Kila mmoja wetu anatambua ulaini na utamu wa nyama ya bata endapo utampika vizuri. Fatilia hapo chini maelezo jinsi ya kukata vipande hivyo vya nyama ya bata na jinsi ya kuitengeneza kwa mtindo safi kabisa, kama ni kwenye mgahawa basi wateja wakula mlo huo watajitokeza kwa wingi na kwa walaji wa nyumbani basi utakua umeongeza chaguo jingine katika ratiba yako ya chakula, pika kifua cha bata acha watu wale kisha muulize kila aliekula hii ni nyama gani utapata majibu mengi sana kuliko utavyotegemea kwa sifa na ubora wa nyama hii.
Huyo ndio bata mzima akiwa ameshachinjwa na kusafishwa vizuri kabisa
Hivyo ni vifua vya bata kwa muonekano wa pande mbili mbele upande wa ngozi na nyuma sehemu yenye nyama tupu bila mfupa.
Huu ni mguu wa bata ukiwa na mfupa na haujatolewa ngozi kwa upande wa pili.
Vitu vta kuandaa ni
Kitunguu swaunu 1 kisage vizuri
Kitunguu maji 1 kata vidogodogo sana
Chumvi na pilipili manga
Maji 100gr
Juisi ya chungwa 1
Asali ya nyuki vijiko 4 vikubwa vya chakula
Bay leaf 1
Oregano kijiko nusu kidogo
Rosemary kijiko nusu kidogo
Mafuta ya maji yakupikia 150ml
Zabibu kavu 150 gr
Kama inavyoonysha katika mtiririko wa kuandaa vitu vya kupika pamoja na bata wako nimesema mafuta ya maji ya kupikia tumia yeyote kulingana na uwezo wako
Chukua vitu vyote ulivyoandaa hapo juu weka katika bakuli kama unavyoona katika picha changanya kwa pamoja vyote.
Kisha weka nyama kwenye chocmbo kitakachotosha vizuri halafu mwagia juu ya nyama ya bata mbichi ule mchanganyiko wako safi usambaze kote.
Weka nyama yako ndani ya friji lenye nyuzi joto 4 hadi 5 kwa masaa mawili kuruhusu ule mchanganyiko wako uingie vizuri katika nyama.
kama hauna friji usiweke kwenye friza acha nje sehemu yenye hewa safi na sio joto kwa muda wa saa 1 ukiwa umefunika ili wadudu wasiingie.
Baada ya muda huo kupita chukua nyama yako ya bata weka katika kikaango chenye mafuta kiasi na moto wa wastani kaanga pande zote mbili pole pole na nyama itaiva vizuri sana ikiwa na ladha safi.
Ule mchanganyiko wako wa mwanzo wa viungo uliomuunga bata wako kabla ya kupika usitupe hifadhi pembeni kwajili ya kutengeneza mchuzi wa kula pamoja na nyama hiyo ya bata.
Kwa wale wasio penda mafuta unaweza choma nyama hiyo katika jiko la mkaa lenye moto wa wastani ili nyama hii iive taratibu isibabuke kama unavyoona hapo chini katika picha.
Hapo chini ni muonekano wa nyama ya bata ikiwa imeshaiva na kukatwa slice za wastani bila kuachanisha kifua hicho ili kisipoteze muonekano wake halisi.
Hapo chini ni muonekano wa ule mchanganyiko uliotumia kumuunga bata akiwa mbichi kabla ya kumpika.
Chukua mchanganyiko huo wote weka katika sufuria au kikaango, washia jiko moto wa wastani ili mchuzi huo uive pole pole pia ongezea na glass moja ya mvinyo mwekundu au ( Redwine).
Hapo chini ni chupa na kipimo ambacho ni glasi halisi ya wine
Red wine italeta harufu na ladha nzuri sana kwa wale wasiotumia pombe wawe na amani kwani pombe yote inabadilika kua mvuke na kuisha kabisa kinachobaki ni harufu nzuri na ladha ya zabibu iliyovundikwa.
Ikishakua nzito tafadhali toa katika jiko tayari kwa kusave sauce hii unamwagia juu ya bata au unaweka katika chombo kidogo unasave pamoja na nyama hiyo ya bata mlaji atajipimia kiasi cha sauce anachopenda.
Muonekano wa upangaji sahani hapo chini hii yote ni kumvutia zaidi mlaji na kukifanya chakula chako kionekane safi na salama.
Nyama hii ya bata unaweza savu na ugali, wali, viazi hata mihogo ya kuchemsha vyovyote upendavyo na utafurahia zaidi ikiwa umefata maelezo vizuri ya uandaaji.
Naimani mtakua mmefurahia sana mapishi haya ya nyama ya Bata. Ukifatilia toka mwanzo nimekua nagusia vyakula ambavyo watu wengi hawapendi sana kula aidha kwakukosa umaarufu au kwa kutokufahamu njia mbada ya kukipika ili kipendeze na kiweze kulika.
Tengeneza bata huyu na usimueleze mlaji kisha baada ya mlaji kula muulize anahisi nyama hii ni nyama gani? kuanzia hapo yule asiye mpenzi wa kula bata atakua mwanachama mzuri sana mama nyumbani unakua umeongeza idadi ya mabadiliko ya chakula nyumbani.
Kuna mdau alieuliza oregano ni nini? hapo chini ni picha ya spice inayoitwa oregano zinapatikana sana kila duka la chakula hapo nyumbani Tanzania na uliza kwa jina hilo hilo supermaket yeyote ile utapata natumai utakua umeifahamu na kwenda kuinunua na ni nafuu bei yake.
Mdau ulie uliza mbadala wa Redwine kwaruza ganda la limao au chungwa upate zile chenga chenga kijiko kimoja cha chai then weka katika mchanganyiko wako utapata harufu safi na ladha nzuri sana.
Asante kutuonyesha mapishi ya chakula ambacho tumekizoea.Asante sana utakuwa umetuwezesha kuboresha chakula hicho.
ReplyDeleteHellow Kaka Issa,
ReplyDeleteAsante kwa mapishi ya BATA, kwakweli nimefurahi kwani familia yetu tunapenda nyama ya bata na ndio kitoweo kwetu kikubwa kwani ndio tunaofuga kwaajili ya kitoweo.
Nina swli moja; hiyo Oregano nin nini?
Natumaini tutaendelea kupata vitu vizuri zaidi.
Hongeraaaaaaa sana.
Kazi njema.
Heloow kaka Issa,
ReplyDeleteNaomba utueleze jinsi ya kuandaa HALF CAKE.
Asante.
Anonymous wa pili hapo juu,Oregano ni kiungo ila nyumbani sijui km ipo kwani hupandwa zaidi Europe,mediterranean na s.n c.Asia,ila ipo km mint vile..natumai nimejaribu kukufahamisha.Then kwako kaka Issa can you tell us instead ya wine mtu waweza kutumia nini tena,najua ukiipika wine inakata hiyo harufu ila watu wengine hatuwezi hatakwenda kuinunua kwani ni dhambi..so any suggestion option yake itakuwa?Hope i aint a bother aight.cheers
ReplyDeleteAsante kwa kunijuza kuhusu Oregano,
ReplyDeleteSasa badala yake tutumie nini?
asante.
kama hujapata oregano basi usiweke viungo vingine ulivyoweka vinatosha kuweka ladha nzuri sana unaweza pika bata wako bado hatakama hujapata oregano.
ReplyDeleteChef Issa