HAPO CHINI NI KITAFUNWA CHA MCHANGANYIKO WA MBEGU ZA UFUTA NA UNGA WA NGANO.
MAHITAJI
MAHITAJI
240 gram maji ya vugu vugu
2-1/2 kijiko cha chai amira ya chenga
1-1/2 kijiko kikubwa cha chakula sukari
600 gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai chumvi
1 kijiko kidogo cha chai mafuta ya kula
1 kijiko kikubwa cha chakula mbegu za ufuta
1 Kitunguu kikubwa
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
Chukua bakuli safi kisha weka maji, amira ya chenga, na sukari. Iweke pembeni kwenye joto la kawaida kisha iache mpaka ianze kutoa mapovu ndani ya dakika 5.
Kisha mwagia unga pole pole na uchanganye kwa kutumia mwiko wa mbao pole pole pamoja na chumvi weka unga kidogokidogo huku ukichanganya mpaka mchanganyiko wako uwe safi kabisa( Ukipenda unaweza kuchanganya kwa kutumia mikono haina neno).
Baada ya kuchanganya safi kabisa huu ndio utakua muonekano. Hamishia katika sehemu uliyomwagia unga wa ngano hasa juu ya meza kisha endelea kukanda mpaka mchanganyiko uwe mgumu na usio nata katika mikono yako kwa dakika 5 tu, kama bado itakua laini unaweza kuongezea unga.
Chukua bakuli kavu kisha lipake mafuta ya wastani na weka humo ule mchanganyiko wa unga na funika kwa juu na karatasi ya nailoni ili kuongeza joto na isaidei kuumuka.
Ukifunika safi unga wako utakua umeshaumuka ndani ya saa 1 tu.
Baad ya kuumuka kata unga huu katika vipande sawa 6. Tengeneza katika umbo la duara na toboa kwa kidole kati kati kama muonekano katika picha. .Paka mafuta juu ya meza kisha weka hapo hiyo miduara na funika kwa kitambaa laini juu yake, acha mpaka iumuke ndani ya dakika 20 hadi dakika 30.
Chukua kikaango kikubwa au sufuria yenye maji mengi na kisha yachemshe yapate moto . Weka kijiko kimoja kikubwa chachakula sukari katika maji ya moto kwenye kikaango. KIsha tupia katika maji hiyo miduara ya unga uliyoandaa kwa dakika 1 kisha geuza upande mwingine kwa dakika 1 tena.
KIsha toa na weka katika baking sheet au baking tray ambayo umeipaka mafuta.
Kwasababu imetoka katika maji moto hapa unaweza mwagia juu chochote unachopenda wewe mimi nilitumia ufuta lakini pia unaweza weka hata karanga au korosho.
Oka katika ovena yenye moto tayari kwa dakika 5 hadi 10 hakikisha imekua ya kahawia safi kabisa au golden/crusty on the surface. Muda wa kuoka unategemea oven na oven inaweza kuchukua hata dakika 20 pia. Kipimo cha kujua sasa imeiva hakikisha upande wa chini wa kitafunwa hiki unakua mkavu na wa mgumu kabisa na rangi ya kahawia.
KIsha toa katika ovena na acha ipoe juu ya wire rack. Kitafunwa hiki ni maarufu san kwa upande wa nchi ya marekani.
No comments:
Post a Comment
Tunaheshimu sana maoni yako