Monday, November 12, 2012

JIFUNZE KUTENGENEZA KEKI KWA KUTUMIA UTE MWEUPE TU WA YAI NA KUONGEZA LADHA KWA SAUCE YA STRAWBERY

 RECIPE SAFI KABISA YA KEKI HII YA KUTUMIA UTE MWEUPE TU WA YAI NA KUONGEZWA LADHA KWA KUTUMIA SAUCE YA STRABERY
 
       MAHITAJI
    Kwajili ya Cake
    400gram sukari, igawe kidogo
    1/4 kijiko cha chai chumvi
    240 gram unga wa ngano special wenye amira yake, kama ukitumia unga wa kawaida basi weka baking powder kijiko kidocgo cha chai 3
    12 pc mayai tenga ute mweupe tu
    60 ngram maji ya vugu vugu
    1 kijiko cha chai Vanilla
    1 na 1/2 cha chai cream
    Kwajili ya strawberry Sauce
    4 kilo ya mchanganyiko wa strawberries, raspberries, blackberries, blueberries) & cherries pamoja na 200 gram Asali kwa ladha. Chemsha katika moto wa wastani kwa saa 1 kisha saga katika blenda iache ipoe na itakua tayari kuliwa
     
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi: 30 dakika mpaka saa 1
Muda wa mapishi Dakika 30
Idadi ya walaji :  Watu 6
 
 
Muonekano wa mayai safi

 
Washa oven moto 350 degrees F. Chukua vijiko 3 vyachakuala sukari changanya na chumvi pamoja na unga wa ngano kisha chuja katika chujio

 
Kisha changanya vizuri na baking powder.

 
Hakikisha unalitenganisha vizuri ute wa njano na ute mweupe ukikosea tu kidogo basi unaharibu kabisa na yai fresh linatengana vizuri.

 
Tumia bakuli la shaba aua la chuma kabisa kwa ubora wa kazi yako usitumie bakulai la aluminum au la mabao hautapata matokeo mazuri kabisa.

 
Tumia mchapo au whisk, kwenye bakuliu weka ute mweupe wa yai, maji, vanilla , ana fresh cream.

 
Endelea kuchapa na baada ya dakika mbili utaona mapovu,

 
Kisha hamishia kwenye mashine au hand mixer.

 
Pole pole mwagia sukari iliyobakia,tumia mashine kuchapa moja kwa moja katika speed ya wastani.

 
Huu ni muonekano baada ya kupata povu la wastani usipige kwa muda mrefu sana 

 
Kisha chukua unga wa ngano ulichangany.wa na mwagia katika povu lako la mayai

 
Tumia spatula au mwiko kuchanganya pole pole. endele mpaka unga uchanganyike vizuri.

 
Tumia kijikjo kuchota mchanganyiko pole pole pia kumbuka pan unayotakiwa kutumia ni kama hiyo hapo katika picha maana hilo bomba kati kati inasaidia eki isishuke pia usipake mafuta pan maana cake za sponge huwa zinatabia ya kushika pana nandio inaweza kupanda juu vizuri.

 
Baada ya kumimina usiitingishe pan yako na weka katika oven tayari kwa kuchoma.

 
Choma katika ove kwa dakik 35 kisha tumia kijiti kwa kuchoma ndani ya keki inatakiwa kitoke kisafi kikiwa na uji uji basi ujue keki ni mbichi.

 
Chukua tray na weka juu ya pan uliochomea keki baada ya kuiva.

 
KIsha igeuze juu chini na uiache ipoe kwa muda wa saa1 kwani ukiitoa mapema itapondeka na kuharibika.
 
 
Kawaida keki hii huwa inashika kwenye pana hivyo ikishapoa igeuze tena kichwa chini miguu juu na utumie kisu kupitisha pembeni ili uiachanisha.

 
Kumbuka kupitisha kisu na kati kati pia

 
Igeuze chini juu tena na pitisha kisu kwenye kitako pia

 
Toa kitako cha pan. Sasa keki ipo tayari. Bahati mbaya keki yangu ilikamata kidogo kwachini lakini nimejitahidi kuitoa vizuri nawe jitaidi pia kama itatokea

 
  Kata kipande cha keki na mwagia sauce ya strawberries
 
 
Niamini, hii spongy cake na mchanganyiko wa sauce hiyo na ukiwa na matunda yenyewe du ndio unapendeza hasa kama ukikosa matunda basi nunua sauce ipo katik maduka ya chakula supermarket.

 


6 comments:

  1. sasa tufatilie mapishi hata vipimo hakuna wala sioni faida ya kuangalia picha bila maelezo

    ReplyDelete
  2. MBONA NAONA NI PICHA TU HAMNA MAELEZO YOYOTE YA RECIPES ZAIDI YA UTE WA YAI NA UNGA.....HII NI IDEA NZURI SANA YA KUWA NA BLOG KAMA HII,PIA FUNGUA NA FACEBOOK/TWITTER AKAUNTI WATU WAWEZE KULIKE HII BLOG....ILA MAELEZO(INSTRUCTIONS) NA HATUA(STEPS) NI MUHIMU SANA.PIA UNAWEZA FUNGUA DUKA LA RECIPES ZA MAPISHI MBALIMBALI/VIFAA MBALIMBALI VYA MAPISHI KWA HIYO UNAPOELEZEA JINSI YA KUPIKA CHAKULA,UNAWAELEZA WATU RECIPES WANAWEZA PATA DUKANI KWAKO....WATANZANIA WENGI HAWAJUI MAPISHI KWASABABU HAWAJUI WAPI PA KUPATA RECIPES HIZO ZAIDI YA SUPERMARKETS THAT WAY NAWEWE UTAENJOY MATUNDA YA BLOG YAKO.

    ReplyDelete
  3. keki inatamanisha na inaonekana ni tamu sana,nitajaribu kuipika sema vipimo na mayai mangapi ndo itakua shida

    ReplyDelete
  4. Assalaam aleikhum sheikh. Naona tumepotezana. Nimekutumia e-mail, naomba unijibu.

    Yasini

    ReplyDelete
  5. tafadhali weka na maelezo chini ya picha

    ReplyDelete
  6. sasa mbonahujatuambia kama tunawka baking powder au hatuweki?

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako