Friday, June 24, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA WAFFLE YENYE LADHA YA NAZI NA UKALA PAMOJA NA MATUNDA MCHANGANYIKO


KAA TAYARI KWA KUJIFUNZA NAMNA YA KUTENGENEZA WAFFLE YENYE LADHA YA NAZI NA KISHA UKAONGEZA LADHA KWA KULA PAMOJA NA MATUNDA MCHANGANYIKO NA UIFANYE SIKU YAKO KUCHANGAMKA

MAHITAJI

KWAJILI YA MCHANGANYIKO WA MATUNDA


2 Maembe yalioiva menya na kisha kata kata vipande vidogo
450 grams ya matunda strawberries au( mchanganyiko wa apple nekundu na kijani na zabibu)
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari


KWAJILI YA WAFFLE

429gram unga wa ngano
2 kijiko kikubwa cha chakula asali
1 kijiko kikubwa cha chakula baking powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
4 kijiko kikubwa cha chakula siagi isiyo na chumvi , iyeyushe
4 kijiko kikubwa cha chakula vegetable oil
300 gram maziwa ya maji cup
4 ute mweupe wa yai, yapige wastani
120 gram tui la nazi
60 gram machicha ya nazi
Fresh mint kwajili ya kupambia 



JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI


Katika bakuli weka vipande vya maembe, strawberries na sukari



Funika matunda na karatasi ya nailoni mapak amatunda yatoe juices, kwadakika 90.Ni vizuri kama ukiandaa matunda haya usiku kucha yakakaa katika friji kisha ukayatumia asubuhi ya siku inayofuata.



Katika bakuli changanya unga, sukari, baking powder na chumvi.



Katika bakuli nyingine safi changanya siagi iliyoyeyushwa, maziwa, mayai na tui la nazi.



Chukua mchanganyiko wa unga na mimina pole pole kwenye mchanganyiko wa mayai na maziwa kisha koroga pole pole mpaka ilainike na kuchanganyika vizuri.



Mwisho weka machicha ya nazi



Hutakiwi kukoroga kwa nguvu sana itaharibu mchanganyiko wako koroga pole pole sana kiasi tu nazi hiyo ichanganyike na mchanganyiko wa unga



Washa ipate moto kwa mujibu wa maelekezo ya waffle maker's na pika mpaka iwe na rangi ya kahawia.



Muonekano huu ndio hasa inavyuotakiwa kua na ni tayari kwa mlaji kufurahia.



Mpatie mlaji ikiwa ya moto pamoja na mchanganyiko ule wa matunda yakiwa na ubaridi saafi 




MWISHO KABISA WEKA JANI LA MINT KWA KUPAMBA NA MLAJI ATAVUTIWA SANA NA MCHANGAYIKO SAFI WA RANGI NA LADHA. 


No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako