Saturday, September 27, 2014

JIFUNZE KUPIKA SUPU YA MAHARAGE AINA YA PINTO PAMOJA NA VIAZI ULAYA

 
JIFUNZE KUPIKA SUPU SAFI SANA YA MCHANGANYIKO WA VIAZI ULAYA NA MAHARAGE AINA YA PINTO
 
MAHITAJI
120 gram pinto beans au maharage ya kitenge
1 kitunguu maji kikubwa chop chop
2 pc za kitunguu swaumu saga
1 kiazi ulaya kikubwa kata kata vipande vidogo
 2 kijiko kikubwa cha chakula tomato paste au nyanya nzima 2
1/4 kijiko kidogo cha chai turmeric powder
1 bay leaf
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
majani ya korienda
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO
 
 
Loweka maharage yako kwa masaa 2 kwenye maji baridi kama utakua unaharaka unaweza kuyapika maharage haya kwenye pressure cooker

 
Baada ya kuyaloweka unaweza kuyapika kwa dakika 20 tu yatakua yameiva na baada ya kuiva hakikisha humwagi maji ya maharage hayo baada ya kuchuja

 
Chukua sufuria na kisha weka katika moto na uweke kijiko kimoja kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia, ikisha pata moto weka kitunguu maji, kitunguu swaumu, turmeric powder, bay leaf na pili pili hoho pamoja na chumvi kanga mapaka vilainike na kutoa harufu safi.

 
Kisha ongezea viazi ulaya pika kwa dakika 4 au mpaka vitakapokua laini. Baada ya kulainika viazi ongeza tomato pest na kumbuka kukoroga ili kila kitu kichanganyike.

 
Chukua yale maji yaliyobaki baada kuchemshwa pamoja na maharage weka kwenye mchanganyiko wako wa viazi na mboga majani unaweza ongeneza maji ya kawaida kidogo ili upate supu. Ikisha chemka tu ongezea maharage na pili pili manga acha ichemke dakika mbili itakua imeiva

 
Unapochemsha maharage hakikisha hayaivi yakapondeka kabisa yawe magumu, mpatie mlaji ikiwa bado ni yamoto na pamba kwa juu na majani ya korienda! Yum!

 
Unaweza maatia mlaji kwenye kikombe na bakupi na ukala pamoja na chapatti au makate na ukafurahia kabisa hasa kwa saubuhi au mchana.
 
 


Monday, September 22, 2014

JIFUNZE KUTENGENEZA SUPU SAFI KABISA YA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI

 
RECIPE SAFI KABISA YA KUPIKA SUPU YENYE MCHANGANYIKO WA LEEKS, BROCCOLI NA ASPARAGUS SAFI SANA KWA AFYA YA MLAJI
 
MAHITAJI
1 kitunguu kikubwa kichop chop
1 leek, isafishe vizuri kasha kata kata
2 viazi vidogo safika vizuri kasha kata kata na maganda yake bila kumenya
1 lita ya maji au unaweza tumia vegetable stock
1 bay leaf
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
500 gram Asparagus osha kisha kata kata 
500 gram broccoli osha katakata
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI
 
 
Chukua leeks, viazi ulaya, kitunguu maji na bay leaf kisha weka kwenye sufuria lenye maji au vegetable stock na funika chemsha kwa dakika 10.

 
Baada ya dakika 10 kisha weka broccoli na asparagus na uendelee kuchemsha

 
kisha punguza moto uwe wa chini na endelea kuchemsha kwa dakika  10min kumbuka kuweka chumvi na pili pili manga na uonje.

 
Toa kwenye jiko na uache ipoe kiasi baada ya hapo toa bay leaf weka pembeni na mimina mchanganyiko wako kwenye blender na usage.

 
Baada ya kusaga rudishia kwenye sufuria na uendelee kuichemsha kiasi kwa dakika 5 baada ya hapo unaweza mpatia mlaji na kwajuu ukapamba na majani ya giligilani na ukampatia mnywaji akafurahia sana.
 
