Tuesday, July 22, 2014

JIFUNZE KUTENGENEZA MCHUZI MZITO WA BILINGANYA MAALUMU KWA KULA NA NYAMA CHOMA

 MCHUZI MZITO WA MBOGA AINA YA BILINGANYA MAALUMU KWA KULA PAMOJA NA UGALI AU WALI NA NYAMA CHOMA INAPENDEZA SANA
 
MAHITAJI
 1 kg Bilinganya
1 kitunguu maji kikubwa
4 nyanya kubwa mbivu
5 vipande vya kitunguu swaumu
50 gram ya tangawizi
1 kijiko kidogo cha chai jeera
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa manjano au tumeric
1/2 kijiko kidogo cha chai pili pili ya unga
1 kijiko kidogo cha chai unga wa Coriander
1 kijiko kidogo cha chakula Garam Masala
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
2 majani ya curry
majani ya korienda kidogo
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Mimi nilitumia bilinganya 3 ambazo zinatimia 1 kilo. weka foil katika tray ya kuokea kisha zipake mafuta bilinganya

 
Hakikisha unatoboka kwa kutumia uma matundu haya yatasidia moto kupenya kwa haraka na kuivisha bilinganya hii.

 
na uweke kwenye oven yenye moto..Inaweza chukua dakika 20 mpaka 30 inategemea na moto wa oven yako. hakikisha kila baada ya dakika tano unageuza iweze kuiva pande zote.

 
Wakati bilinganya inaendelea kuiva chop chop kitunguu kwa umakini upate vipande vidogo dogo sana kuboresha mchuzi wako.

 
Washa jiko katika moto wa wastani kisha weka kikaango. weka mafuta ya kupikia kisha weka jeera mpaka ianze kupasuka , kisha weka kitunguu swaumu, kitunguu maji na tangawizi pamoja na ,majani ya curry, chumvi na pili pili manga endelea kupika.

 
baada ya vitunguu kulainika na kutoa harufu safi ya kunukia ongeza nyanya na uongeze moto kiasi ili nyanya iweze kuiva kwa haraka.

 
Kuongeza moto kutafanya nyanya zianze kuiva na kutengeneza mchuzi mzito. kama nyanya zilikua hazikuiva vizuri unaweza nyunyizia maji kiasi kusaidi kuzilainisha na kutengeneza mchuzi mzito.

 
Endelea kukorogo na kuponda ponda nyanya zilainike na kufanya mchuzi uwe laini.

 
kisha punguza moto na uweke viungo vyote vilivyobakia

 
changanya mpaka ichanganyike vizuri.

 
funikia kisha endelea na kuandaa bilinganya iliokua inaiva kwenye oven

 
Angalia bilinganya zimeiva safi kabisa na zimelainika iache ipoe mpaka utakapoweza kuzishika.

 
Kisha anza kumenya ngozi ya bilinganya pole pole. Sababu ya mafuta uliyozipaka kabla ya kuzioka kwenye oven ndio yanasaidia kumenya ngozi kwa urahisi sana

 
Tumia uma na ponda ponda bilinganya iliyokwisha menywa.

 
kisha chukua bilinganya uliyokwisha iponda pamoja na mchuzi wake na uweke kwenye mchuzi wa nyanya uliokwisha iva.

 
Koroga ichanganyike vizuri kisha onja nini kinapungua na unaweza kuongezea ili uweze kupata ladha safi kabisa. Baada ya kuhakikisha ladha ipo safi unaweza kufunika na mfuniko ili iendelee kuiva na kuchangayika vizuri kati ya mchuzi ya nyanya, viungo pamoja na bilinganya yako.

 
Pika kwa dakika chache tu kisha toa na unaweza pakua mpatie mlaji ikiwa yamoto. unaweza kula pamoja na mkate, viazi, ugali , wali au chapatti na ukafurahia sana

 
Mimi binafsi huwa anapenda sana kurushia kitunguu maji chop chop vibichi na majani ya korienda kwa juu inaongeza ladha safi sana

2 comments:

  1. Weka maneno tafadhali pics are confusing!!

    ReplyDelete
  2. apo ule na ugali wa dona au udaga safi mno

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako