Friday, June 10, 2011

JIFUNZE KUTENGENEZA WALI WA NJEGERE

KAA TAYAI KWA RECIPE SAFI SANA YA WALI HUU WA NJEGERE

MAHITAJI
240 gram mchele wa Basmati
120 gram njegele za kumenywa (chickpeas)
3 majani ya kitunguu maji (spring onions), kata kata
1 fungu la giligilani chop chop
 1 fungu la parsley chop chop
1 kijiko kikubwa cha cakula siagi (butter) kwakuongeza ladha ya chakula
5 gram chumvi

UTAALAMU ZAIDI


Ukitaka kuongeza ubora wa muonekano na ladha unaweza weka zafarani au safron rangi yeyote ile wakati unapika wali wako. Pia unaweza kuweka aina tofauti ya viungo ipendavyo na wali ukaendelea kuvutia mlaji. 


JINSI YA KUANDAA FATILIA MAELEZO NA PICHA HAPO CHINI


Loweka mchele kwa dakika 30, sio lazima ingawa nakushauri tu kitaalamu.Binafsi huwa naloweka ili kusaidia kulowana na uive haraka pia uchambuke. Chukua kikaango weka siagi kisha ikiyeyuka weka majani kiasi ya kitunguu maji na uendelee kukaanga. Kisha chuja mchelewako wa basmati nao weka ukiwa mkavu na endelea kukaanga mpaka unukie.



 kisha weka chumvi pamoja na njegere koroga kiasi.



Kisha weka maji safi 400 gram hii inategemea na kiwango cha mchele wako,Funika mfuniko wa kikaango au sufuria yako na pika kwa dakika 10



Unaweza funua sufuria yako hata kabla ya dakika 10 hii inategemea na aina ya mchele pia kama uliloweka unaweza iva mapema zaidi. Ukiweka njegere mbichi kaaida zinaiva pamoja na wali wako na zinakua laini safi kabisa.


Kisha funua sufuria yako uangalie maendeleo.



Kisha weka chop parsley na chop giligilani kisha koroga zichanganyike na wali wako.



Baada ya hapo wali wako utakua umeiva na unaweza kula na mboga yoyote upendayo.




Chakula hiki kwa vipimo vilivyopo hapa kinatosha kuliwa na watu 3. waandalie familia yako wafurahie mapishi haya weekend hii.

No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako