Saturday, November 16, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA KWA UMARIDADI NA UFASAHAA KIFUA CHA KUKU

KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA YA KUTENGENEZA KIFUA CHAKUKU

MAHITAJI
1 kijiko kidogo cha chai Kosher Salt
1 kijiko kidogo cha chai Freshly Ground Black Pepper
1 kijiko kidogo cha chai Onion Powder
1 kijiko kidogo cha chai Garlic Powder
1 kijiko kidogo cha chai Dried Parsley Flakes

JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Changanya viungo vyote kwa mara moja kisha mwagia juu ya vifua vya kuku

Ukitaka upate harufu na ladha safi toka katika viungo hivi hakikisha umeasha moto na kikaango kipate moto wa kutosha kisha mwagia mafuta yakupikia yakutosha na mwagia pia viungo vilivyobakia kwenye kikaango kisha weka hivyo vifua vyakuku na upunguze moto uwe wa wastani.

Chukua mfuniko funika ila acha wazi kiasi kama muonekano kwenye picha lengo ni kupunguza mvuke isiwe kama tunachemsha badala ya kukaanga. Kaanga kwa dakika 3 kisha geuza upande wa pili uweze pata rangi ya kahawia nzuri.
 
Baada ya kugeuza upande wa pili huu ndio muonekano wake na kisha pika pia kwa dakika 3 na kifua cha kuku kitakua kimeiva. Kumbuka unapogeuza upande wa pili toa na mfuniko usifunike tena.

Huu ni muonekano wa perfectly cooked and seasoned chicken breast baada ya kukata ndani inakua laini na ladha safi kabisa sio kau kau na kupoteza ladha.


KIfua hiki cha kuku mimi na familia yangu tulikula na mchanganyiko wa parachici, slice za vitunguu, slice za nyanya mbivu limao na giligilani mhhhhhh safi sana.
 
NDANI YA DAKIKA 10 CHAKULA TAYARI
 

No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako