Saturday, December 7, 2013

JIFUNZE KUTENGENEZA PANCAKE SAFI NA NZITO KWAJILI YA KITAFUNWA

RECIPE SAFI KABISA YA PANCAKE NZITO NA SAFI KWA KITAFUNWA CHA ASUBUHI, MCHANA AU JIONI
 
MAHITAJI
240 gram unga wa ngano
3 kijiko kikubwa cha chakula sukari (white sugar)
1/2 kijiko kidogo cha chai Baking Soda
1/2 kijiko kidogo cha chai Baking Powder
1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
360 gram cups fresh cream
1 pc yai
kijiko kikubwa cha chakula butter  au (Siagi)
kijiko kikubwa cha chakula vanilla 
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
Chukua bakuli safi kavu kasha changanya unga wa ngano, sukari, chumvi, baking powder na baking soda.

Kisha chukua bakuli nyingine safi na kavu kasha changanya pamoja mayai, vanilla essence, siagi na fresh cream kama huna unaweza tumia maziwa badala yake.

Kisha chukua mchanganyiko wa mayai na maziwa mwagia kwenye mchanganyiko wa wa unga na koroga pole pole. Kisha weka pembeni acha kwa dakika 5 hadi 10 sio lazima lakini kama ukiweka kwa muda huo itulie pancake yako itatoka vizuri sana.

Chukua non stick pan, mwagia mafuta kiasi hakikisha jiko lako halina moto mkali au moto mdogo . Medium heat is perfect for pancakes. chukua kijiko kikubwa au upawa mmoja chota na mwagia katika kikaango.

Ukitaka kujua recipe umeipatia au jiko lako linamoto safi basi utaona  holes au bubbles zinatokea kwa juu sasa ujue ndio na muda wa kugeuza umefika igeuze pancake yako. Kawaida inachukua kama 50 sekunde mpaka dakika.

Turn the pancakes when golden brown and let it cook for another few seconds or until done.

Angalia pancake ilivyochambuka safi sana na nzito ukila unashiba

Hapa familia lazima ijiume videle bwana


Tumia kitambaa kizito au towel kuzifunika wakati unaendelea kupika ili zibaki na moto kwani zinapendeza kuliwa zikiwa za moto wakati wa kula unaweza mwagia maple syrup oooooh ladha yake itakua baabkubwa (a must! Dont even think of skipping it) and feel heaven coming down :) Pia unaweza kutumia chocolate sauce au strawberry syrup.

3 comments:

  1. santee sana chef.chapati maji hizi ni chakula nikipendacho sana sana nyumban na pia mie uwa naweka kidogo iliki niloitwanga uwa naingia jikoni mwenyewe kupika siku iyo.familia inajilamba sana

    ReplyDelete
  2. yan nimejaribu hiii ni nzuri na tamuuu..

    ReplyDelete
  3. mimi naomba unifundishe kupika keki ya kawida kabisa ila sina oven natumia gas na jiko la mkaa je itafaa kunifundisha kutumia mkaa? na ikiwezekana unifundishe na kupamba.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako