Saturday, December 31, 2011

KHERI YA MWAKA MPYA WAPENZI WOTE WA BLOG YA CHAKULA SALAMA NA BORA



HABARI WAPENZI WA BLOG HII SAFI YA CHAKULA BORA NA SALAMA

NASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WENU NA MCHANGO WA MAWAZO YENU PAMOJA NA KUA WASOMAJI WAZURI SANA WA BLOG HII.

CHANGAMOTO ZIMEKUA NI NYINGI SANA IKIWA MOJA WAPO NI MUDA WA KUKAA CHINI KUWEKA PICHA NA MAELEZO YA MAFUNZO JINSI YAKUNDAA VYAKULA.

TUOMBE UZIMA MOLA AKIPENDA NITIMIZE NDOTO YANGU YA KUANZA KUWEKA VIDEO HII HAITAKUA NA MASWALI MENGI MAANA KILA MMOJA WENU ATAONA NA MNAKIELEWA KISWAHILI KWA UFASAHA KABISA.

PIA WALE WOTE WALIOJIANDIKISHA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WAPISHI TANZANIA KAENI TAYARI KABISA KWA MKUTANO MKUU WA CHAMA PIA TUWEZE KUCHAGUA VIONGOZI NA SHUGHULI ZA CHAMA KUANZA RASMI

KWA NIABA YA ACTIVE CHEF ASSOCIATION OF TANZANIA NA CULINARY CHAMBER BLOG NAWATAKIA MWAKA WA MAFANIKIO NA AFYA NJEMA 2012 MOLA ATULINDE SOTE NA ATUSIKILIZE DUA ZETU SOTE AMIIN

WASALAAM

CHEF ISSA


Thursday, December 29, 2011

JIFUNZE KUPIKA KITAFUNWA CHA SPINACH NA DENGU


KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABIS A YA KITAFUNWA HIKI CHA DENGU NA SPINACH

MAHITAJI

240 gram dengu (Whole Black Gram)

2 pili pili mbuzi (green chillies)
5 gram tangawizi ya kusaga
1 kitunguu maji kikubwa chop chop
240 gram spinach mbichi ikate kate (chopped Spinach)
5 gram chumvi
majani ya giligilani ya kuongeza ladha (Cilantro)
majani ya curry kwa kuongeza ladha (Curry leaves)
JINSI YA KUPIKA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPA CHINI

Muda wa kuandaa : masaa 3 hadi 4

Muda wa kupika: dakika 30
Idadi ya walaji: Watu 4
Idadi wa vitafunwa : Kiasi cha 8-10 inategemea na upana au umbo


Loweka kwenye dengu  kwenye maji kiasi cha lita moja kwa masaa 2 hadi 3 au mpaka utakapo ona zimeshameza maji na kulainika.



Hakikisha unazichuja na kuzikausha vizuri kama picha inavyoonyesha.



Weka dengu zako kwenye blenda ( food processor) pamoja na chumvi, tangawizi na pili pili ila sio lazima kama hutumii pili pili ingawa inaleta ladha ya kuchangamsha. 


Hakikisha unasaga mchanganyiko uwe na muonekano kama huo usiweke kabisa maji ila kama blenda yako unaona haiwezi kusaga sababu ya ukavu basi weka maji kidogo sana ili uweze kusaga na kupata mchanagnyiko mkavu kama huo.



Kisha chukua dengu zilizosagwa weka katika bakuli pamoja na kitunguu maji, majani ya gili gilani, majani ya curry pamoja na spinach pia unaweza nyunyizia ndimu kiasi kuongeza ladha sio lazima.



Hakikisha unachanganya vizuri sana.



Kata kidogo na kisha hakikisha unatengeneza umbo la kama mpira.



Tumia karatasi ya Plastic na uipake mafuta kisha weka ule mviringo wa machanganyiko wa dengu na spinach juu yake kisha tumia vidole vyako viwili na ukandamize.



Tumia kidole chako na choma kati kati upate umbo kama la doughnut. Ni jinsi ya kutengeneza umbo zuri lakini sio lazima!



Chukua sufuria au kikaango weka mafuta kisha pata moto wa wastani chukua ile mchanganyiko kisha weka katika sufuria na endelea kukaanga hakikisha mafuta ni moto wasatani ili isibabuke na matokeo yake haiivi ndani (med-hot).



Kumbuka kugenuza mara kwa mara mpka upate rangi hii nzuri ya kahawia.



Kisha toa na weka katika karatasi ili yapoe na kuchuja mafuta pia. Kama ulifata maelekezo vizuri basi itaiva vizuri na wala hazitakau na mafuta kabisa karatasi haitaloana mafuta kabisa.



Hakikisha unampatia mlaji haraka sana ikiwa bado inamoto kwani ndio inakua na ladha nzuri pia unaweza kula na- Coconut chutney, spicy tomato chutney au tomato ketchup! ni nzito sana ukila unashiba kabisa.


Hazipendezi kukaa kwenye friji zaidi ya siku moja zinapoteza ladha na ubora pia

 



MIMI NA FAMILAI YANGU HUWA NAPENDA KULA NA SPICE TOMATO KETCHUP NA TUNAFURAHIA SANA. NI RAHISI KUTENGENEZA NA FAMILIA ITAFURAHIA SANA KITAFUNA HIKI.