Saturday, January 2, 2010

ZIJUE SIFA NA JINSI YA KUPIKA UYOGA AINA YA PORTOBELLO



Huu ndio uyoga fresh unaoitwa portobello wengine wanautamka portobera matamshi yote ni sawa, Uyoga huu ni mbadala wa nyama kutokana na mapishi mbalimbali utakavyopenda kuupika. Fatilia picha na maelekezo jinsi ya kuupika hapo chini.




Andaa vitunguu, karoti, uyoga, pilipili hoho rangi yeyote ile sawa na vitunguu swaumu ( garlic) mboga zote hizo zikate katika saizi ndogo kama uonavyo katika picha.




Kisha safisha uyoga wako vizuri na ukate shina kwa chini kua muangalifu sana ni rahisi kuupasua uyoga na ukapoteza umbo lake halisi





Kisha tengeneza sauce rahisi kwajili ya kunyunyizia juu ya uyoga wako,

Chukua fresh basil, kitunguu swaumu, olive oil, chaives, chumvi, pilipili managa ya unga na balsamic vinegar.

Changanya vitu vyote hapo kama uonavyo katika picha kisha chukua brush chota sauce hiyo pitisha brush

kwenye uyoga ambao tayari upo katika tray ya kuokea katika oven.

Kama hauna brush basi tumia kijiko chota hiyo sauce na nyunyizia juu ya huo uyoga kisha weka pembeni kwa masaa 2 kuruhusu ile sauce iingie ndani ya uyoga na kuleta ladha nzuri.

Kisha weka katika oven kwa dakika 4 hadi 5 utakua tayari umeiva.




Wakati uyoga wako upo katika oven chukua ule mchanganyiko wa mboga ulizokata anza na mafuta tia katika sufuria au kikaango,

Kisha acha yapate moto wa wastani.

Weka vitunguu swaumu kaanga kidogo kisha weka mchanganyiko wa mboga zote zilizobaki. Kaanga kwa dakika 4 hadi 5 toa katika moto usisahau kunyunyiza chumvi kiasi.




Chukua mchanganyiko wako wa mboga majani uliokisha pikwa wastani Tumia kijiko kuchota mchanganyiko huo na weka juu ya uyoga wako.

Kisha chukua parmesan cheese iliyokwaruzwa vizuri nyunyizia juu ya mboga majani zilizopo juu ya uyoga.

Rudisha uyoga wako katika oven kwa dakika 2 au mpaka rangi ya cheese itakapobadilika kua ya kahawia ( brown).

Toa uyoga weka katika sahani bado ukiwa wa moto.



Huu tayari unakua ni mlo kamili na unaweza kula na hindi lakuchemsha au chips au viazi vyakuchemsha, ugali au wali. Kumbuka chakula kikiliwa chamoto kinakua na ladha nzuri sana.


PISHI LINGINE LA UYOGA AINA YA PORTOBELLO




Hatua za uaandaaji ni zile zile kama mwanzo.

Safisha uyoga wako vizuri kisha kata shina la chini na kua makini usiupasue uyoga wako ukapoteza umbo lake zuri.

Chukua  uyoga wako nyunyizia sauce kama ile ile ya mwanzo kisha uache uyoga masaa 2 ili sauce iweze kuingia ndani na kuleta ladha nzuri.

Baada ya hapo chukua uyoga wako na kuupitisha kwenye unga wa mkate uliokaushwa ( bread crumbs).

Baada ya hapo chukua uyoga wako weka katika kikaango chenye mafuta ya wastan na anza kukaanga.

Kwa wale wasiopenda mafuta mengi unaweza choma katika mkaa (BBQ) au ukaweka katika oven.

Baada ya muda ukishabadilika rangi ukawa kahawia iliyoiva sana ( Golden brown) utakua tayari umeshaiva.



Ulemchanganyiko wako wa mboga unaweza ukaubadilisha kwa kuongezea nyanya ya kopo na kua na mchuzi mzito.

Weka mchanganyiko wako wa mboga kwenye sahani kisha juu yake weka uyoga wako.

Juu ya uyoga weka kipande cha cheese yeyote ile chembamba kwakua uyoga ni wamoto toka jikoni cheese yako itayeyuka nakusambaa juu ya uyoga.

 kumbuka kusevu chakula hiki kikiwa bado kichamoto.


FAIDA UTAKAZOZIPATA KWA KULA UYOGA AINA YA PORTOBELLO

Wataalamu wa chakula na afya wanashauri kwa kila chakula tunachokula kila siku angalau kiwe na mchango wa 10% mpaka 20% za nutrients kwa siku.

Kwa kila gramu 100 za uyoga wa portobello kuna
Calories 26
Protein 2.5 gramu
Carbohydrate 5.1 gramu
Mafuta kwa ujumla 0.2 gramu
Fiber 1.5 gramu


Kwakula uyoga wa portobello katika mapishi mbali mbali utakua umejiwekea uhakika wa afya bora na kinga ya mwili wako kwa kuongeza madini ya potassium, selenium na niacin. Licha ya kufaidi utamu wa chakula hiki ambacho ni maarufu sana na wasifu wa uyoga huu unafaninishwa na nyama. Familia jitaidini sana kuwabadilisha wale wote wasiopenda kula mboga za majani kwa kuandaa vyakua vyenye mvuto.

No comments:

Post a Comment

Tunaheshimu sana maoni yako