NI RAHISI SANA ENDAPO UTAFATA MAELEZO VIZURI KWANI HAIITAJI UTAALAMU SANA NA INAMUONEKANO NADHIFU SANA
MAHITAJI
1 lita ya fresh cream
1 pc tikiti maji kubwa
250 gram ya matunda aina ya blue berry(unaweza tumia zabibu za bluu au nyekundu mbichi)
250 gram ya zabibu mbichi za kijani
250 gram pia unaweza tumia korosho au karanga za kuoka
250 gram pia unaweza tumia machicha makavu ya Nazi
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
1. Kama muonekano ulivyo katika picha kwanza kata pande zote mbili za tikiti maji kwenye kitacho chini na juu.
2. Menya kwa mtindo wa duara pole pole hata ganda likikatika hamna neon cha msingi tikiti liwe safi na mviringo.
3. chukua cream fresh piga piga kwa kutumia mashine au mchapo mpaka ie nzito kabisa.
4. Chukua crema fresh uliyokwisha piga pakaza kuzunguka sehemu zote za tikiti maji lako hakikisha hamna sehemu hujapaka cream ya kutosha.
5. Mwagia karanga au korosho au machicha ya Nazi makavu kwa upande wa pembeni.
6. Kisha juu yake panga matunda hayo inategemea msimu na unamatunda gani unaweza weka aina yeyote ile ya matunda kwajuu ilimradi upate muonekano wa rangi tofauti toka katika aina ya matunda uliyonayo au uliyoyapenda.
HII NI NJIA BORA SANA YA KUWASHAWISHI WALE WOTE WASIOPENDA KULA MATUNDA IWE MTU MZIMA AU MTOTO WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE.
kitu kimetulia mnooooooo hongera sana kaka Issa
ReplyDelete