Monday, November 7, 2011

JIFUNZE KUPIKA MKATE HUU WA UNGA WA ATTA NA KITUNGUU SWAUMU



KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA CHAPATI HII YA AINA YAKE

MAHITAJI

720 gram unga wa atta
3/4 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
3 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu cha kusagwa
1 kijiko kikubwa cha chakula sukari
60 gram olive Oil
120gram plain Yogurt
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya samli ( ghee)
60 gram majani ya korriender
5 gram chumvi


JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : saa 1
Muda wa mapishi : dakika 15
Idadi ya walaji : 4 watu
Idadi ya chapati : 10-12 inategemea na upana na ukubwa utakao penda



Weka unga wa atta katika beseni pamoja na baking powder, chumvi na sukari kisha changanya vizuri.



Kisha ongeza majani korienda, samli (ghee) pamoja na kitunguu swaumu na mtindi halisi usio na ladha ( Plain yorghut).



Kisha changanya vizuri.



Kisha chukua maji ya vugu vugu na weka kijiko kimoja kisha unachanganya endela na zoezi hilo mpaka upate mchanganyiko safi.



Endelea kuchanganya mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.



Kisha chukua unga wako weka katika mbao iliyomwagiwa unga na endelea kukanda kwa muda ili ulainike kabisa.



Hapa sasa mchanganyiko wako umekua laini na safi



Chukua mchanganyiko na uweke katika bakuli safi na kavu kisha funika kwasaa 1 hadi 2 na karatasi laini ya nailoni.



kisha anza kukata kiasi cha mduara ya unga ukubwa wowote unaopenda



Tumia rolling pin kisha tengeneza miduara. Usisahau kuweka unga kwenye kibao na kwenye rolling pin.



Mimina kiasi unga wa ngano kwenye kikaango.Kisha mwagia pande zote mbili za chapati yako mafuta na ukitaka ladgha safi tumia samli.



Kisha itaanza kuumuka kwa upande wa chini hiyo chapati.



Kisha geuza upande wa pili kisha chapati yako itaendelea kuumuka mara mbili ya umbo ulilosukuma mwanzo kisha malizia kupika kwa dakika 2.



Hakikisha unampatia mlaji chapati ikiwa yamoto. Mimi binafsi huwa napenda kula na yummy chicken au beef stew.



Huu ni muonekan safi wa chapati




Unaweza kula na soda, juisi, au chai pia hata kahawa na mchuzi mzito


7 comments:

  1. IDD MUBARACK KAKA UNATUSAHAU SANA KAKA.
    ASANTE KWA RECIPIE.

    ReplyDelete
  2. nimeupenda sana huu mkate kwa picha tu ila sielewi hiokitu cheupe ni hamira au ni yogat naona siku hizi unatuonesha kijuu juu huoneshi vipimo wala vitu vingine inakuw angumu kuelewa tafadhali nakuomba nioneshe vipimo na hio kitu nyeupe


    ubarikiewe

    ReplyDelete
  3. picha hazitoshi,tunaomba maelezo ya maneno,tunashindwa kutambua vitu vingine,a
    asante

    ReplyDelete
  4. unga wa ATTA unapatikana ktk maduka yetu ya bongo?pliz fafanua

    ReplyDelete
  5. Asante kwa picha nzuri, lakini tunaomba recipe kamili ili tuelewe vipimo tafadhali

    ReplyDelete
  6. inshaalah ntamikia mumewangu....lol

    ReplyDelete
  7. inshaqalah ntampikia mumewangu......lol

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako