Mkate wa mchele mwekundu
Mkate wa mchele pori
Mahitaji
540gram unga mweupe wa mchele
240 gram unga wa kahawia wa mchele
1 kijiko kidogo cha chai gelatin isiyo na ladha
3 Sukari kijiko kikubwa cha chakula
1 1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi
2 kijiko kikubwa cha chakula corn starch
120 gram maziwa ya unga
2 1/4 kijiko kidogo cha chai amira ya chenga
3 mayai
1 kijiko kidogo cha chai vinegar
3 Kijiko kikubwa cha chakula cha mafuta ya alizeti au ya karanga au ya mahindi chaguo lako.
12omls maji ya vugu vugu (110 degrees F/45 degrees C)
Maelekezo ya Upikaji
Changanya unga wa mchele mweupe, unga wa mchele wa kahawia na chumvi. Changanya vizuri sana uchanganyike kabisa katika bakuli moja.
Chukua bakuli nyingine changanya gelatin isiyo na ladha, sukari, corn stach, maziwa ya unga, mayai yaliyopigwa, vinegar na mafuta changanya mapaka ichanganyike vizuri zaidi.
Kisha Changanya ulemchanganyiko wa unga na ule mchanganyiko wa bakuli la pili lenye mayai na maziwa pia weka amira ya chenga iwe changanya vizuri mpaka upate mchanganyiko wa kati sio kimiminika kama mchanganyiko wa keki na sio ngumu kama mchanganyiko wa mkate kama bado nzito tumia maji salama ya baridi kiasi ili kulainisha mchanganyiko wako.
Weka katika sufuria au chombo maalumu kwa kuokea chenye urefu wa inchi 9 na upana wa inchi 5 acha katika joto la chumba mchanganyiko wako uvimbe na kua mara mbili ya ulivyokua mwanzo. washa oven yako katika joto la 325 Degree F au sawa na 165 degree C mpaka mkate wako utengeneze gamba gumu la kahawia saafi. Kisha toa mkate wako katiak oven uache kwa dakika 10 katika chombo ulichopikia kisha utoe uache nje katika joto la chumba kwa dakika tano kisha mkate wako uko tayari kwa kuliwa.
FURAHIA NA FAMILIA YAKO KWA KUBADILISHA LADHA YA MKATE PIA KWA WALE WENYE MATATIZO WASIO TUMIA NAFAKA ZENYE GLUTEN MTAKUA MMEFAIDIKA PIA MAKATE HUU UNAWEZA UKAUBADILISHA LADHA TOFAUTI KWA KUONGEZEA VITU MBALI MBALI KAMA ZABIBU KAVU, STRAWBERY, KARANGA, MBEGU ZA MABOGA, MBEGU ZA ALIZETI, MBEGU ZA UFUTA.
Asante sana Chef Issa. Tulimiss sana hizi recipes.
ReplyDeleteNitajaribu huu mkate na nitakutumia majibu.
Ila je Hii Gelatin ni kitu gani. Je kuhusu vinegar, naweza kutumia rice vinegar au yeyeote?
Mama Jeremiah
Asante kaka kwa pishi la mkate ,si unajua siku hz na hasa ughaibunikila kitu unatumia mashine kama una bread maker utatengenezaje huu mkate maana ile huwa kazi ni kumimina tu vitu kisha yenyewe inachanganya ,sasa naona kama michanganyiko ni mingi kwa bread maker naona kama nitaharinu ,asante
ReplyDelete