FISH TERRINE
Mshangaze mgeni wako nyumbani siku utakapomualika kwa chakula cha mchana au usiku kwa kumpatia terrine hii safi kabisa ya samaki wakati akisubiri mlo kamili.
Chukua fileti ya samaki weka katika ubao iponde vizuri pole pole mpaka iwe bapa kama inavyoonekana katika picha.
Chukua fileti kiasi ya samaki kata vipande vidogo vidogo na ichemshe na limao kidogo kwenye maji ya wastani iive kisha chuja acha samaki peke yake weka pembeni ipoe na ule mchuzi weka pembeni upoe pia.
Kisha chukua zucchin ikate kwa urefu slice nyembamba sana kata nyingi zakutosha inategemea na ukubwa wa chombo utakachotumia kutengenezea terrine yako.
Chukua chombo ambacho ungependa kutengenezea terrine yako chenye mtindo wowote ule kama ni cha mviringo au mraba au pembe tatu kama hicho hapo juu, Kinaweza kua cha chuma au plastik inayostahimili moto.
Tanguliza clinfilm kwenye chombo chako, kisha panga slice za zucchin kwa kuzipandanisha kiasi usiache nafasi.
Baada ya hapo panga fileti ya samaki mbichi ambayo imeshapondwa ikawa flat kabisa.
Katika picha tunaona samaki iliyochemshwa katika kikaango ute mweupe wa yai na ute wa njao wa yai
Samaki iliyochemshwa imechanganywa na majani aina dill yamekatwa katwa vizuri yakawa madogo kabisa
Baada ya kuweka dill fresh ongezea ute wa yai mweupe ( mayai matatu yanatosha kwa samaki gramu 500) pamoja na cream mililita 200.
Weka chumvi na pili pili manga ilivichanganyike vizuri.
Weka katika mashine ya kusagia saga mchanganyiko wako mpaka uwe mzito kabisa sio kimiminika, kama hua mashine basi unaweza tumia mwiko kuponda mpaka mchanganyiko wako uwe mzito na safi.
Mchanganyiko wako uko safi kabisa kama unavyoonekana hapo katika picha ni mzito na umekamilika.
Kumbuka fileti yetu ya samaki ni rangi nyeupe ili tupendezeshe na kupata mchanganyiko safi wa rangi chukua safron ya njano weka katika mchanganyiko wako wa samaki.
Kisha chukua mchanganyiko wako wa samaki na uweke katika chombo ulichokiandaa kwajili ya terrine yako safi.
Kama unavyoona katika picha slice za zucchin na fileti ya samaki vimezidi katika chombo chetu cha terrine tutaona faida yake hapo chini.
Ukishamaliza weka mchanganyiko wako wa samaki ukatosha vizuri kabisa.
Chukua zile zucchin zilizozidi pamoja na fileti ya samaki funika kwa juu tayari utakua umeshapata umbo kamili la pembe tatu napia usisahau kufunika na ile clingfilm juu ya chombo chako cha kupikia terrine.
Pika kwenye stimer kwa dakika 30 hadi 45 kisaha itoe itakua imeshaiva vizuri na kua ngumu kabisa tayari kwa kuliwa.
Kama hauna stimer basi unaweza tumia sufuria weka chombo chako cha terine kisha weka maji katika sufuria yasizidi kile chombo chako cha kupikia terrine yawe nusu tu kisha chemsha kwa muda huo huo kumbuka kufunika sufuria yako wakati wa kuchemsha.
Baada ya kutoa katika stimmer weka pembeni terrine yako ipoe.
Ikishapoa toa katika chombo na iweke katika ubao wa kukatia muonekano utakua kama hapo juu unavyooona terrine yetu ipo tayari matumizi ya chakula.
Wakati wa kukata posheni unafata mikato ya zucchini ndio posheni moja kwa mlaji mmoja tu. pia unaona muonekano mzuri wa rangi 3 yeupe, kijani na najano.
Terrine hii ikishapoa unaweza ihifadhi katika friji kwenye ubaridi wa nyuzi joto 4 hadi 5 ikisubiri kuliwa pia inaweza kaa mwezi mzima bila kuharibika.