 


JIFUNZE KUTENGENEZA VIAZI VYA LIMAO NA KITUNGUU SWAUMU

 
RECCIPE SAFI KABISA YA KUPIKA VIAZI ULAYA VYENYE MCHANGANYIKO WA LIMAO NA KITUNGUU SWAUMU
 
MAHITAJI
4 vikubwa viazi ulaya, osha vizuri
3 kijiko kikubwa cha chakula olive oil
2 kijiko kikubwa cha chakula juice ya limao
2 kijiko kikubwa cha chakula majani ya korienda au giligilani
4 kijiko kidogo cha chai kitunguu swaumu kilichosagwa
5 gram chumvi
5 gram pili pili manga
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

 
Osha vizuri viazi kasha kata vipande vine kwa kiazi kidogo na vipande sita kwa kiazi kikubwa kata kwa urefu kama inavyoonekana kwenye picha, watu wengi huwa menya maganda ya viazi lakini mimi simenyi naacha maganda ili nisipoteze virutubisho au nutrient zilizojaa kwenye ngozi.
 
 
Washa jiko katika moto wa kati kisha weka vijiko viwili vya mafuta yapate moto, mafuta yakishapata moto weka viazi vyako kwenye kikaango

 
Hakikisha viazi vyako vinakua na rangi ya kahawia pande zote na pika kila upande kwa sakika 5 hadi 6 ndio safi.

 
Punguza tena moto uwe wa kati ili usiunguze, kisha funika mfuniko na acha viendelee kuiva ili viwe laini kabisa na safi kwa mlaji.

 
Wakati huo huo chukua bakuli safi kavu na uchanganye mafuta ya olive vijiko viwili , juice ya limao, majani ya corriender au gili gilani, kitunguu swaumu, chumvi na pili pili manga. Hakikisha unachanganya vizuri.

 
Baada ya viazi kuwa laini, chukua ule mchanganyiko wenye mafuta na mwagia kwenye viazi hakikisha unachanganya pole pole bila kuvivunja.

 
Toa mfuniko na kasha endelea kuvipika kwa dakika 3 hadi 4. wakati mzuri ni pale unapomwagia ule mchanganyiko wa mafuta na kitunguu swaumu ooohh ghafla italipuka harufu safi ya kuvutia pia viazi vitakua na ngozi ya kukauka na yakuvutia kama unavyoona kwenye picha.

 
 Unaweza ongezea majani ya giligilani au korienda kwani pia inahusika sana kwenye kuongeza ladha ya viazi hivi
 
 
Viazi hivi ni maarufu sana kwa nyama choma au samaki choma au kuku choma waandalie familia au wateja hotelini kwako na watafurahia sana sana, ni niafuu na rahisi sana kuandaa.
 
 


Sunday, September 7, 2014

NAWASHUKURU SANA KWA KUNIUNGA MKONO NA TUMEFIKA WASHABIKI 1000 KATIKA FACEBOOK

 
NAWASHUKURU SANA KWA KUNIUNGA MKONO NA KWAKUIPENDA KAZI YANGU YA KUELIMISHA JAMII KWA MAPISHI NA CHAKULA BORA. UKURASA WA FACEBOOK UMETIMIZA MASHABIKI 1000 NI HATUA KUBWA SANA NA NINAWAOMBA MUENDELEE KU LIKE TUFIKE 2000 NA KUENDELEA.
 
KWA KUWAKUMBUSHA UKITAKA KUJIUNGA KWA URAHISI BONYEZA LINK HII 
                https://www.facebook.com/pages/Active-chef/509561519067534
KISHA MOJA KWA MOJA UTAFUNGUKA UKURASA WA FACEBOOK WA ACTIVE CHEF NA UTAWEZA PATA MAELEZO JUU YA MAFUNZO AU HABARI ZANGU ZOTE MARA MOJA
 
 
NAWATAKIA SIKU NA KAZI NJEMA ASANTENI SANA TUPO PAMOJA
 
CHEF ISSA

JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA MCHANGANYIKO WA TIKITI MAJI, LIMAO NA NAZI

 
PATA MBINU SAFI KABISA YA KUTENGENEZA JUISI HII SAFI NA MURUA YA MCHANGANYIKO WA TIKITI MAJI, LIMAO NA NAZI
 
MAHITAJI
 450 grams Vipande vya Watermelon vyenye ubaridi,
250 gram ya maji ya dafu au Nazi changa
1 limao kubwa
10 vipande vya barafu au Ice cubes,
Fresh Mint kwajili ya kupambia
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA MAELEZO NA PICHA HAPO CHINI
 
 
Kata nusu tikiti maji zuri lililoiva kama unavyoona kwenye picha kisha likate kate vipande na uweke kwenye friji vipoe kabla ya kutengeneza juisi yako
 
 
Chukua maji ya dafu, limao, vipande vya barafu na vipande vya tikiti maji kisha weka kwenye blender. Lengo la kuweka limao ni kuongeza na kubalance ladha. kama wewe ni mpenzi sana wa maji ya madafu unaweza ongeza zaidi ili ladha ya madafu isikike sana.
 

Blend vizuri mpaka vitu vyote vichanganyike safi kabisa.
 

 
 
Perfect drink for your summer, waandalie familia wafurahie pia kama unabiashara waandalie wateja wako wafurahie sana hasa kipindi hiki cha majira ya joto. kumbuka tikiti maji na dafu vyote vinasukari kwahiyo huna haja ya kuongeza sukari kabisa na ukafurahia kinywaji hiki murua.
 


JIFUNZE KUPIKA HUU WALI WA MCHANGANYIKO WA KOROSHO, MBOGA MAJANI MCHANGANYIKO NA UYOGA

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA NITAIWEKA LEO LEO
 
MAHITAJI
1 kilo ya wali uliopikwa 
360 gram ya mchanganyiko wa mboga majani
3 fungu la majani ya vitunguu kata kata
120 gram korosho mbichi
2 Garlic cloves
150 gram uyoga kata kata
1 tangawizi menya na kisha kata kata vipande vidogo
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia
2 kijiko kikubwa cha chakula Soy Sauce
5 gram pili pili manga
5 gram chumvi
1 fungu la celery kata kata vipande vidogo
1 kitunguu swaumu
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO JUU
 
 
Kufanya urahisi hasa kwasisi tunaoishi nje ya nchi baadhi ya mboga majani kuzipata fresh ni shida unaweza nunua mchanganyiko wa mboga majani uliogandishwa, yenye mchanganyiko wa carrots, beans, peas na corn.Hii itakuasaidia kuokoa muda wa kukatakata au kuandaa lakini ukipata fresh ni bora zaidi kwani nyumbani Tanzania kuna ubora utajiri wa mboza za majani.

 
Washa jiko liwe na moto mkali kisha weka kikaango pia weka mafuta yapate moto. Halafu tupia korosho kanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia

 
Kisha toa korosho weka pembeni katika kikaango hicho hicho kilichopata moto weka majani ya vitunguu maji, celery, kitunguu swaumu na tangawizi kanga kiasi ukishapata harufu safi wa kuiva kwa mboga ndani ya dakika moja tu.

 
Kisha tupia mchanganyiko wa mboga majani na uendelee kukaanga kwa dakika moja tu.

 
Kisha tupia uyoga uliokatwa katwa endelea kukaanga.

 
Kisha mwagia soya sauce pia unaweza ongezea na chili sauce kidogo kama unatumia.

 
Kisha tupia wali wako uliokwisha pikwa ukaiva na uendelee kukaanga

 
kisha weka chumvi na pili pili manga na uonje uangalie kama ladha inatosha

 
mwisho weka korosho na uendelee kukoroga changanya vizuri 

 
Hakikisha imechanganyika vizuri.

 
Chakula hiki kinajitosheleza hakikisha unampatia mlaji ale kikiwa cha moto pia hakipendezi kulala na kupashwa kinapoteza ladha na ubora. Unaweza kula kama kilivyo au unaweza kula na nyama choma, samaki wa kukaangwa au mchuzi mzito wa nyama hata maharage,

WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE NI RAHISI NA NAFUU SANA