Tuesday, July 22, 2014

JIFUNZE KUTENGENEZA MCHUZI MZITO WA BILINGANYA MAALUMU KWA KULA NA NYAMA CHOMA

 MCHUZI MZITO WA MBOGA AINA YA BILINGANYA MAALUMU KWA KULA PAMOJA NA UGALI AU WALI NA NYAMA CHOMA INAPENDEZA SANA
 
MAHITAJI
 1 kg Bilinganya
1 kitunguu maji kikubwa
4 nyanya kubwa mbivu
5 vipande vya kitunguu swaumu
50 gram ya tangawizi
1 kijiko kidogo cha chai jeera
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa manjano au tumeric
1/2 kijiko kidogo cha chai pili pili ya unga
1 kijiko kidogo cha chai unga wa Coriander
1 kijiko kidogo cha chakula Garam Masala
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
2 majani ya curry
majani ya korienda kidogo
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Mimi nilitumia bilinganya 3 ambazo zinatimia 1 kilo. weka foil katika tray ya kuokea kisha zipake mafuta bilinganya

 
Hakikisha unatoboka kwa kutumia uma matundu haya yatasidia moto kupenya kwa haraka na kuivisha bilinganya hii.

 
na uweke kwenye oven yenye moto..Inaweza chukua dakika 20 mpaka 30 inategemea na moto wa oven yako. hakikisha kila baada ya dakika tano unageuza iweze kuiva pande zote.

 
Wakati bilinganya inaendelea kuiva chop chop kitunguu kwa umakini upate vipande vidogo dogo sana kuboresha mchuzi wako.

 
Washa jiko katika moto wa wastani kisha weka kikaango. weka mafuta ya kupikia kisha weka jeera mpaka ianze kupasuka , kisha weka kitunguu swaumu, kitunguu maji na tangawizi pamoja na ,majani ya curry, chumvi na pili pili manga endelea kupika.

 
baada ya vitunguu kulainika na kutoa harufu safi ya kunukia ongeza nyanya na uongeze moto kiasi ili nyanya iweze kuiva kwa haraka.

 
Kuongeza moto kutafanya nyanya zianze kuiva na kutengeneza mchuzi mzito. kama nyanya zilikua hazikuiva vizuri unaweza nyunyizia maji kiasi kusaidi kuzilainisha na kutengeneza mchuzi mzito.

 
Endelea kukorogo na kuponda ponda nyanya zilainike na kufanya mchuzi uwe laini.

 
kisha punguza moto na uweke viungo vyote vilivyobakia

 
changanya mpaka ichanganyike vizuri.

 
funikia kisha endelea na kuandaa bilinganya iliokua inaiva kwenye oven

 
Angalia bilinganya zimeiva safi kabisa na zimelainika iache ipoe mpaka utakapoweza kuzishika.

 
Kisha anza kumenya ngozi ya bilinganya pole pole. Sababu ya mafuta uliyozipaka kabla ya kuzioka kwenye oven ndio yanasaidia kumenya ngozi kwa urahisi sana

 
Tumia uma na ponda ponda bilinganya iliyokwisha menywa.

 
kisha chukua bilinganya uliyokwisha iponda pamoja na mchuzi wake na uweke kwenye mchuzi wa nyanya uliokwisha iva.

 
Koroga ichanganyike vizuri kisha onja nini kinapungua na unaweza kuongezea ili uweze kupata ladha safi kabisa. Baada ya kuhakikisha ladha ipo safi unaweza kufunika na mfuniko ili iendelee kuiva na kuchangayika vizuri kati ya mchuzi ya nyanya, viungo pamoja na bilinganya yako.

 
Pika kwa dakika chache tu kisha toa na unaweza pakua mpatie mlaji ikiwa yamoto. unaweza kula pamoja na mkate, viazi, ugali , wali au chapatti na ukafurahia sana

 
Mimi binafsi huwa anapenda sana kurushia kitunguu maji chop chop vibichi na majani ya korienda kwa juu inaongeza ladha safi sana

Tuesday, July 15, 2014

JIFUNZE MBINU MPYA YA KUPIKA MAPISHI AINA YA CURRY NA MAYAI YA KUCHEMSHA

 
JIFUNZE JINSI YA KUPIKA CURRY KWA MBINU MPYA KWA MAPISHI TOFAUTI
 
MAHITAJI
  • 240 gram mtindi halisi ( yoghurt)
  • 2 kijiko kikubwa cha chakula unga wa dengu
  • 240 gram maji masafi
  • 3/4 kijiko kidogo cha chai Turmeric powder
  • 1 kijiko kidogo cha chai pili pili nyekundu ya unga
  • 5 gram chumvi
  • 1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kula
  • 1 kijiko kikubwa cha chakula samli sio lazima kama hupendi tumia siagi
  • 1 kijiko kidogo cha chai  Cumin seeds au jeera
  • 2 vitunguu maji chop chop
  • 3 vipande vya kitunguu swaumu visage 
  • 8 majani ya Curry
  • 8 au 10 mayai ya kuchemsha (Hard Boiled Eggs)
  •  
    JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
     
     
    Tumia mchapo kwa kupiga mtindi au Yogurt

     
    Mpaka ilainike kabisa kama unavyoona kwenye picha.

     
    Kisha weka kwenye mtindi unga wa dengu, Turmeric, pilipili ya unga nyekundu na chumvi.

     
    Piga piga mpaka ichanganyike vizuri kabisa.

     
    Kisha ongeza maji na endelea kupiga piga mpaka ichanganyike vizuri kabisa 

     
    Baada ya kuchanganyika vizuri weka pembeni uendelee na atua nyingine

     
    Chukua kikaango kisha weka katika jiko lenye moto na umimine mafuta ya kupikia pamoja na samli.  Mafuta yakipata moto weka jeera na ikianza kupasuka ongeza vitunguu maji na kitunguu swaumu.

     
    Hakikisha unakoroga mpaka kitunguu kiwe laini, ongezea majani ya curry na uendelee kupika kwa dakika 2. Punguza moto uwe wa wastani

     
    Endelea kukoroga na pole pole mimina ule mchanganyiko wa mtindi na viungo. Hakikisha ulipunguza moto ili kuhakikisha mtindi hauungulii kwa chini.
     
     
    Wakati inaendelea kuiva, menya mayai na uweke pembeni. mimi nilitumia mayai 10 in this recipe but 8 should be good enough for 4 people normally.

     
    Hakikisha unaendelea kukoroga mara kwa mara. Zoezi hili linachukua muda kwani unatakiwa kua mvumilivu pika kwa dakika 20 mpaka chuzi wako uwe mzito, unaladha ya kuiva na rangi safi ya njano, tastes cooked and looks yellow.

     
    Onja tafadhali uone kama inatakiwa chumvi zaidi. Unaweza ongezea sukari kijiko kimoja kidogo cha chai kubalance test safi  .

     
    koroga vizuri ichanganyike.
     

    Kisha weka mayai na acha ichemke kwa dakika 5.

     
    Mpatie mlaji ikiwa yamoto pamoja rushia kwa juu majani yakijani ya vitunguu maji na giligilani au koriander.  unaweza kula pamoja na wali, mkate au chapati

    
     
     MUONEKANO SAFI KABISA WA CHAKULA HIKI
     
    1. kwa nyama ya ngombe, mbuzi, kondoo, kuku au samaki unatakiwa kuichemsha kwanza iive vizuri kasha una ichanganya kayika mchuzi huu wakati tulioweka mayai na uache ichemke kwa dakika 10 ili nyama ipate ladha ya mchuzi na viungo.
     
    WAANDALIE FAMILAI YAKO WAFURAHIE
     

    Tuesday, July 1, 2014

    JIFUNZE KUTENGENEZA PIZZA KEKI


    MUDA SI MREFU KAA TAYARI JIFUNZE KUTENGENEZA  PIZZA KEKI
     
    MAHITAJI

  •  480 gram unga wa ngano
  • 2 sukari kijiko kikubwa cha chakula
  • 1 kijiko kikubwa cha chakula Baking Powder
  • 1 kijiko kidogo cha chai Dried Basil
  • 1 kijiko kidogo cha chai chumvi
  • 1/2 kijiko kidogo cha chai Baking Soda
  • 240 gram Cheddar cheese kata cubes
  •  180 gram mtindi halisi
  •  60 gram maziwa ya maji
  • 4 ute mweupe wa yai
  •  60 gram siagi iliyoyeyushwa
  • 120 gram mchanganyiko wa kitunguu, pilipili hoho, nyanya na bilinganya chop chop
  • 60 gram Pizza Sauce
  • 120 Mozzarella cheese iliyokwaruzwa
  •  
    JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
     
     
    Washa moto wa oven nyuzi joto (200 C). Chukua bakuli kubwa safi na kavu kasha changanya unga wa ngano, sukari, baking powder, salt, basil and baking soda

     
    Changanya vizuri ichanganyike kasha tupia katika mchanganyiko wako vipande vya cheddar cheese.

     
    Chukua bakuli jingne na weka mtindi, ute mweupe wa yai na siagi piga piga mpaka ichanganyike vizuri.

     
    Chukua mchanganyiko wa mtindi na mayai kisha mwagia kwenye mchanganyiko wenye unga wa ngano.

     
    Hakikisha una changanya vizuri pole pole ichanganyike vizuri. Don't be too rough,

     
    hakikisha inachanganyika vizuri na unga wote umelowana kusiwe na unga mkavu au mabonge bonge.

     
    Tupia mboga majani na uendelee kuchanganya

     
    Sasa mchangayiko wako utakua mzito na safi kabisa

     
    Chota mchanganyiko wako na kisha weka kwenye muffin cups.  Hakikisha kabla ya kuweka mchanganyiko wako unapaka mafuta katika hizo cups ili pizza yako isishike baada ya kuiva.

     
    Chota pizza sauce 1 kijiko kidogo cha chai kisha weka juu ya kila moja wapo

     
    Mwisho unachukua ile mozzarella cheese ilyokwaruzwa na unamwagia kwa juu.

     
    Choma katika oven kwa dakika 20

     
    Choma mpaka upate rangi ya kahawia au mpaka ukichoma toothpick  katikati inatoka safi kabisa.  Kisha toa katika oven na iache ipoe kwa dakika 5 kabla hujazitoa kwenye tray uliochomea,

     
    Zikishapoa muonekano ndio huo weka juu ya mweza kisha anza kuzitoa moja moja.  Unaweza kuigandisha pizza hii kwenye freezer tumia an airtight container na inaweza kukaa kwa mwezi mzima; siku ukitaka kula basi toa kwenye freezer na yeyusha katika joto la chumba au  room temperature pole pole usitumie microwave.


    Ukikata kwa ndani muonekano ndio huu, safi sana waaandalie family wafurahie
     

    KAA TAYARI KWA KUPATA MAFUNZO YA CHAKULA KWA NJIA YA VIDEO

     
    MUDA SI MREFU KATIKA BLOG YA JAMII www.issamichuzi.blogspot.com UTAWEZA PATA MAFUNZO YA CHAKULA KUTOKA KWA CHEF ISSA KWA NJIA YA VIDEO KUPITIA Michuzi TV. VITAFUNWA VYA AINA MBALI MBALI UKIZINGATIA MWEZI HUU NI WA MFUNGO WA RAMADHANI like facebook page Active chef utapata update zoote za mapishi

    SOMA RECIPE MPYA ZIPO HAPO CHINI
     
     
    Je wajua kutengeneza breakfast burger?