Wakati wa kusevu baada ya kukata posheni yako weka katika kisahani kidogo cha kikombe cha chai ili kiendane na ukubwa wa terrine yako.
Kumbuka mwanzo tuliweka pembeni ule mchuzi wa samaki, uchemshe changanya na cream, safroni ya njano, chumvi na pilipili manga pika kwa moto mdogo mapaka mchuzi huu uwe mzito kabisa.
Mwagia mchuzi huo juu kila unapo save terrine hii na unaweza pamba juu ya terrine hiyo na kitu chochote kile upendacho. Juu ya terrine hiyo nimepamba na vitunguu vya kukaanga vinasaidia kuleta harufu nzuri.
KUMBUKA KUA HUO SIO MLO KAMILI BALI NI KITIA HAMU WAKATI UNASUBIRI MLO KAMILI. RECIPE HIYO HIYO UNAWEZA TUMIA KWA KUTENGENEZA TERRINE YA KUKU AU NG'OMBE NA IKAPENDEZA SANA SANA.
Haya ndio majani aina ya dill,
Mdau alieuliza ule ute wa njano ule hauna kazi tena.
Kutengeneza slice za zucchin pia unaweza tumia kifaa kile cha kumenyea karoti au viazi utapata slice nzuri tu natumai wadau hapa nitakua nimejibu maswali yenu vizuri kabisa.
Nashukuru kwa kushare recipe zako nzuri. Naomba uzidi kushare zaidi
ReplyDeleteShukran chef Issa, ni mimi niliyeomba hizo finger foods, nakushukuru tena na tena, kwanza jinsi nilivyo mpenzi wa samaki, hii itanisaidia sana kutengeneza starter za samaki. Mungu akuzidishie ilmu, na akuondolee mabalaa.
ReplyDeleteMswahili in UK
kile kiini cha yai kimewekwa wapi? au hakitumiki?
ReplyDeletena hizi slice za zucchin kuna kitu maalumu cha kukatia? je nikitumia kile cha karoti naweza kupata slice km hizi?
Kijo
ASANTE SANA KWA MAPISHI, SASA HEBU TUWEKEE NA JINSI YA KUTENGENEZA NYAMA AINA MBALI MBALI NA KWA URAHISI. NA VIUNGO UNAVYOANDIKA JARIBU KUANDIKA KISWAHILI/KIZUNGU MAANA KUNA BAADHI YA VIUNGO UMEVIANDIKA SIDHANI KAMA HUKU KWETU AFRICA VIPO AU PENGINE VINA MAJINA MENGINE.
ReplyDeleteASANTE SANA
Tunashukuru sana kwa wazo lako zuri la kuanzisha blog, kwakweli utakuwa umetusaidia na sisi kuweza kuboresha ndoa zetu na vilevile kuweza kula vyakula vinavyorisha.umesoma na hukupenda kuwa mchoyo wa elimu uliyoipata,mungu akubariki sana ktk hilo.
ReplyDeleteNingependa kushauri uanze na vyakula vya kawaida ambavyo kila leo sisi waswahili tunakula ndiyo uendelee na vya kizungu ambavyo unadhani waswahili tunaweza kuvila,maana vingine haviliki waviweza wenzetu wazungu.hii itatusaidia kuboresha mapishi yetu ya kilasiku na kuanzisha mapishi mapya ambayo hatukuyazoea kuyapika kilasiku.
Nashukuru sana tutajitahidi kufuata je Dill ni majani gani naomba unisaidie ili twende sawa
ReplyDeleteKaka Isa, Hongera sana, COOKING IS MY PASSION, Though am not proffessional. NAOMBA TUTUMIE MAPSIHI MABLIMBALI YA NYAMA, CHONDE MAJINA YA RECIPE KWA KISWAHILI PLZ OR TUPE ALTERNATIVE ZA VIPATIKANAVYO BONGO.
ReplyDeletenakumegea hot topic ya kuanza nayo.
JINSI YA KUANDAA HEALTH FOOD YA MTOTO ASIYEPENDA KULA FROM 1-5YRS.
Lim2217
kaka check spelling hii iko okay kweli, ipo chini ya picha yako
ReplyDelete"CULINARY CHEMBER"
lim2217