Ndugu zangu watanzania kinywaji hiki ni dawa ya mafua safi kabisa unatumia siku moja tu unakua na nafuu kabisa ila dozi yake inataka utumie mwezi mmoja hadi mwezi mmoja na nusu mfululizo bila ya kuacha.
MAANDALIZI
Chukua maji lita moja
Chukua asali vijiko 3 vikubwa vya chakula
Chukua tangawizi ya unga kijiko kimoja kikubwa cha chakula au chukua tangawizi mbichi itwange upate mchanganyiko uliopondeka kijiko kimoja kilichojaa.
Chemsha mchangyanyiko wako wote huo kwa pamoja mpaka ichemke vizuri inategemea na moto wa jiko lako lakini mpaka utakapoona imechemka vizuri usiache ikakaukia jikoni nashauri dakika 15 hadi 20 inatosha.
Kisha iache ipoe kunywa nusu glasi mara tatu kwa siku yaani asubuhi , mchana na usiku.
Kwa wale walio na mafua sugu yanadondoka muda wote na kupiga chafya nyingi sana zisizo na idadi basi zitakata mara moja na siku ya pili zitaisha kabisa kumbuka kunywa dawa hii mwezi mzima au hadi miezi miwili utapona kabisa.
Asante kaka hii itanisaidia sana. Kwani sasa hiyo kitu ukishaitengeneza unaweka kwenye fridge au maana mwezi mzima au unakuwa unatengeneza kila siku au kila wiki kwa mwezi mzima?
ReplyDeleteHi
ReplyDeleteasante kwa hili maana mie nina mafua ya alergy napiga chafya zaidi ya kumi kwa mpigo mpaka naskia kizunguzungu nahisi hii itanisaidia sana
Ehhh Asante sana brother Issa yani mimi ninasumbuliwa na mafua kwa muda mrefu sasa "allergy". yananinyima raha usiku nikilala ndio nabanwa kabisa naanza kukwaruza koo. Am going to try is as from today na am sure 100% am going to get rid of my cronic discomfort. Thanx alot na ubarikiwe sana
ReplyDeletesafi kaka, big up and happy vacation in dar
ReplyDeleteasante sana kaka,hii itanisaidia sana kwani huku nilipo na hii baridi mafua hayaishi.kazi njema!
ReplyDeleteThank you big boss
ReplyDeleteOle wako nisipone mafua niliyonayo utanikoma
ReplyDeleteKaka tunaomba recipe ya SAMBUSA JAMANI, I cant wait to cook for my kids, za kununua barabarani siziamini sana na zina viungo sana. Please help
ReplyDeleteLim2217
Kaka tunaomba recipe ya SAMBUSA JAMANI, I cant wait to cook for my kids, za kununua barabarani siziamini sana na zina viungo sana. Please help
ReplyDeleteLim2217
kaka niliomba recipe ya biriani siku nyingi,nisaidie kwa hilo tafadhali,sijui kabisa kulipika na natamani ningejua hata leo...lipe kipaumbele tafadhali,zaidi sana wewe ni kiboko katika mambo ya maakuli.
ReplyDeleteAsante sana Chef Issa.
ReplyDeleteJe hiki kinywaji unaweza kumpa mtoto? hii ninauliza kwa haya mafua ya kawaida yanayowapata watoto.
Nitashukuru sana.
Mama Jeremiah