Monday, February 22, 2010

JINSI YA KUPIKA WALI WA BIRYAN YA KUKU, NG.OMBE AU MBUZI

Mahitaji
1 kilo mchele wa basmati mrefu

1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.

1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)

1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana

240 gram ya mafuta ya kupikia

240 gram ya samli au mafuta yeyote ya kupikia

2 maggi chicken soup cubes

3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu

1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari (turmeric powder)

3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (coriander powder)

2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa (ginger-garlic paste )

50 gram korosho iliyo kaangwa usizisage zibaki nzima

50 gram majani ya girigilani (fresh coriander leaves, washed and chopped)

8-12 mbegu za nzima ya hiriki (green cardamoms)

4 bay leaves ( sifahamu kiswahili chake)

15 mbegu nzima ya pili pili manga (whole black peppercorns)

30 gram majani mabichi ya minti ( mint leaves )

salt kulingana na ladha yako binafsi

Jinsi ya kuanda

Weka mafuta katika sufuria yako iliyo juu ya moto tayari, kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemshwa mpaka iwe na rangi ya kahawia (golden brown)

Kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta ili mafuta yanayobaki weka kitunguu na endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa binzali, unga wa pili pili mwekundu, unga wa girigilani, bay leaves, mbegu za hiriki na nusu ya mbegu za pili pili manga.

Changanya vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzuri mkavu miminia humo maji uliyotunza baada ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe. kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuoneka kwa juu ndani ya sufuria.

Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria pole pole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama vikamate ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayopenda.

Chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu ilivyoslice kisha kaanga na majani ya girigilani, majani ya mint na korosho funika kwa dakika 10 picha inaonyesha hapo chini, kisha weka wali wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto maji yakisha kauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu tu juu ya wali wa basmati acha wali uive kabisa kisha itakua tayari kula na pakua chakula chako kikiwa cha moto



Wali wa pishori ( Basmati rice) uliokwisha iva


Wali wa pishori ( Basmati rice) uliokwisha iva ukakaangwa na vitungu na korosho


muonekano wa majani ya girigirani wakati wa kukaangwa


Nyama ya kuku iliokaangwa vizuri na viungo na nyanya ukapata mchanganyiko mzuri mzito





Muonekano halisi wa biriyani yako baada ya kuiva ikiwa imechanganyikana na nyama pia kumbuka kunamchuzi mzito na nyma ilibaki pembeni mlaji ataweza kujongezea kiasi apendacho.

Furahia chakula hiki pamoja na familia yako.





20 comments:

  1. mambo vipi Chef?kwanza kabisa shukrani kwa ili darasa unalotoa hapa yaani si mchezo naanza kuwashangaza rafiki zangu hapa ughahibuni kwa mapishi.Na ili la leo(biryani)nimekuwa nikijaribu for years ila wapi.sasa naona nitaweza sasa ila kuna uwezekano wowote wa kufanya recipes zisiwe nyingi hivyo?

    ReplyDelete
  2. Nashukuru sana kaka kwa kutimiza ombi langu,nitajitahidi nami nitoe biriani yenye mvuto kama hiyo yako ila nauliza hivyo vitunguu swaumu na tangawizi unachanganya wakati wa kupika hiyo nyama?maana hujahitaja wakati wa kupika na hayo majani ya mint na girigilani na bay ni lazima katika mapishi haya ya biriani, nasema hivi kwasababu mimi sijawahi tumia kabisa,korosho pia unaisaga ama unaweka nzima nzima?na kuna mahitaji umeyataja na hujayatumia kama samli na vingine.Ahsante kwa darasa hili la mapishi.

    ReplyDelete
  3. ndio unaweza ukaifanya recipe isiwe ndefu hivyo kwa kupunguza viungo au vitu usivyovipenda na wali wako utakua mzuri tu

    chef Issa

    ReplyDelete
  4. Vitu hivyo vyote ni muhimu sana lakini kama huvipendi unaweza kuvitoa tu bila shida na wali wako bado utakua mtamu tu pia korosho usizisage ziache nzima ukisoma kwasaa nimerekebisha na utaelewa zaidi

    chef Issa

    ReplyDelete
  5. Mambo vipi Chef Issa!! Yaani nasikia raha sana, hebu endelea kutupa MENU niendelee kufurahisha familia yangu.

    Hilda

    ReplyDelete
  6. apa ndipo napopataka mie asa iyo keki apo juu lolololl chef safiiii sana mbona umetuokoa wengine??

    endeleza kazi na kipaji iki kaka

    good work

    ReplyDelete
  7. Chef Issa, uko juuu ile mbaya. Tunaenjoy kinoma. Mi naomba nisaidie jinsi ya kutumia machine iitwayo 'sandwich maker'. Nimezawadiwa long lakini sijui kuitumia kutengeneza hizo sandwich. Najua kwa maelezo yako ntaelewa. So, Please, usiweke ombi langu kapuni.

    Mama George

    ReplyDelete
  8. week end hii ntaijiachia na biriani. lol, ahsante

    ReplyDelete
  9. s.a matumai umzima wa afya tele. birian zipo za aina nyingi je unaweza kutuonesha aina mabli mbali? mi nikipika napenda ile ya kuweka na maziwa ya mtindi inakuwa na ladha flan nzuri na kuwela mapapai yalo kunwa.hiyo picha ingekuwa inaliwa mhhhhhhhhhh

    ReplyDelete
  10. asant sana chef Issa, mungu akubariki kwa kazi hii yakutuelimisha.Nilipika biriani weekend iliyopita kwa kufuata maelekezo yako, kiukweli mume wangu alichanganyikiwa,chakula kilikuwa kitamu mno alishangaa sana.Alisema hii menyu ya Movenpick imetoka wapi.
    Hivyo tunashukuru kwakutuboreshea ndoa zetu,mungu akubariki sana.

    ReplyDelete
  11. Issa you rock..... hongera sana! Yaani I cant stop gettin impressed...

    ReplyDelete
  12. asante kwa maelekezo,je unaweza kutumia mchele wa kawaida kuandaa biryani hii?

    ReplyDelete
  13. asante kwa maelekezo,je unaweza kutumia mchele wa kawaida kupika biryani hii?

    ReplyDelete
  14. A. A ..Jazak Allah Kheir for sharing this..

    ReplyDelete
  15. mbona kila recipie ya biriani inakuaga na maziwa ya mtindi EXEPT hii ya kwako? elaborate pls m confused kidogo

    ReplyDelete
  16. This recipe is good but abit confusing. you dont explain when to add the garlic and ginger paste and when to add the remaining black pepper seeds.

    ReplyDelete
  17. This quite interesting. Should I try this at home. Kudos!

    ReplyDelete
  18. thanks for your intructions, now i will be able to prepare biriyan please contionue to give us good things, a lot of appreciation to you

    ReplyDelete
  19. I appreciate it..
    Home nmepewa Kazy ya kupika birian...
    I Just saw it pershally... I had no idea I had to Google and here I Am.I found this...Thank-you...
    And Am going to make them washangae...

    ReplyDelete

Tunaheshimu sana maoni yako