
5 gram chumvi



JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa kuandaa: 30 dakika mpaka saa 1

Muda wa kupika: Chini ya dakika 15
Idadai ya walaji : Watu 2

 


Saga kwa pamoja machicha ya nazi, pilipili ya kijani na cumin seed upate tui zito.


Baada ya kupata tui zito kisha weka pembeni.


Weka mchanganyiko wa mboga zako katika sufuria yenye maji moto kisha chemsha kwa dakika 3 mpaka 3 kumbuka kuweka unga wa manjano na chumvi.


Baada ya kuchemsha kwa dakika 3 au 5 mboga zako zitakua zimeiva na maji yatakua yamepungua ongezea tui la nazi na endelea kuchemsha.



Wakati inaendelea kuchemka chukua mafuta ya nazi kisha weka katika kikaango na kaanga manjani ya giligilani au coriender leaves .Ikishatoa harufu safi tu toa katika moto



Chukua kikaango na mimina majani hayo kwenye sufuria ili ichemke.


Kisha toa sufuria katika moto. Baada ya chakula hiki kupoa kiasi kwa 37C ongeza mtindi (yogurt)


Hakikisha unachanganya vizuri.


Mchuzi mzito wa mboga mboga na nazi upo tayari! Hapa unaweza kula na wali au chapati au chochote upendacho wewe.

 


Lengo la kusubiri ipoe kiasi ni kusaidia mtindi usikatike ikiwa utachanganya wakati chakula bado ni cha moto

WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE SANA



 



5 comments:

  1. Tunashukuru sana kwa moyo uliojitolea kutuelekeza namna ya kupika vyakula mbali mbalia
    ila mimi napenda vile unavyotuandikia maelekezo kwa chini pia na aina gani ya vyakula ulivyoviandaa naona hii haujatuandikia chochote nina buni tu labda hizo ni pilipili hoho yani mengi nina kisia ila ukiweka kila moja na jina leke inakuwa rahisi hata sisi wadau kuelewa hicho hasa ndo kimenifanya nikakupigia kura wewe

    ReplyDelete
  2. kwakweli wee baba ni kiboko na hatari yani una mapishi ba'kubwa,twajifunza mengi uku adi watu wanajilamba mikono na kujing'ata.wanaume wanatulia majumbani sasa kwa misosi motomoto kwakwel....na uzuri ni kwamba binafsi napenda vyakula vya asili vyenye afya yani visivo na mafuta vikolombwezo viiingi na juisi fresh
    safi sana keep up the good job

    ReplyDelete
  3. Safi sana, kweli sasa nimesikia njaa, natamani kula,

    ReplyDelete
  4. SHUKRAN KWA HII KAKA LKN TATIZO NI KM MDAU WA KWANZA ALIVYOSEMA HAKUNA MAELEZO SO HATUJUI NI MAJANI YA AINA GANI TUTUMIE NA KIASI GANI NA TUPIKE KWA MUDA GANI.

    KWELI WENGINE KUSOMA HATUONI ILA PICHA PIA HATUJUI HIhihiiii just jokin'

    ReplyDelete
  5. Nashukuru kwa kutufungua mawazo katika nyanja ya mapishi. Ila nilikuwa na suggestion moja tu, unaweza kuweka maelezo ya ziada kuhusu portions i.e. "serving"? ili mtu kabla hajajaribu kupika anaweza jua kuwa chakula kinaweza lisha watu wangapi (just an approximation) na pia kama mtu anapika kwa idadi kubwa au ndogo na utakayo onyesha, anaweza kupuguza au kuongeza viungo kwa makadirio yaliyo sahihi zaidi ( appropriate ratios...) bila kuharibu/ kutoa ladha ya chakula iliyo tofauti... ni maoni tu...

    Akhsante kwa mchango wako

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako