Wednesday, June 20, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA CHAPATI KWA KUTUMIA AINA KUMI NA TANO ZA NAFAKA PAMOJA NA MCHELE WA KAHAWIA


JIFUNZE KUTENGENEZA CHAPATI YA AINA YAKE KWA KUTUMIA NAFAKA ZA AINA 15 PAMOJA NA MCHELE WA BROWN, NI TAMU SANA NA FAMILIA ITAFURAHIA SANA
 
MAHITAJI
 
240 gram mchele wa Brown
240 gram nafaka aina 15  Mchanganyiko
2 pilipili nyekundu kavu
1 Tangawizi osha na umenye
120 gram tui la nazi, nazi ya pakiti au kopo inafaa
majani ya Curry kwajili ya ladha
majani ya giligilani kwajili ya ladha
5 gram chumvi

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAFUNZO HAPO CHINI


Muda wa maandalizi : Masaa 8 hadi siku 1
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 5
 


Picha inaonyesha mchanganyiko wa nafaka kiswahili chake ni kigumu lakini ukiangalia katika picha unaweza jua pia n a sio lazima uweke aina zote 15 unaweza tumia hata aina 5 na ikafaa majina ya nafaka hizo kwa kiingereza ni dried beans, peas, and lentils : Northern, Pinto, large Lima, Yellow eye bean, garbanzo, baby Lima, Green Split Pea, Kidney, cranberry bean, small White, Pink bean, small red, yellow split pea, lentil, navy, white kidney, black bean.

 
Loweka nafaka zote katika bakuli 1 kisha loweka mchele wa brown katika bakuli jingine loweka kwa usiku mzima.

 
Kesho yake asubuhi, Chuja maji vizuri

 
Kisha chukua nafaka zote na uziweke katika food processor/ blenda.

 
Weka tui la nazi pamoja na chumvi, majani ya gili gilani na majani ya curry kisha saga

 
Hakikisha umesaga vizuri kisha mimina katika bakuli pembeni
 
 
Kisha chuja mchele wa brown mimina katika processor ilie ile uliotumia mwanzo kusagia nafakla wala usihangaike kuiosha

 
Saga mpaka upate kimiminika.

 
Kisha chukua mchanganyiko wa zile nafaka changanya na mchanganyiko wa mchele.

 
Hakikisha mchanganyiko wako unachanganyaika vizuri na kisha ikiwa nzito unaweza ongeza maziwa au maji kiasi upate kimiminika kizito cha wastani.

 
Kuongeza ladha na sio lazima kama unapenda unaweza kuongezea kitunguu maji chop chop na pili pili ya kijani.

 
Chukua kikaango kisafi na mwagia mafuta kwa juu kisha kata kitunguu nusu na tumia kusambaza mafuta katika kikaango chako

 
Mwagia unga kati kati ya kikaango.

 
Chukua kijiko na kisha tumia kusambazia pole pole ukitengeneza mduara
 
 
Hakikisha unaweka mduara safi na mwembamba ili chapati yako iwe laini na kavu pia.

 
Ukishaona inaanza kua ya kahawia unatakiw akuigenuza
 
 
Hakikisha unatumia moto wa kati  na choma chapati yako kwa dakika 5 au 6 tu iwe imeiva pande zote 2
 
 
Kumbuka kunyunyizia mafuta tu kila unapomaliza kugeuza ili upande ambao haujaiva nao uive uwe wa kahawia na kunukia harufu safi sana
 
 
Unaona inavyopendeza na ni kavu na laini safi kabisa
 
 
Chapati hii inapendeza sana kula ikiwa yamoto, pika kiasi tu ili mlaji aweze kula ikiwa fresh na yamoto kwa matumizi yajayo tafadhali weka unga huu katia friji na unaweza kuutumia hata baada ya wiki 1 waandalia wateja hotelini au nyumbani famia wafurahie kitafunwa hiki.
 
 


SALAD YA NYANYA NA CHEESE


KWA WALE WOTE WAPENZI WA SALAD NAIMANI MCHANGANYIKO HUU MRAHISI NA NAFUU WA SALAD MTAUPENDA SANA KWANI MAHITAJI YOTE NI RAHISI SANA KUPATIKANA. JINA MAARUFU INAITWA TOMATO AND MOZARRELA SALAD.

MAHITAJI
 
460 grams nyanya nzuri za kuiva
230 grams fresh Mozzarella cheese
60 gram majani ya Basil
3 kijiko kikubwa cha chakula Extra Virgin Olive Oil
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga 
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi: dakika 30
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 3


Mimi binafsi huwa napenda dsana kutumia cherry tomatoes zinamuonekano safi sana na zinaladha safi sana.

Nyanya zikate nusu kwa urahisi wa kutafuna


Kisha kata na mozarella cheese vipande vidogo

 

Mimina na Changanya katika bakuli moja


Mwagia chumvi na pili pili manga

Picha hapo chini mwagia Extra Virgin Olive Oil hakikisha mafuta haya ya olive unaweka tu wakati unataka kumaptia mlaji.

Hakikisha unaweka mafuta wastani

kisha weka majani ya basil na uchanganye pole pole



Huu ndio muonekano halisi wa salad yako ni vizuri kama utapata nyanya zenye rangi tofauti kama nyekundu na njano kwa ulaya ni rahisi sana kupatikana kwa miji mikubwa nyumbani kama dar au Arusha ukienda kwenye supermaket kubwa utazipata aina hizi za nyanya au uliza cherry tomato.


Unaweza kula kama starter au mlo kamili ukiwa na mkate kwa pembeni. Waandalie familia au wageni hotelini watafurahia sana.