Tuesday, December 29, 2009

CHEF ISSA PIA ANAPENDA SANA SOKA



Siku ya graduation Timu ya culinary aka machef tulikabidhiwa kombe la ushindi upande wa soka na mmatumbi nilipiga goli mbili safi na kuisaidia timu yangu kunyakua ubingwa mashindano yalikua ni ya pale shuleni tu kila idara walikua na timu yao.



 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Culinary kabla ya mechi wengine walikua wanapasha misuli




Chef Issa Akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya timu ya Uongozi wa hotel na matukio





Namshukuru mungu ilikua ni good time si mchezo maana kila baada ya tukio kinachofata ni misosi ya nguvu hapa ilikua BBQ night baada ya Sport day kumalizika spring mpaka summer jua huwa linazama saa 3 usiku



Hii ilikua kona ya salad na cheese kibao pamoja na nyama kavu



Hii ilikua kona ya vyakula vya mboga mboga



Na hapa haswa ndio ilikua ni BBQ yenyewe unachagua unachokitaka mpishi anarushia kwenye moto haraka naona wengi walipendelea kula mbavu za kondoo au sausage au hamburger steak na salad.




6 comments:

  1. Kaka kumbe na soka unatandika hahahahaha duh inapendeza sana

    ReplyDelete
  2. nimeona hilo BBQ mhhh full kujiramba

    ReplyDelete
  3. usisahau recipe zetu za chapati na makongoro hahahahahahaaaaa

    ReplyDelete
  4. very professional mpaka raha unapangilia na kinapangika na kinaeleweka na kinalika na kinatamanisha big up chef mzalendo kweli ni culinary chember nakuunga kwa mikono na miguu yote minne Mdau USA

    ReplyDelete
  5. chapait chapati chapati kweli kabisa wengine tukikaanga badala itoke kurasa inakuwa kama mtu unatafuna ngozi kama una mgeni ni aibu tunaomba hili pishi usichelewe kuliweka kwa kweli

    ReplyDelete
  6. Sasa,hizo hapo mwisho nahisi ndio hamburger steaks,sasa kama mimi niko uswahilini naziweka juu ya jiko la mkaa au?Na je hapa DSM naweza kuzipata wapi au ni lazima nitengeneze?kwa kweli hii blog itatusaidia wapenzi wa mamabo haya.
    KT

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako