Monday, November 12, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI KWA KUTUMIA UTE MWEUPE TU WA YAI NA KUONGEZA LADHA KWA SAUCE YA STRAWBERY

 RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII YA KUTUMIA UTE MWEUPE TU WA YAI NA KUONGEZWA LADHA KWA KUTUMIA SAUCE YA STRABERY
 
       MAHITAJI
    Kwajili ya Cake
    400gram sukari, igawe kidogo
    1/4 kijiko cha chai chumvi
    240 gram unga wa ngano special wenye amira yake, kama ukitumia unga wa kawaida basi weka baking powder kijiko kidocgo cha chai 3
    12 pc mayai tenga ute mweupe tu
    60 ngram maji ya vugu vugu
    1 kijiko cha chai Vanilla
    1 na 1/2 cha chai cream
    Kwajili ya strawberry Sauce
    4 kilo ya mchanganyiko wa strawberries, raspberries, blackberries, blueberries) & cherries pamoja na 200 gram Asali kwa ladha. Chemsha katika moto wa wastani kwa saa 1 kisha saga katika blenda iache ipoe na itakua tayari kuliwa
     
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi: 30 dakika mpaka saa 1
Muda wa mapishi Dakika 30
Idadi ya walaji :  Watu 6
 
 
Muonekano wa mayai safi

 
Washa oven moto 350 degrees F. Chukua vijiko 3 vyachakuala sukari changanya na chumvi pamoja na unga wa ngano kisha chuja katika chujio

 
Kisha changanya vizuri na baking powder.

 
Hakikisha unalitenganisha vizuri ute wa njano na ute mweupe ukikosea tu kidogo basi unaharibu kabisa na yai fresh linatengana vizuri.

 
Tumia bakuli la shaba aua la chuma kabisa kwa ubora wa kazi yako usitumie bakulai la aluminum au la mabao hautapata matokeo mazuri kabisa.

 
Tumia mchapo au whisk, kwenye bakuliu weka ute mweupe wa yai, maji, vanilla , ana fresh cream.

 
Endelea kuchapa na baada ya dakika mbili utaona mapovu,

 
Kisha hamishia kwenye mashine au hand mixer.

 
Pole pole mwagia sukari iliyobakia,tumia mashine kuchapa moja kwa moja katika speed ya wastani.

 
Huu ni muonekano baada ya kupata povu la wastani usipige kwa muda mrefu sana 

 
Kisha chukua unga wa ngano ulichangany.wa na mwagia katika povu lako la mayai

 
Tumia spatula au mwiko kuchanganya pole pole. endele mpaka unga uchanganyike vizuri.

 
Tumia kijikjo kuchota mchanganyiko pole pole pia kumbuka pan unayotakiwa kutumia ni kama hiyo hapo katika picha maana hilo bomba kati kati inasaidia eki isishuke pia usipake mafuta pan maana cake za sponge huwa zinatabia ya kushika pana nandio inaweza kupanda juu vizuri.

 
Baada ya kumimina usiitingishe pan yako na weka katika oven tayari kwa kuchoma.

 
Choma katika ove kwa dakik 35 kisha tumia kijiti kwa kuchoma ndani ya keki inatakiwa kitoke kisafi kikiwa na uji uji basi ujue keki ni mbichi.

 
Chukua tray na weka juu ya pan uliochomea keki baada ya kuiva.

 
KIsha igeuze juu chini na uiache ipoe kwa muda wa saa1 kwani ukiitoa mapema itapondeka na kuharibika.
 
 
Kawaida keki hii huwa inashika kwenye pana hivyo ikishapoa igeuze tena kichwa chini miguu juu na utumie kisu kupitisha pembeni ili uiachanisha.

 
Kumbuka kupitisha kisu na kati kati pia

 
Igeuze chini juu tena na pitisha kisu kwenye kitako pia

 
Toa kitako cha pan. Sasa keki ipo tayari. Bahati mbaya keki yangu ilikamata kidogo kwachini lakini nimejitahidi kuitoa vizuri nawe jitaidi pia kama itatokea

 
  Kata kipande cha keki na mwagia sauce ya strawberries
 
 
Niamini, hii spongy cake na mchanganyiko wa sauce hiyo na ukiwa na matunda yenyewe du ndio unapendeza hasa kama ukikosa matunda basi nunua sauce ipo katik maduka ya chakula supermarket.

 


JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA KAROTI NANASI NA TANGAWIZI

 
JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI SAFI KABISA YA NANASI TANGAWIZI NA KAROTI NI RAHISI SANA NA PIA INAONGEZA SANA HAMU YA KULA KWA MTOTO AU MTU MZIMA AKIWA AMEPOTEZA HAMU YA KULA.
 
MAHITAJI
 

1 450 grams au nanasi 1 kubwa
50 gramsTangawizi osha na menya
1 Carrot ya wastani osha menya katakata vipande vidogo
5pc Ice cubes 
 
FATILIA MAFUNZO NA JINSI YA KUANDAA KATIKA PICHA HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : Dakika 15
Muda wa mapishi : Dakika 15
Idadi ya walaji : Watu 2
 
 
Huu ni muonekano wa vyakula vyako

 
Menya nanasi kisha toa ile sehemu ngumu ya kati kisha kata kata vipande vidogo.

 
Baada ya kukata kata nanasi vipande vidogo kisha kata karoti na tangawizi na weka katka bleda au  (or juicer).

 

Saga vizuri ilainike na kisha chuja kwa chujio.

 
Chuka vipande vya barafu na weka katika bakuli safi ulilochuja ili ipoe na uweze mpatia mnywaji.

 
WATENGENEZEE FAMILIA WAFURAHIE KINYWAJI HIKI SAFI WAKATI HUU WA JOTO KALI SANA NA HASA KWA WALE WAVIVU WA KUNYWA MAJI HII NI NJIA MOJA WAPO YA KUZOEA NA KUJIFUNZA KUNYWA MAJI
 


Monday, November 5, 2012

PISHI LA KEKI TOKA KWA CHEF RUKIA MTINGWA

NIMEFURAHI SANA KUPOKEA PICHA YA CHAKULA TOKA KWA CHEF WANGU RUKIA MTINGWA MAPISHI SAFI KABISA YA KEKI NA RECIPE ALIJIFUNZA TOKA KWA BLOG HII NAOMBA HUU UWE MFANO WA KUIGWA KWA WENGINE NAOMBA MNITUMIE PICHA ZA MAPISHI YENU MAZURI NITAFURAHI SANA.
 
 
 
Muonekano wa keki baada ya kuiva

 
huu ni muonekano wa keki baada ya kukatwa laini na tamu kabisa kwa muonekano tu

 
safi sana chef Rukia naimani familia walifurahia sana sana
 
 

PICHA ZA PISHI LA BAMIA TOKA KWA CHEF LILIAN ISAACK

 
NIMEFURAHI SANA KUPOKEA PICHA YA CHAKULA TOKA KWA CHEF WANGU LILIAN ISAACK MAPISHI SAFI KABISA YA BAMIA NA RECIPE ALIJIFUNZA TOKA KWA BLOG HII NAOMBA HUU UWE MFANO WA KUIGWA KWA WENGINE NAOMBA MNITUMIE PICHA ZA MAPISHI YENU MAZURI NITAFURAHI SANA.
 
 
 
Huu ni muonekano safi kabisa wakati wa maandalizi kabla ya kupika
 

 
Huu ni muonekano safi kabisa wa bamia baaa ya kuiva tayari kwa mlaji kuendela kufurahia
 
SAFI SANA CHEF LILIAN