BISKUTI ZA UNGA WA NGANO NA VIAZI VYA KUCHEMSHA
MAHITAJI
480 unga wa ngano ( self raising unapatikana katika maduka mengi tu)
3 kijiko kikubwa cha chakula siagi au butter, iache wazi katika joto la chumba ili iyeyuke
5 gram chumvi
1 kijiko kikubwa cha chakula fresh dill ichop chop vizuri kabisa ( sio lazima)
2 viazi vikubwa ( vichemshe katika maji moto kisha viponde ponde)
3 kijiko kikubwa cha chakula maziwa ya maji
3 kijiko kikubwa cha chakula siagi au butter, iache wazi katika joto la chumba ili iyeyuke
5 gram chumvi
1 kijiko kikubwa cha chakula fresh dill ichop chop vizuri kabisa ( sio lazima)
2 viazi vikubwa ( vichemshe katika maji moto kisha viponde ponde)
3 kijiko kikubwa cha chakula maziwa ya maji
JINSI YA KUANDA FATILIA PICHA NA MAELEOZ HAPO CHINI
Muda wa maandalizi : Dakika 30
Muda wa mapishi : Dakika 30
Idadi ya biscuti : Kiasi cha biscuti 20 mpaka 25
Chukua unga wako weka katika bakuli safi na kavu kisha washa oven kwa moto wa 450F.
Kisha changanya siagi, chumvi, unga na majani ya dill, Hakikisha unachanganya vizuri na ichanganyike safi kabisa.
Kisha chukua vile viazi vya kupondwa pondwa na uchanganye katika unga pamoja na maziwa ya maji na uhakikishe inachananyika vizuri kabisa.
Kwa kukanda pole pole na kwa umakini kwa dakika 5 tu utaona mchanganyiko wako upo safi kabisa na muonekano ndio huu.
KIsha unaanza ku roll kwa kutumia mpini huo mchanganyiko wako wa unga hakikisha juu ya meza unayosukumia umeweka unga wakutosha ili mcnganyiko uweze sukumima vizuri na usinatie kwenye meza.
Kisha kata maumbo aina yeyote upendayo kwa kutumia cutter.
Baada ya kukata hakikisha unatoa miduara yako na kuiweka pembeni kisha unaliunganisha lile unga lililobakia na kusukuma tena na unendelea zoezi la kukata kisha unarudia zoezi hili mpaka utakapo malizia mchanganyiko wa unga wote.
Paka kwa juu mafuta katika tray unayotaka kuokea kisha ziweke biscuti juu yake na uchome katika oven. Kwa wale wanaopenda sukari basi vunja mayai kwa pembeni au unaweza tumia maziwa ya maji na ukatukmia brush unapaka yale mayai au maziwa kwa juu ya biscuti kisha unanyunyizia sukari kwa juu na biscuti zako zikiiva zitakua na ladha ya sukari.
Kisha choma katika oven kwa dakika 20 mpaka 25 au mpaka zitakapo kua na rangi ya kahawia.
Ni rahisi sana au sio? Kitafunwa safi kabisa mhhh , Kitafuna hiki kitakuafanya kila ukipita karibu yake unatupia mdomoni kipande kimoja au viwili.
Muonekano safi kabisa wa biscuti hizi na unaweza zihifadhi kwa muda mrefu kwa matumizi ya baadae na bila ya kuharibika.
Sio lazima uweke dill unaweza hata kutumia maji ya machungwa, maganda ya limao, au ladha ya vanila.
WAANDALIE FAMILIA YAKO WAFURAHIE KITAFUNWA HIKI RAHISI KW AKUANDA NA GHARAMA NAFUU.
Mbona pishi hili (biskuti za viazi) halina maelekezo ya mahitaji,tafadhali tuwekee.Asante
ReplyDelete