KWA WALE WOTE WAPENZI WA SALAD NAIMANI MCHANGANYIKO HUU MRAHISI NA NAFUU WA SALAD MTAUPENDA SANA KWANI MAHITAJI YOTE NI RAHISI SANA KUPATIKANA. JINA MAARUFU INAITWA TOMATO AND MOZARRELA SALAD.
MAHITAJI
460 grams nyanya nzuri za kuiva
230 grams fresh Mozzarella cheese
60 gram majani ya Basil
3 kijiko kikubwa cha chakula Extra Virgin Olive Oil
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Muda wa maandalizi: dakika 30
Muda wa maandalizi: dakika 30
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 3
Mimi binafsi huwa napenda dsana kutumia cherry tomatoes zinamuonekano safi sana na zinaladha safi sana.
Nyanya zikate nusu kwa urahisi wa kutafuna
Kisha kata na mozarella cheese vipande vidogo
Mimina na Changanya katika bakuli moja
Mwagia chumvi na pili pili manga
Picha hapo chini mwagia Extra Virgin Olive Oil hakikisha mafuta haya ya olive unaweka tu wakati unataka kumaptia mlaji.
Hakikisha unaweka mafuta wastani
kisha weka majani ya basil na uchanganye pole pole
Huu ndio muonekano halisi wa salad yako ni vizuri kama utapata nyanya zenye rangi tofauti kama nyekundu na njano kwa ulaya ni rahisi sana kupatikana kwa miji mikubwa nyumbani kama dar au Arusha ukienda kwenye supermaket kubwa utazipata aina hizi za nyanya au uliza cherry tomato.
Unaweza kula kama starter au mlo kamili ukiwa na mkate kwa pembeni. Waandalie familia au wageni hotelini watafurahia sana.
Jamani ni nini shida Chief au huoni watu wanavyocomment kwamba hamna recipts in picha tu?
ReplyDeletesamahani kaka, haujaweka maelezo jinsi ya kuandaa salad hii
ReplyDelete