Saturday, January 9, 2010

BISKUTI SAAFI ZA KARANGA

Namna ya kutengeneza biskuti safi za karanga na jam pia zinadumu kwa miezi 3 mpaka 6 zikiwa katika ubora safi wa kuliwa inategemea na usafi na utunzaji wako. Unaweza tumia aina yeyote ile ya karanga mfano almonds, ground nuts, wholenuts au pistacchio. pia ukiweza kuzichanganya hizi zote itapendeza zaidi.


Kina mama kwa chai ya saa 10 jioni mpatie mwanao au mzee biskuti hii na chai au kahawa utakua umefanya jambo la maana sana. Kwenye migahwa mnapowahudumia wageni walioagiza kahawa au chai tupu unaweza mpatie kipande hiki cha biskuti bila ya kumchaji kama motisha ili kuongeza hamasa na kumfanya mteja ajisikie kua yeye kweli ni mafalme na thamani ya pesa yake inatumika kihalali.


Biscuti hii sio gahli na ni rahisi sana kutengeneza na inakaa kwa muda mrefu sana.

Vitu vyakuandaa

Unga wa ngano gr 600
Sukari  gr 240
Kijiki kidogo cha chai robo chumvi
Karanga gr 200
Butter ( siagi) gr 240
Vijiki 2 vya chai vanilla ya maji
Mayai 2
Ganda la machungwa 2 lililokwaruzwa ( lemon zest)


Hatua za kutengeneza

Chukua sukari na siagi changanya pamoja

Baada ya kuchanganyika safi weka maganda ya limao, vanilla, chumvi, karanga na mayai.

Kisha weka unga wa ngano changanya uchanganyike safi kabisa toa weka katika friji kwa muda mchanganyiko wako upoe na uwe mgumu zaidi kwajili ya kutengeneza shape nzuri ya biskuti.





Baada ya mchanganyiko waku kukamilika na kua katika umbo gumu, chukua baking sheet au karatasi ya kuokea kama hauna basi tumia karatasi nyeupe ipake mafuta ya siagi yote ilowane utatumia kuokea na haita ungua kwenye oven yako. Kisha kata kipande kiasi na zungusha kwa mikono yakua miwili utengeneze umbo la duara kama mpira kisha ingiza kidole cha mwisho kidogo kati kati ya umbo hilo la duara utapata shimo dogo kisha panga biskuti hiyo kwenye tray ukisubiri hatua inayofuata.




Chukua kiini cha njano cha yai changanya na maji kidogo tu ili upate ute mwepesi kisha chukua brush na pakaza ute huo juu ya biskuti zako zote saafi kabisa.




Katika picha hapo juu ni mfuko wa nailoni ukiwa na mchanganyiko saafi wa matunda aina ya redcourant pia pembeni unaweza ona tunda hilo halisi mchanganyiko huo wa tunda utauweka katika lile shimo kwenye biskuti ilikuongezea ladha zaidi.




Tumia mfuko wa nailoni kuweka mchanganyiko huo wa ladha ya tunda unaweza weka ladha yeyote ile ya tunda ulipendalo au jam uwezo wako tu na bado biskuti itapendeza sana. kisha weka kwenye oven amabayo tayari inamoto wa watani choma kwa muda wa kisha toa weka pembeni zipoe.



Biskuti zetu zipo pembeni na zimeshapoa tayari kwa matumizi ya kula zikiwa na rangi safi ya kahawia na nyekundu ya redcorant.




muonekano huo hapo juu ni maumbo mbali mbali ya biskuti lakini zikiwa zinatumia njia na vipimo sawa vya uandaaji, tofauti yake ni jinsi yakukata kenye maumbile.

Hiyo yenye rangi nyeusi ni baada ya kuiva na kupoa unachovya kwenye chocolate iliyoyeyushwa kisha unaiweka biskuti yako pembeni tena ili ipoe na chocolate ishikevizuri.

Hiyo yenye rangi nyeupe, chukua ute mweupe wa yai piga na sukari nyeupe kiasi kidogo sana kisha utapata povu chukua na pakaza juu katika biskuti mbichi kisha choma itakapo iva itatoka na muonekano huo

Utapunguza gharama ya kuwanunulia watoto biskuti madukani kwani utengenezaji wake ni nafuu sana na unatengeneza nyingi zitakazo kaa kwa muda mrefu sana bila kuharibika wala kupoteza ubora.


3 comments:

  1. Chef vipi kimya kimezidi? Bado twala biscuti za karanga tu? Au umepata dharura?

    ReplyDelete
  2. I think waweza pia tumia hii njia kupika biskuti za aina zingine,,wengine karanga hapana kabisa

    2.sasa unalipwa kwa kutoa hii shule bure hivi apa bloguni?maana to me ili ni zinga la dili,,,

    ReplyDelete
  3. Salam chumvi na sukari na vitu viwili tofauti je chumvi haitajitokeza kwenye ladha ya mandazi?Naomba unipe maelekezo ya kupika mkate wa(Boflo)ukiikata unapata Slesi?Ni mzuri kula kwa BlueBand.

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako