Sunday, September 7, 2014

JIFUNZE KUPIKA HUU WALI WA MCHANGANYIKO WA KOROSHO, MBOGA MAJANI MCHANGANYIKO NA UYOGA

 
KAA TAYARI KWA RECIPE SAFI KABISA NITAIWEKA LEO LEO
 
MAHITAJI
1 kilo ya wali uliopikwa 
360 gram ya mchanganyiko wa mboga majani
3 fungu la majani ya vitunguu kata kata
120 gram korosho mbichi
2 Garlic cloves
150 gram uyoga kata kata
1 tangawizi menya na kisha kata kata vipande vidogo
1 kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya kupikia
2 kijiko kikubwa cha chakula Soy Sauce
5 gram pili pili manga
5 gram chumvi
1 fungu la celery kata kata vipande vidogo
1 kitunguu swaumu
 
JINSI YA KUANDAA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO JUU
 
 
Kufanya urahisi hasa kwasisi tunaoishi nje ya nchi baadhi ya mboga majani kuzipata fresh ni shida unaweza nunua mchanganyiko wa mboga majani uliogandishwa, yenye mchanganyiko wa carrots, beans, peas na corn.Hii itakuasaidia kuokoa muda wa kukatakata au kuandaa lakini ukipata fresh ni bora zaidi kwani nyumbani Tanzania kuna ubora utajiri wa mboza za majani.

 
Washa jiko liwe na moto mkali kisha weka kikaango pia weka mafuta yapate moto. Halafu tupia korosho kanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia

 
Kisha toa korosho weka pembeni katika kikaango hicho hicho kilichopata moto weka majani ya vitunguu maji, celery, kitunguu swaumu na tangawizi kanga kiasi ukishapata harufu safi wa kuiva kwa mboga ndani ya dakika moja tu.

 
Kisha tupia mchanganyiko wa mboga majani na uendelee kukaanga kwa dakika moja tu.

 
Kisha tupia uyoga uliokatwa katwa endelea kukaanga.

 
Kisha mwagia soya sauce pia unaweza ongezea na chili sauce kidogo kama unatumia.

 
Kisha tupia wali wako uliokwisha pikwa ukaiva na uendelee kukaanga

 
kisha weka chumvi na pili pili manga na uonje uangalie kama ladha inatosha

 
mwisho weka korosho na uendelee kukoroga changanya vizuri 

 
Hakikisha imechanganyika vizuri.

 
Chakula hiki kinajitosheleza hakikisha unampatia mlaji ale kikiwa cha moto pia hakipendezi kulala na kupashwa kinapoteza ladha na ubora. Unaweza kula kama kilivyo au unaweza kula na nyama choma, samaki wa kukaangwa au mchuzi mzito wa nyama hata maharage,

WAANDALIE FAMILIA WAFURAHIE NI RAHISI NA NAFUU SANA





1 comment:

  1. hakuna kitu napenda kama mchanganyiko huu,nitajaribu kuupika asa uyoga niuwekee

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako